TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ndugu wanahabari,
Chama
cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa majonzi na masikitiko makubwa sana
taarifa ya kushambuliwa na kuuawa kwa askari wa jeshi la Polisi wakiwa
katika kutekeleza majukumu yao ya ulinzi eneo la Mbande, Temeke jijini
Dar Es Salaam.
CCM
tayari imemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP
Ernest Mangu pamoja na familia za marehemu waliofikwa na umauti katika
tukio hilo baya katika historia ya nchi yetu.
Tunalaani
tukio hilo na kutoa wito kwa wananchi kuvipa ushirikiano wa kutosha
vyombo vya dola ili kufanikisha wahusika wa tukio hilo kusakwa popote
pale na kupatikana ili wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria haraka.
Serikali
ya Chama Cha Mapinduzi itaendelea kuhakikisha amani ya Taifa letu
inalindwa dhidi ya wachache wanaofurahia madhila kwa wananchi wetu.
Wananchi wetu wanapenda, wamezoea na wanastahili amani. Ndio maana
Tanzania imekuwa nchi ya kupigiwa mfano, ikionesha uongozi katika maeneo
mengi. Tuendelee kuilinda taswira hii.
MAFANIKIO YA AWAMU YA TANO
Ndugu wanahabari,
CCM
inachukua nafasi hii kumpongeza Rais Mhe Dkt John Pombe Magufuli na
Serikali yake kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika muda mfupi wa
uongozi wake.
Rais
Magufuli aliahidi mabadiliko. Tunampongeza kwa kusimamia vema
utekelezaji wa ilani ya CCM. Katika muda mfupi wa miezi tisa tu, Rais Dk
Magufuli amefanya mambo makubwa.
Sote
tunafahamu kuwa Shirika letu la Ndege, ATCL, limekuwa linafanya kazi na
ndege moja. Serikali ya Dk Magufuli imekwisha lipia ndege tatu za
abiria toka Canada, ndege mbili zitaingiza nchini mwezi ujao.
Reli
ya kati inajengwa kwa kiwango cha Standard Gauge. Meli katika ziwa
viktoria inanunuliwa ktk bajeti ya mwaka huu. Elimu ya msingi na
sekondari inatolewa bure. Wanafunzi wetu sasa wanakalia madawati na
kujifunza vizuri zaidi.
Barabara
zimeendelea kujengwa. Makusanyo ya kodi yameongezeka. Huduma za jamii
zinaendelea kuimarika. Lakini pia, nidhamu katika utumishi wa umma sasa
imeimarika. Wananchi wanastahili huduma nzuri na kuthaminiwa na
wafanyakazi wa Umma.
Mataifa
mengi ya Afrika na nje ya Afrika yanaiga mbinu za Rais wetu katika
kuleta mabadiliko nchini mwao. Hapa Kenya tu, Waziri mmoja wa Elimu
anayesifika kwa utendaji kazi mzuri, anajiita “MAGUFULI.” Hata
Australia, baadhi ya wananchi waliwahi kumtaka Waziri Mkuu wao afanye
kazi kama Dk Magufuli.
Dk.
Magufuli ameazimia kujenga uchumi wa viwanda. Ifikapo mwaka 2025,
Tanzania itakuwa nchi yenye uchumi wa kati. Maisha ya wananchi wetu
yataboreka.
Vijana
wetu wapate ajira katika viwanda, watauza malighali na mahitaji
mbalimbali ya viwanda. Wakulima watapata masoko ya bidhaa zao katika
viwanda hivyo. Kilimo kitaongezeka thamani kutokana na mahitaji
mbalimbali ya viwanda vyetu. Hatua za kuelekea huko tayari
zimechukuliwa.
Wapo
wachache wanaelekea kutafuta mbinu chafu za kuhujumu mafanikio haya,
lakini hawatafanikiwa. Watanzania wamemchagua Dk Magufuli ili awaletee
maendeleo.
Serikali
ya CCM, itawasaidia vijana wa Tanzania kuendesha uongozi wa Taifa lao.
Kamwe tusikubali ndoto ya kuongoza mapinduzi haya makubwa kwa ajili ya
Taifa na Bara letu ikapokonywa na watu wachache wasiokuwa na dira ya
kuliletea maendeleo Taifa letu. Tuwapuuze.
UPINZANI KUSUSIA VIKAO VYA BUNGE
Ndugu Wanahabari,
Bunge
kama ilivyo kwa mhimili mingine linaongozwa kwa katiba, sheria na
kanuni katika mijadala na maamuzi yake. Kama Mbunge hajaridhika na
maamuzi ya Spika, Naibu Spika au Mwenyeki wa kikao, kuna taratibu za
kufuata. Utaratibu wa kikanuni ni kuulalamikia uamuzi huo kwa Katibu wa
Bunge.
Wakiwa
wanafahamu taratibu za kikanuni, kama kawaida yao, WAPINZANI, waliamua
kuzisigina na badala yake wakataka Naibu Spika aondolewe.
Hivyo
wakaratibu kupigwa kura ya kutokuwa na imani na Naibu Spika. Ambapo
suala hilo lilipelekwa kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya
Bunge.
Kutokana
na kutokuwepo kwa Spika nchini, hoja hiyo haikufikia ukomo.
Tunamshukuru Mungu afya ya Spika imeimarika. Sasa hoja hiyo huenda
itafikishwa katika mkutano wa Bunge litakalokaa mwezi ujao.
Kana
kwamba hiyo haitoshi, kama kawaida yao, hawakuwa na subira ya kufuata
taratibu. Wakaamua kufanya kihoja. Wakaamua kutohudhuria vikao vyote vya
Bunge vilivyokuwa vikiongozwa na Naibu Spika.
Na
hata walipoingia Bungeni waliziba midomo yao na kuamua kutowasalimia
wabunge wenzao wa CCM, kutopeana mikono na hata kutohudhuria misiba na
sherehe zao.
Vitendo
vyao hivi ndivyo vimeasisi chuki ndani ya jamii yetu iliyozoea UPENDO,
UDUGU, UMOJA NA MSHIKAMANO. Watanzania tunafahamika na tunaona fahari
kuishi kama ndugu.
Baada
ya kitendo hicho cha kuwasaliti wapigakura wao kulaaniwa kila kona ya
nchi, sasa wamekubali kutumiwa kama vibaraka kuichafua taswira ya nchi
yetu, nao kwa hila iliyo wazi, wamekubali kuwafitinisha watanzania kwa
kuandaa maandamano ya nchi nzima, yasiyo na ukomo. Hatua hii ni uvunjaji
wa katiba ya nchi, Sheria na inalenga kuvunja amani, utulivu na
mshikamano wa watu wetu.
Ileleweke
kwamba, wanachokifanya hawa CHADEMA ni kuchochea wananchi kwa makusudi
kutotii maagizo halali ya vyombo vya dola na Serikali kwa visingizio
mufilisi kuwa katika Katiba imewapa uhuru huo. Katika haitoi haki na
uhuru usio na ukomo. Ibara ya 29 (5) inasema;
“Ila
watu wote waweze kufaidi haki na uhuru vinavyotajwa na katiba hii kila
mtu ana wajibu wa kutenda na kuendesha shughuli zake kwa namna ambayo
haitaingilia haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma”
Baada
ya kusema hayo, ninaomba CHADEMA wakumbuke na kutilia maanani kuwa kila
haki ina wajibu na hakuna haki au uhuru usiokuwa na ukomo hususani pale
inaposababisha kuingiliwa ama kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu
wengine. Rejea ibara ya 30 (1) na (2) ya Katiba.
Ndugu wahabahari,
Mwisho
tunatoa pole kwa wenzetu wa CUF kutokana na mapambano huko kwao.
Tumestushwa sana na yanayoendelea huko. CCM inawapa pole na tunawatakia
maelewano ili waje tusaidiane kuwaletea watanzania maendeleo.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
0 comments:
Post a Comment