Home »
Habari Moto
» #YALIYOJIRI>>>>WALIMU 22 Azania Sekondari Waondolewa Baada ya Shule Kuwa ya Mwisho Matokeo Kidato cha Sita.Fahamu zaidi hapa.
Walimu 22 wa Shule ya Sekondari ya Azania Manispaa ya Ilala, akiwamo
Mwalimu Mkuu, wamehamishwa kwa kile kilichodaiwa ni kutokana na matokeo
mabaya ya kidato cha sita.
Chanzo hicho cha habari kiliongeza kuwa kati ya walimu hao, 17 walikuwa
wanafundisha kidato cha tano na sita huku wanne kidato cha kwanza hadi
cha nne na mmoja aliyekuwa mkuu wa shule hiyo.
Taarifa hizo ziliongeza kuwa kati ya walimu 17, wengi wao walikuwa
wanafundisha mchepuo wa ECA ambao wote wamehamishwa na kupangiwa shule
nyingine huku wengine wakihamishiwa shule za kata na kupangiwa
kufundisha kidato cha kwanza, pili na tatu. Awali, walimu hao walikuwa
wakifundisha kidato cha tano na sita.
Hivi karibuni Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), lilitangaza matokeo
ya kidato cha sita na shule hiyo kongwe ikajikuta imo katika kundi la
shule 10 za mwisho zilizokuwa na matokeo mabaya.
Related Posts:
#YALIYOJIRI>>>> Clinton: Nusu ya wafuasi wa Trump ni wahuni.Fahamu zaidi hapa.Mgombea wa urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic, Bi.
Hillary Clinton, amesema nusu ya wafuasi wa mpinzani wake, Donald Trump
ni wahuni.
Akiongea katika hafla ya kuchangisha
fedha za kampeni yake, Clinton… Read More
#YALIYOJIRI>>>Vitambulisho vya Taifa Kubadilishwa kuanzia Jumatano Septemba 14, 2016.Fahamu zaidi hapa.
Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inatarajia kubadilisha vitambulisho
vyote vya zamani ambavyo havina saini, huku ikitarajia kutoa
vitambulisho vipya vyenye saini kwa wananchi wote, waliokamilisha
taratibu za us… Read More
#BURUDANI>>>>Alikiba kutumbuiza kwenye tuzo za MTV MAMA, Oktoba 22.Fahamu zaidi hapa.Muimbaji wa Aje, Alikiba ni miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye tuzo za MTV MAMA huko Johannesburg, Afrika Kusini.
Kupitia mtandao wa Instagram wa meneja wa msanii huyo, Seven Mosha
ameweka picha ya msanii wake huy… Read More
#YALIYOJIRI>>>Mrema Awapongeza Wabunge wa UKAWA Kwa Kukubali Kurudi Bungeni.Fahamu zaidi hapa.
Mwenyekiti
wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) Taifa, Augustine Mrema amewapongeza
wabunge wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), kwa
kuamua kuacha kususa kuhudhuria vikao vya Bunge kushinikiza Naibu S… Read More
#YALIYOJIRI>>>>Freeman Mbowe awasili Bukoba leo kwa lengo la kuwajulia khari wahanga wa tetemeko.Fahamu zaidi hapa.
MwenyeKiti wa chama cha Chadema Freeman Mbowe akiwa na wahanga wa tetemeko Bukoba leo kwa lengo la kuwajulia khari na kuwafariji.
Hii ndiyo pole aliyotoa Freeman Mbowe
"Pole zangu za dhati kwa wahanga wa tetem… Read More
0 comments:
Post a Comment