Baada ya kupata ushindi wa magoli 3-1 kwenye mchezo wake wa kwanza dhidi ya Ndanda FC, Simba SC imejikuta ikibanwa na maafande wa JKT Ruvu na kulazimishwa suluhu (0-0) katika mchezo wa ligi ku Tanzania bara uliomalizika kwenye uwanja wa taifa.
Ibrahim Ajib aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Frederick Blagnon lakini haikutosha kuisaidia Simba kupata ushindi mbele ya JKT Ruvu
Ikumbukwe May 21 2016, JKT Ruvu waliikomalia Simba na kuitandika bao 2-1 kwenye mchezo wao wa mwisho wa ligi kuu msimu uliopita.
Kocha wa Simba Joseph Omog akitoa maelekezo kwa wachezaji wake
Vikosi vilikuwa kama ifuatavyo:
Simba: Vicent Angban, Malika Ndeule, Novalty Lufunga, Method Mwanjali, Mohamed Hussein, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin, Laudit Mavugo, Fredrick Blagnon/Ibrahim Ajib, Jamal Mnyate/Mwinyi Kazimoto.
JKT Ruvu: Michael Aidan/James Msuva/Nashon Naftali, Said Kipao, Salum Gila,Nurdin Mohamed, Rahim Juma,Ismail Amour Hassan Matemela, Hassan Dilunga, Atupele Green, Saady Kipanga, Pera Mavuo.
Matokeo ya mechi nyingine zilizochezwa leo kwenye viwanja vingine:
Mtibwa Sugar 2-0 Ndanda FC
Azam FC 3-1 Majimaji FC
Tanzania Prisons 1-1 Ruvu Shootings
Mbao FC 0-1 Mwadui FC
Kagera Sugar 0-0 Stand United
0 comments:
Post a Comment