MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), ameendelea kugoma kula kwa siku ya tatu mfululizo tangu alipokamatwa Oktoba 26 mwaka huu, nyumbani kwake mjini hapa, akidaiwa kutoa maneno ya uchochezi.
Lema
alikamatwa siku hiyo saa 12 alfajiri akiwa nyumbani kwake, Njiro, na
hadi sasa anashikiliwa katika mahabusu ya kituo kikuu cha polisi mjini
Arusha.
Kutokana
na kuendelea kugoma kula, Wakili wake, John Mallya amesema leo saa sita
mchana atakwenda Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha kufungua kesi ya kutaka
mteja wake afikishwe mahakamani.
Malya
jana alisema katika kesi hiyo atashirikiana na Chadema kuwashtaki
mwendesha mashitaka mkuu wa Serikali na mkuu wa upelelezi wa makosa ya
jinai, Mkoa wa Arusha.
Tangu mbunge huyo akamatwe amegoma kula kwa kile anachodai kupinga udhalilishwaji aliofanyiwa na polisi wakati wa kukamatwa.
Pia, Lema anasema alinyanyaswa mbele ya watoto wake nyumbani kwake huku wakijua yeye ni kiongozi na amechaguliwa na wananchi.
Neema, mkewe Lema,jana alithibitisha kwamba mumewe amegoma kula.
“Anaendelea kugoma kula mpaka sasa kwa sababu hata sasa nimetoka polisi asubuhi kumpelekea chakula, lakini amekataa kula.
“Lakini nilipouliza pale polisi kuwa wanampeleka lini mahakamani, nilijibiwa wanaendelea kumhoji,”alisema Neema.
Juzi,
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, alithibitisha
kukamatwa kwa Lema na kueleza kuwa alihojiwa dhidi ya matamshi ya
uchochezi na kuwa atafikishwa mahakamani baada ya kukamilika
uchunguzi.
Kwa
mujibu wa Kamanda Mkumbo, Lema anatuhumiwa kuwachochea wakazi wa Arusha
kuandamana Septemba mosi, mwaka huu kuhamasisha kile kinachoitwa Umoja
wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta).
0 comments:
Post a Comment