Home »
Habari Moto
» #YALIYOJIRI>>>Mfanyabiashara Ataka Kujirusha Daraja la Ubungo.Fahamu zaidi hapa.
Katibu wa Chama cha Wafanyabiasha za Mezani katika maeneo ya Stendi ya
Mkoa, Ubungo jijini Dar, John Shayo amekusanya umati baada ya kupanda
juu kabisa ya daraja jipya lililopo eneo hilo na kutaka kujirusha,
akihitaji Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda afike hapo kwani hakutendewa
haki.
Tukio hilo lililovuta hisia za wengi lilijiri kwenye Daraja la Ubungo
ambapo katibu huyo alitaka afe kwa kuwa anadai hajatendewa haki na
alitaka Makonda afike amwelezee shida zake katika suala zima la ufanyaji
biashara ndipo aweze kushuka la sivyo angejirusha.
Kundi kubwa la watu lilikusanyika eneo hilo huku polisi na gari lao la
zima moto wakitanda wakimshangaa akiwa anazungukazunguka akisema yeye ni
Mtanzania anahitaji haki ndipo walimsubiria alipokuwa akimpa mkono
ndugu yake kama ishara ya kumuaga wakamvuta na kufanikiwa kumshusha.
Baada ya kushushwa, aliwekwa chini ya ulinzi wa polisi kisha akapelekwa
katika Kituo cha Polisi cha Ubungo ambapo wafanyabiashara wenzake
walidai kwamba alikuwa na mgogoro na mwenzake waliyekuwa wanafanya
biashara pamoja. Hata hivyo, hadi mwandishi wetu anaondoka kituoni hapo,
jamaa huyo alikuwa akitoa maelezo.
Stori/picha: Gladness Mallya/GPL
Related Posts:
Chadema Walianzisha ..!!!!..Fahamu zaidi hapa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kakonko, Juma Maganga amepewa siku saba kueleza sababu ya kupitisha
bajeti ya mwaka 2017/18 ikidaiwa ni kinyume na utaratibu.
Wakizungumza na waandishi wa habari,
madiwani k… Read More
Mahaba Niue..!! Tazama Hapa Jinsi Trump na Mkewe Walivyoonyeshana Mahaba Ikulu Wakati Wakicheza Muziki..!!..Fahamu zaidi hapa.
Donald Trump na mkewe, Melania juzi
walilionyesha jiji la Washington mvuto wa familia yao wakati
walipopanda kudansi kwenye jukwaa lililopambwa kwa taa za rangi
nyekundu, nyeupe na bluu ambazo ni za bendera ya Mar… Read More
Waumini Kanisa la Anglikan Wamzuia Askofu Mokiwa kufanya vikao.Fahamu zaidi hapa.
Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam wa Kanisa la Anglikana, Dk valentino
Mokiwa jana alishindwa kuendesha vikao viwili baada ya kundi la waumini
kufika Usharika wa Ilala kwa lengo la kuzuia.
Askofu Mokiwa,
ambaye an… Read More
Inasikitisha Mnoo!! Mama Atupa Kichanga Chake Chooni Kisa Eti Anaokoa Ndoa Yake Isivunjike..!!!..Fahamu zaidi hapa.
MATUKIO mawili ya mama
kutupa vichanga chooni baada ya kujifungua, yametikisa katika wilaya za
Sikonge na Shinyanga. Katika tukio la wilayani Sikonge, mama akichukua
uamuzi huo ili kulinda ndoa isivunjike, baada ya kupa… Read More
Yahya Jammeh aondoka nchini Gambia kwenda kuishi uhamishoni.Fahamu zaidi hapa.
Aliyekuwa
Rais wa Gambia, Yahya Jammeh ameondoka nchini humo baada ya mvutano wa
muda kufuatia kushindwa katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika
Disemba Mosi mwaka jana.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na EC… Read More
0 comments:
Post a Comment