Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwaondoa wafanyabiashara wadogo maarufu kama Machinga katika maeneo ya soko la Kariakoo na barabarani, hususan karibu na barabara za mabasi ya mwendo kasi.
Akizungumza
jana na Kamati ya Bunge, Waziri huyo wa TAMISEMI alisema kuwa kurejea
kwa wafanyabiashara hao katika maeneo hayo kumeleta usumbufu mkubwa na
uchafu wa mazingira katika maeneo ya jiji.
“Namuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam awaondoe na asilegeze kamba,” alisema Waziri Simbachawene.
Alisema kuwa hali hiyo imetokana na tafsiri isiyo sahihi ya agizo la Rais John Magufuli alipokuwa ziarani Mkoani Mwanza.
“Wala agizo la Mheshimiwa
Rais halikumaanisha hicho. Mheshimiwa Rais alisema tuwatafutie maeneo
mbadala ambao wapo maeneo kama ya Mwanza na walikuwa wanafanya biashara
ya kuuza nguo, akizungumzia wale particular group walioko pale Mwanza.
Kwa Dar es Salaam tulishamaliza huko,” alisema.
Aidha,
alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha hakuna hata machinga
mmoja atakayeonekana akifanya biashara katika maeneo ya barabara za
mabasi yaendayo kasi.
Aigizo
hilo la Waziri Simbachawene liliungwa Mkono na wajumbe wa Kamati hiyo
ya Bunge ambao walisema kuwa hali ya soko la Kariakoo imekuwa mbaya
kutokana na kuzagaa kwa machinga.
0 comments:
Post a Comment