Wakati
viongozi wa dini wakiendelea na jitihanda za kusaka suluhu kati ya
upande wa Serikali na Chadema kuhusu namna ya kuzuia kwa amani kufanyika
kwa Operesheni ya chama hicho iliyopewa jina la UKUTA, Septemba 1,
Kiongozi Mkuu wa Chama Cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ametoa maoni yake.
Zitto
ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini amesema kuwa haoni haja ya
kufanyika kwa vikao hivyo vya kusaka maridhiano kwani Chadema
wanachotaka kufanya kiko kikatiba.
“Sioni
ni kwanini tunahangaika na vikao vya maridhiano na tahariri nyingi
kuhusu shughuli ya CHADEMA kufanya operesheni yao ya UKUTA. Kuandamana
ni Haki ya KIKATIBA. Tuache watu watimize Haki yao Kwa amani. Kuzuia
watu kufanya jambo lao la kikatiba ndio kuvunja amani. Wanaotaka
kuandamana waandamane na wanaotaka kufanya Kazi zao nyingine tuendelee
na Kazi zetu. Kwanini kutekeleza Haki ya kikatiba iwe ni kuvunja amani?
Kwanini?,” Zitto ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Hata
hivyo, vikao vya maridhiano vinavyoendelea tayari vimeonesha kuzaa
matunda kwenye suala la mgogoro wa Bunge ambapo wabunge wa vyama vya
upinzani wameridhia kurejea Bungeni katika vikao vitakavyoanza mapema
mwezi ujao.
Serikali
imeendelea kuwaonya watu wote wanaopanga kuandamana Septemba 1 huku
viongozi wa Chadema wakisisitiza kuwa siku hiyo watafanya maandamano
kama walivyopanga.
Hali
hiyo imepelekea kumtoa hadharani Kingunge Ngombale Mwiru ambaye ameomba
marais wastaafu kumshauri Rais Magufuli ili kuruhusu Serikali kukaa na
Chadema kusaka muafaka wa masuala ya kisiasa nchini.
0 comments:
Post a Comment