Jeshi
la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) leo linaanza shamrashamra za
maandalizi kuelekea siku ya maadhimisho ya 52 ya majeshi inayotarajiwa
kufanyika Septemba Mosi mwaka huu kwa kufanya usafi na upandaji miti
katika kambi za jeshi na baadhi ya taasisi nchini.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, Msemaji wa JWTZ
Kanali Ngemela Lubinga aliwatoa hofu wananchi kuwa wasitishike pindi
watakapoona wanajeshi katika maeneo ya karibu na makazi yao.
“Kesho
(leo) tuaanza kufanya usafi kuanzia maeneo ya Kawe hadi karibu na kambi
ya Lugalo, na kwamba niwatoe hofu wananchi pindi watakapoona wanajeshi
wengi mitaani kwa kuwa hatuna nia mbaya hivyo wasitufikilie vibaya,” alisema.
Alisema
jeshi hilo litafanya usafi pamoja na upandaji miti katika baadhi ya
maeneo nchini hadi siku ya kilele cha maadhimisho hayo. Pia wanajeshi
watajitolea damu salama katika hospitali za kambi za jeshi.
“Siku
kuu ya majeshi itaadhimishwa pamoja na wanajeshi kujitolea damu kwenye
vituo maalumu vya kutolea damu salama mikoani, katika hospitali zetu za
kanda,” alisema na kuongeza.
“Sanjari
na utoaji damu, madaktari wetu JWTZ watatoa huduma za tiba bure kama
upimaji wa virusi vya Ukimwi, kisukari, na upimaji wa shinikizo la damu.
“
“Kama
ilivyo mila na desturi ya majeshi kufanya usafi na utunzaji wa
mazingira, kuelekea siku ya maadhimisho tutafanya usafi na kupanda miti
maeneo ya jirani na kambi na kwenye taasisi za kiraia kadri mahusiano
yatakavyofanyika na taasisi hizo, ” alisema.
Pia
alisema siku hiyo ya maadhimisho itaadhimishwa kwa kuienzi michezo na
kudumisha urafiki baina ya JWTZ, wananchi, na Taasisi na kwamba
mashindano mbalimbali yatafanyika.
Tarehe
hiyo hiyo ya Septemba 1 , Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
kimetengaza kufanya maandamano na mikutano nchi nzima ili kulaani kile
wanachokiita udikteta unaofanywa na serikali ya awamu ya tano.
Tayari tangazo hilo la Chadema limepingwa vikali na Rais John Magufuli, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani na Nsato Marijani, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Operesheni na Mafunzo huku chama hicho kikiendelea kusisitiza azma yake.
Tayari tangazo hilo la Chadema limepingwa vikali na Rais John Magufuli, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani na Nsato Marijani, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Operesheni na Mafunzo huku chama hicho kikiendelea kusisitiza azma yake.
0 comments:
Post a Comment