Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema amepandishwa mahakamani katika kesi mbili tofauti.
Kesi
ya kwanza namba 351/2016 anatuhumiwa kumtumia ujumbe wa simu wa
uchochezi Mkuu wa mkoa Arusha, Mrisho Gambo wenye maneno kuwa “Karibu
tutakudhibiti kama mashoga walivyodhibitiwa Uarabuni”
Kesi ya pili namba 352/16 Lema anatuhumiwa kuhamasisha maandamano Septemba Mosi kinyume cha sheria.
Hakimu amepinga hoja za wakili wa Serikali, Vincent Njau kuzuia dhamana kwa sababu za kiinterejensia kwa usalama wake.
Baadaye
vurugu ziliibuka mahakamani wakati polisi wanataka kumpeleka Lema
magereza kwa madai kuwa wanadhani wamechelewa, lakini mbunge huyo
alipinga hatua hiyo kwa maelezo muda wa mahakama saa 9.30 ulikuwa bado.
0 comments:
Post a Comment