Sheria
ya Fedha ya Mwaka 2016 iliyopitishwa kuhusu utozaji ushuru kwenye ada
ya kutuma na kupokea fedha kwenye miamala ya benki na simu, imeanza
kuzaa matunda kutokana na ongezeko la mapato lililoanza kushuhudiwa
kutoka kampuni za simu.
Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu iliyokutana jana na Mamlaka ya
Mawasiliano (TCRA), iliambiwa kutokana na sheria hiyo iliyopitishwa
Bunge baada ya kupitisha bajeti ya mwaka huu, mwezi uliopita serikali
imeshuhudia ongezeko kubwa la mapato, yaliyotolewa na kampuni za simu.
Taarifa
hiyo ilitolewa jana kwenye Kamati ya Kudumu ya Miundombinu, imeonesha
Kampuni ya Vodacom ilikuwa ikitoa kodi ya ushuru wa bidhaa kwa fedha
zinazotumwa kwa wastani wa Sh milioni 360 kwa mwezi, lakini baada ya
mabadiliko ya sheria, Julai pekee mwaka huu imelipa Sh bilioni 1.9.
Mwakilishi
wa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Godwin Barongo aliiambia
kamati hiyo kuwa kwa upande wa Kampuni ya Tigo, walikuwa wanatoa wastani
wa Sh milioni 250 kwa mwezi, lakini sasa wametoa Sh bilioni 1.48.
Barongo
ambaye ni Meneja Msaidizi, Kitengo cha Walipa Kodi Wakubwa TRA alikuwa
akizungumzia namna Mtambo Maalumu wa Kusimamia Mawasiliano na Udhibiti
wa Mapato yatokanayo na Simu (TTMS) unaosimamiwa na Mamlaka ya
Mawasiliano (TCRA) ulivyowezesha kufanikisha ukusanyaji mapato.
“Pamoja
na mabadiliko ya sheria yaliyoanza mwezi Julai mwaka huu, kampuni za
simu zilikuwa zikitoza transfer, lakini sheria ilikuwa haigusi kwenye
kutoa, Baada ya hiyo, tuligundua kuwa sasa kamisheni nyingi zilipelekwa
kwenye kutoa kwa sababu hakuna tozo na kwenye transfer zinapungua,” alisema Barongo.
Aliendelea kusema, “Kwa hiyo mabadiliko haya ya sheria ya sasa hivi ambayo tunatoza kwenye kuweka na kutoa, yametusaidia.”
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso
alisisitiza kuwa wabunge wanategemea Wizara ya Miundombinu kupitia
sekta ya mawasiliano, ichangie mapato mengi kwa serikali.
Baada
ya Bunge kupitisha mabadiliko ya sheria ya fedha yaliyopitisha utozaji
kodi ya ushuru wa bidhaa katika miamala ya benki na simu za mkononi,
ulijitokeza mjadala ambao baadhi ya watu walidai ushuru huo utaathiri
wateja wa kampuni za simu na benki.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alifafanua kwamba serikali
imeamua kutoza ushuru kwenye ada ya kutuma na kupokea fedha au vyote kwa
kadri itakavyotozwa akisisitiza kwamba utalipwa na benki na kampuni na
si mtumiaji au mpokeaji wa fedha katika miamala itakayofanyika.
0 comments:
Post a Comment