Kamishna Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Nsato Marijan amesema kuwa mauaji yaliyotokea jana usiku katika benki ya CRDB Mbande Mbagala yanahusishwa na Operesheni UKUTA iliyotangazwa na viongozi wa vyama vya upinzani.
Marijan ameyasema hayo leo akizungumza na waaandishi kuhusu mauaji ya Askari wanne waliouawa jana usiku ambapo amesema kuwa viongozi wa vyama vya siasa wamekuwa wakihamasisha wafuasi wao kuwashambulia Maafisa wa Jeshi la Polisi hivyo kutokea kwa tukio hilo huenda kuna uhusiano na maneno hayo yanayotolewa.
Kufuatia hatua hiyo, Jeshi la Polisi nchini limepiga marufuku mikutano au vikao vyote vya ndani ya vyama vya siasa kutokana na matukio ya kihalifu kutokea.
Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi limekiri kuwa mazoezi ambayo yamekua yakifanywa na Askari wake katika maeneo tofauti tofauti ya nchi ni kwa ajili ya kukabiliana na waandamanaji Septemba Mosi na matukio mengine ya kihalifu.
Katika tukio la mauaji, Askari wanne waliuawa jana usiku na majambazi na kisha kutoweka na silaha na kwenda kuvamia kituo cha polisi na kuondoka na silaha pamoja na sare za polisi. Maaskari hao waliouawa walikuwa wakibadilishana lindo na wenzao waiokuwa wakati wa mchana.
0 comments:
Post a Comment