Monday, 27 February 2017

Mwanamuziki Barnaba Apata Pumziko Jingine Baada ya Kuachana na Mkewe.Fahamu zaidi hapa.

Haya sasa Barnabas Naye ameanza taratibu kutuonyesha MTU wake ama Nene? Kama wengi mjuavyo Mwanamuziki Barnaba alizenguana na mkewe na kuachana ambapo aliyekuwa mkewe Siku ya Valentine day alionyesha ulimwengu kuwa AME move on kwa picha iliyosambaa akiwa na mwanaume mwingine..

Sasa Barnaba na yeye amekuja na kupost picha akiwa na msichana mwingine huku akituachia kitendawili...
.

#Repost #barnabaclassic
・・・
Pale Crush brother anapokutaka na crushe sister #iam_just_rakel 😘🌺πŸ”₯πŸ—½☀️ Doll metalick Moshi Moshi -Classic Yuko Njiani Jesus is my Power 😊☕️Asante mzazi #@Regrann from @crazyvoicess - Follow @crazyvoicess (me) for more videos like this! ❤πŸ˜„
Amazing 😍
Tag a friend πŸ‘‡
🎀
#crazyvoicess #amazing #vocals

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa


Hussein Machozi Afunguka Mazito...Adai Watu Wake wa Karibu Wanataka Kumpora Mke Baada ya Kushuka Kisanii.Fahamu zaidi hapa.

Kwa msanii au mtu maarufu, kinga pekee inayomsaidia kuendelea kuwa na heshima yake, ni kuwa na wimbo unaofanya vizuri ama kuwa na fedha.



Anapokosa hivyo, mambo hubadilika na hapo ndipo ule usemi wa Fid Q kuwa usupastaa ni mzigo wa miiba huwa na maana. Hussein Machozi anaijua hali hiyo na kupitia mitihani aliyopitia miaka miwili iliyopita, amejifunza mengi.


“Nimejifunza kuna watu wa kweli na kuna watu feki,” Machozi ameiambia Bongo5.
“Kuna watu wa kweli ambao wamekaa na mimi kwa shida mpaka sasa hivi wapo na mimi, marafiki wa kweli. Na kuna watu baadhi ambao walikuwa wapo karibu sana na mimi kipindi nipo juu, lakini kipindi ambacho nilikuwa kimya kwa muda mrefu, wameniacha mbali wamenitupa,” anasema.

“Wamenisahau,wameninyanyasa, imefikia kipindi wengine wanatongoza mpaka mke wangu. Ni kitu ambacho kinauma sana na sio kwamba mtu anamtongoza mtu hamjui, anamtongoza anajua kabisa huyu ndio future ya Hussein Machozi, yaani ndio mtu anayemtegemea. Siwasemi wengine ni mabosi walikuwa wanajifanya mabosi na vitu kama hivyo. Lakini yote tupilia mbali, ni kwamba mimi nasonga mbele na maisha naendelea na maisha yangu, nimesahau mabaya yote, nimefungua ukurasa mpya.”

Machozi ambaye kwa sasa anaishi nchini Italia amesema amenyanyuka tena na sasa yupo tayari kurudi kwenye muziki. Anatarajia kuachia kazi yake mpya iitwayo Nipe Sikuachi.
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa


Kichuya supper Sub hatari mbayo akiingia tu afanyi makosa.Fahamu zaidi hapa.

WINGA Shiza Ramadhani Kichuya, kwa mara nyingine tena siku ya Jumamosi  aliibuka shujaa wa Wekundu wa Msimbazi baada ya kutokea benchi na kuisaidia Simba kushinda 2-1 dhidi ya mahasimu, Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Kichuya aliyempokea beki Novatus Lufunga dakika ya 55, kwanza alimsetia mshambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo kuifungia bao la kusawazisha Simba dakika ya 66 kabla ya yeye mwenyewe kufunga la ushindi dakika ya 81.

Ikumbukwe Kichuya ndiye aliyeifungia Simba bao la kusawazisha dakika ya 86 Oktoba 1, mwaka jana timu hizo zikitoka sare ya 1-1 baada ya Amissi Tambwe kutangulia kuifungia Yanga dakika ya 26 kwa makosa ya Lufunga tena.

Yanga SC walitangulia kwa bao la mapema tu dakika ya tano la Simon Msuva kwa mkwaju wa penalti, baada ya kiungo Mzambia, Obrey Chirwa kuangushwa kwenye boksi na Lufunga.
 Obrey Chirwa akimtoka beki Novaty Lufunga leo kabla ya kuangushwa na kusababisha penalti
 Laudit Mavugo akimiliki mpira mbele ya beki wa Yanga, Kevin Yondan.
 Haruna Niyonzima akigombea mpira na Janvier Bokungu.
Amissi Tambwe akiwa chini baada ya kugongana na Lufunga

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa


Lori Laporomoka Mlimani, Laua Wafanyabiashara 6 na Kujeruhi 12.Fahamu zaidi hapa.

Wafanyabiashara sita wamekufa papo hapo na wengine 12 kujeruhiwa, baada ya lori lililokuwa likiwapeleka mnadani kuacha njia na kuporomoka kwenye mlima wenye kona nyingi zinazofikia 99 wilayani Lushoto.

Taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba zilisema ajali hiyo ilitokea jana Jumapili jioni katika mlima wenye idadi hizo za kona zinazoanzia Mng’aro hadi Mlalo wilayani Lushoto, baada ya lori aina ya Mitsubishi Fuso Canter kuporomoka.

Watu walioshuhudia ajali hiyo walisema lori hilo lilikuwa likitokea Kijiji cha Mng’aro kilichopo uwanda wa chini lilipokuwa likipanda mlima kuelekea Mlalo kwa ajili ya kuwahi soko siku inayofuata.

Walisema lori hilo lilipofika katikati ya mlima liliacha njia na kurudi nyuma hatimaye likaporomoka bondeni, huku mizigo ikiwaangukia watu hao.

Kamanda Wakulyamba aliwataja waliokufa kuwa ni Jamal Hemed (40), mkazi wa Mlalo, Hassan Rashid (33) wa Nyasa, Bisura Seif wa Kifungilo, Hadija Said wa Mhelo, Zuena Juma wa Kwedege na Husna Athumani wa Hemtoye.

Alisema majeruhi wa ajali hiyo walipelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto kwa matibabu. Kamanda huyo alisema dereva wa lori hilo, Nassoro Athumani (25) anatafutwa kwa kuwa alitoroka baada ya ajali.

Alisema uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva na ubovu wa gari.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa


#Breaking News>>>Jenerali Ulimwengu Aiomba Mahakama Imuunganishe Katika Kesi Ya Mbowe Dhidi Ya Makonda.Fahamu zaidi hapa.

Mwanahabari nguli Jenerali Ulimwengu, leo anatarajia  kuwasilisha maombi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, akiomba kuungana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe  katika kesi ya katiba iliyofunguliwa hivi karibuni.
Ulimwengu anaomba kuunganishwa katika kesi ya katiba namba 1 ya 2017 kama mdai dhidi ya wadaiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam na Ofisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
“Maombi ya kumuunganisha yameandaliwa na kesho(leo) yatakuwa mahakamani kuomba naye awe mdai. Anaomba kujiunga kwa kuwa mambo anayopigania Mbowe naye ana maslahi nayo kwa sababu ni mambo muhimu ya katiba,” alisema mmoja wa jopo la Mawakili kutoka Kurugenzi ya Katiba Sheria na Haki za Binadamu ya Chadema, Peter Kibatala.
Katika kesi hiyo ya katiba, Mbowe anaomba Mahakama Kuu itamke   kuwa Mkuu wa Mkoa hana mamlaka ya kudhalilisha na kukamata.
Mbowe pia anaomba mahakama itengue vifungu vya 5 &7 vya Sheria ya Tawala za Mitaa kwa kuwa ni batili na vinakiuka haki ya katiba.
Mbowe alifungua kesi hiyo akidai Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekiuka sheria na taratibu katika kushughulikia watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya nchini.
Kesi hiyo ya katiba inasikilizwa na majaji watatu, Jaji Sakieti Kihiyo, Jaji Lugano Mwandambo na Jaji Pellagia Khaday.
Baada ya kufungua kesi hiyo Mbowe pia aliomba mahakama itoe amri asikamatwe mpaka maombi yake ya zuio yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Mahakama ilitoa zuio la muda kwa Jeshi la Polisi  kutomkamata Mbowe hadi maombi yake ya kupinga kukamatwa aliyowasilisha mahakamani yatakaposikilizwa.
Maombi hayo yalitakiwa kusikilizwa mwishoni mwa wiki lakini upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Gabriel Malata uliwasilisha pingamizi, ukiomba mahakama iyatupilie mbali kwa sababu  hana msingi katika sheria.
Upande wa mdai ulijibu hoja za kupinga maombi yao na Mahakama ilisikiliza hoja za pande zote mbili na kupanga kutoa uamuzi wa pingamizi hilo Machi 2, mwaka huu.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa


Waziri Kigwangalla Amehairisha Mkutano wa Kuwataja Wanaohusika na Mapenzi ya Ushoga.Fahamu zaidi hapa.

Naibu Waziri Kigwangalla ameahirisha mkutano wa waandishi wa habari alipotegemewa kutaja wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Dkt Kigwangalla amesema kuwa ameshindwa kufanya mkutano huo na kuwataja mashoga hao wanaojiuza mtandaoni kutokana na sababu za kiufundi.

Mnamo tarehe 6 mwezi Februari Naibu Waziri huyo alimtaka kijana anayefahamika kama James Delicious kufika kituo cha Polisi kwa kujitangaza kuwa ni Shoga. - #regrann

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa



Mahakama yaicharukia serikali kesi ya Godbless Lema......Yahoji sababu za mbuge huyo kunyimwa dhamana.Fahamu zaidi hapa.

Mwenyekiti wa kikao cha jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, kinachoendelea Arusha, Bernard Luanda, leo amegeuka mbogo kwa wanasheria wa serikali kwa kitendo cha kumnyima Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema dhamana kwa lengo la kumnyima haki.

Akizungumza Mahakamani hapo leo mbele ya majaji wenzake Stella Mugasha na Jaji Kipenka Mussa, Luanda amesema haipendezi na haingii akilini mtu (Lema) kushikiliwa kwa miezi minne bila sababu kwa misingi ya kumnyima haki.

“Tunaomba ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikai (DPP) muwe makini sana maana mnatufanya wanasheria wote hatuna akili na mnachafua Mahakama, kwa hali ya kawaida mtu mumshikilie kwa misingi ya kisheria, lakini katika kesi hii tumepitia jalada hatujaona kitu chochote cha kumshikilia Lema hadi leo na imetushitua sana,” alisema huku akishauriana na wenzake mara kwa mara kwa masikitiko.

Aliendelea kusema kuwa ofisi ya DPP inaitia najisi taaluma hiyo, kitu kipo wazi ila wanafanya vitu vya ajabu na havipendezi.

Alihoji jaji Luanda kuwa “Tumesoma faili lote tunashangaa hivi kweli ofisi ya mwanasheria mkuu ina wanasheria kweli na kama wapo kwa nini huyu mtu (Lema) awe ndani mpaka leo?”.

Alisema kwa kuwa mikono yao kisheria imefungwa hawawezi kufanya chochote kwa leo na kuwataka Mawakili upande wa Lema kurudi Mahakama Kuu, kuendelea na maamuzi ya dhamana.

Hali hiyo ilitokana na Wakili wa serikali Faraja Nchimbi kusimama mahakamani hapo na kuomba kuiondoa rufaa hiyo kwa madai kuwa ipo nje ya uwezo wake.

“Waheshimiwa Majaji baada ya timu yetu ya wanasheria kupitia kwa kina rufaa hii kwa sababu zisizozuilika tumeona hatupo tayari kuendelea na rufaa hii, maana hatukupeleka kusudio (Notisi) kwa msajili muda ulipita, hivyo tunaomba kuiondoa na uamuzi wa kuiondoa rufaa hii tumeufikia Ijumaa muda uliisha kuja mahakamani,”. Alisema Nchimbi.

Baada ya kuwasilisha ombi hilo, Wakili wa Lema Peter Kibatala, alisimama na kusema upande wao hawana pingamizi ila waliomba hoja za awali za rufaa hiyo ziondolewe Mahakamani hapo bila kunakiliwa.

Baada ya ombi hilo Jaji Kipenka Mussa alipokea kwa niaba ya Majaji wenzake na kukubali ombi la kuiondoa rufaa hiyo namba 9/2017.

Aidha Jaji Luanda alimkaribisha jaji Stella Mugasha pia kuongea kwa niaba yao ambapo alisema mahakama imekubali ombi la pili la kuiondoa rufaa namba 10/2017, baada ya Wakili Paul Kadushi kuomba kuiondoa pia.

Wakili wa Lema Peter Kibatala, alilazimika kusimama tena Mahakamani hapo kusema kuwa upande wao unasikitika kuona ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na DPP wanatumia Mahakama kwa njia ya kumnyima haki mteja wao, hivyo aliomba mahakama hiyo iwatatulie tatizo la kisheria lililojitokeza hadi mteja wao awe ndani hadi sasa.

Kibatala aliongea hayo huku akishindwa kujizuia na kumwaga chozi la huzuni mahakamani hapo mbele ya Majaji hao.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa


Saturday, 25 February 2017

Kuelekea pambano la watani Simba na Yanga kati ya MAVUGO na TAMBWE nani ataifungia timu yake magoli siku juma mosi ya week hii???... Naomba majibu hapa.

Kati ya Mavugo na Tambwe na ataifungia timu yake???..
Toa maoni yako hapa chini.
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Friday, 24 February 2017

DOWNLOAD WIMBO MPYA WA TANZANITE x DEE PESA UNAOITWA "USINIVUKE".

DOWNLOAD WIMBO WA TANZANITE x DEE PESA – USINIVUKE.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa


Download wimbo wa Mimi Mars - Shuga.

Download wimbo wa Mimi Mars - Shuga.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa


Download wimbo wa Lumino Ft. Mohombi, Diamond Platnumz, Franko - Lumino - Rockonolo (Remix).

Download wimbo wa Lumino Ft. Mohombi, Diamond Platnumz, Franko - Lumino - Rockonolo (Remix)


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa


KRC Genk Inayochezewa na Mbwana Samatta Inaungana na Man United 16 Bora ya Europa League.Fahamu zaidi hapa.

Usiku wa February 23 2017 mtanzania Mbwana Samatta akiwa na timu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji aliingia kwenye headlines baada ya kufanikiwa kufuzu kucheza hatua ya 16 bora ya Europa League kwa kuitoa FC Astra ya Romania.

Samatta akiwa na KRC Genk waliikaribisha FC Astra ya Romania katika mchezo wao wa pili wa marudiano wa Europa League, katika uwanja wa Luminus Arena ikiwa ni wiki moja imepita toka watoke sare ya 2-2 ugenini.

Katika game hiyo ya marudiano iliyochezwa na KRC Genk kupata ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Pozuelo kwa faulo dakika ya 67, wameiondoa FC Astra kwa jumla ya goli 3-2, hivyo Genk wanaungana na timu nyingine 15 kucheza hatua 16 bora ya Europa League ikiwemo Man United.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa


Download wimbo mpya wa Man Fongo unaoitwa "Nani Asiyependa".

Download wimbo wa Man Fongo – Nani Asiyependa.



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa


Angalia Video mpya ya Lumino Ft. Mohombi, Diamond Platnumz, Franko - Lumino - Rockonolo (Remix).

Lumino Ft. Mohombi, Diamond Platnumz, Franko - Lumino - Rockonolo (Remix)


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa


MAKONDA AJIBU MADAI YAKUTUMIA CHETI CHA MTU MWINGINE.Fahamu zaidi hapa.

RC Makonda asema hawezi zungumzia suala la cheti chake cha kidato cha nne sababu ni habari za kwenye mitandao ambapo kuna maswali na majibu.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa


RICH Mavoko Atoa Povu Kwa Wanaosema Amekosea Kujiunga na Lebo ya Diamond WCB.Fahamu zaidi hapa.

Muimbaji wa Kokoro, Rich Mavoko amedai kuwa kama bado kuna watu wanaona uamuzi wake wa kusainishwa na label ya Diamond, WCB ni kujishusha sababu yeye ni msanii mkubwa, hawaijui biashara yake.


“Mimi nakutana vitu vingi, mtu mwingine nyuma ya pazia haoni,” muimbaji huyo alikiambia kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz cha Salama Jabir.
“Tunashoot, tunatoa video, tunarelease ngoma inahit, mimi ndo nakuwa napata tabu.Mtu anayesema nimejishusha kimuziki kujiunga WCB anakuwa hajui biashara yangu,” aliongeza.

Rich alisainishwa na WCB mwaka jana na kuachia wimbo wake wa kwanza, Ibaki Story.

Kwa upande mwingine, Rich alidai kuwa asipofanya muziki atakuwa akiwaandikia watu wengine mashairi na kwamba Tanzania ina upungufu mkubwa wa waandishi wa Bongo Flava.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa


LEICESTER CITY YAMTIMUA KAZI RANIERI, NI SIKU 298 BAADA YA KUIPA UBINGWA.Fahamu zaidi hapa.

Leicester City imemtimua kazi kocha wake Claudio Ranieri.


Ranieri ametimuliwa kazi ya kuinoa Leicester ikiwa ni siku 298 na saa kadhaa baada ya kuipa ubingwa wa England.

Ranieri raia wa Italia ametimuliwa siku moja na usher tokea kikosi chake kichapwe mabao 2-1 katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kikiwa ugenini Hispania dhidi ya Sevilla.

Uongozi wa Leicester City umeuita uamuzi huo ni wenye “maumumovu” na sasa msaidizi wake, Craig Shakespeare na kocha mkuu wa timu ya akiba Coach Mike Stowell ndiyo wamekabidhiwa jahazi.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa


TASWIRA MANCHESTER CITY WAKIJIFUA BAADA YA KUJICHIMBIA ABU DHABI.Fahamu zaidi hapa.

Baada ya mchezo wao dhidi ya Manchester United kuahirishwa, Man City wameona ni nafasi nzuri ya kufanya mazoezi nje ya England.


Sasa wamejichimbia Abu Dhabi ambako watakuwa wakifanya mazoezi kujiandaa dhidi ya Monaco. Pia mechi yao ya Kombe la FA dhidi ya Huddersfield, itakayopigwa wiki ijayo.
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa


Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Chaipinga TCU, Chasema Hakijawahi Dahili Wanafunzi Vilaza.Fahamu zaidi hapa.

Siku moja baada ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kutangaza utata wa udahili wa wanafunzi wa vyuo vikuu, wadau wakubwa wa elimu, wamejitokeza kupinga hatua hiyo. Wadau hao ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) .

UDSM kimeeleza kwamba hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyedahiliwa chuoni hapo, ambaye hana sifa za kujiunga na chuo hicho.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Florens Luoga alisema jana kuwa chuo hicho kimeweka utaratibu ambao unaweza mwanafunzi yeyote anayedahiliwa chuoni hapo, awe na sifa zinazohitajika kwa kuwa hawafanyi biashara.


“Sisi hapa ni wakali kuhusu jambo hilo, tukibaini kuwepo kwa mwanafunzi ambaye hana sifa tunamfukuza. Hatusubiri TCU iseme...hata tukibaini kuwa mtu alifanya udanganyifu na alishamaliza chuo, lakini hakuwa na sifa, tunamnyang’anya digrii tuliyompa,” alisema Profesa Luoga na kuongeza:

“Hiki ni chuo, hatufanyi biashara, sisi kazi yetu hapa ni kuandaa wataalamu na ndio maana tunakuwa wakali na makini kuhakikisha wanafunzi tunaowachukua, wote wanakuwa na sifa stahiki”, alisema

 Profesa Luoga alisema uhakiki ambao umefanywa na TCU na kutoa idadi ya wanafunzi 224 wanaosoma chuoni hapo, kuhakikisha wanawasilisha ushahidi wa nyaraka zao, wanaufanyia kazi, kwani kuna uwezekano tume hiyo haina taarifa kuhusu programu zinazoendeshwa na chuo hicho.

Alifafanua kuwa kuna baadhi ya programu maalumu, ambazo Serikali ya Tanzania imeingia na nchi nyingine kwa ajili ya kuendesha programu maalum.

Alisema kozi hizo zimekuwepo chuoni hapo kwa muda wa miaka 40 sasa na zinafanywa kutokana na makubalino ya Serikali ya Tanzania na nchi husika.

Alisema chuo hicho kikongwe Tanzania, kutokana na kuwepo makubaliano hayo kimekuwa kinapokea baadhi ya wanafunzi ambao wanatoka nje ya nchi na akasisitiza kuwa yawezekana ndio hao ambao TCU imeshindwa kupata nyaraka zao.

“Yawezekana kuna taarifa ambazo hazijakaa sawa, tumepokea taarifa ya TCU sisi kama chuo ni jukumu letu kuitekeleza,” alieleza Profesa Luoga.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa


Mzee wa Upako amuonya Nay wa Mitego baada ya kudai anakuja na kanisa lake......Asema kana ana Mama Amkanye.Fahamu zaidi hapa.

Baada ya hivi karibuni msanii wa hip hop, Nay wa Mitego kutangaza kuwa atafungua kanisa lake ambalo litakuwa si la biashara bali ni la kumuabudu Mungu aliye hai, Mchungaji maarufu nchini, , Lusekelo Anthony aka Mzee wa Upako amemuonya kutomchezea Mungu.

Mzee wa upako ameyasema hayo alipotafutwa na E-News ya EATV baada ya kuulizwa maswali juu ya kauli hiyo.

“Kama unakuja kanisani kwa maana kuna biashara, nakupa miaka hii mitatu sio utatembelea ndala utatembelea kucha, ni mtoto mdogo sana hana akili. 
"Mungu hataniwi, anafanya kufuru, kama ana mama yake amemzaa amuonye. Mimi biblia nimesoma na hizo lugha zake nyepesi zitamtokea puani, asithubutu kufanya kanisa kama biashara. 
"Baada ya miaka hii mitatu atajua kwamba kuongoza watu sio kama kuongoza ngo’mbe hakuna jambo gumu kama kuongoza watu wenye akili kama wewe wenye ufahamu kama wewe, wapo watu wengi walianzisha makanisa kwanini walifunga, ujinga hujui ni ujinga ni utoto,” alisema Mzee wa Upako.

Nay amedai kuwa kanisa lake litajengwa Mbezi ya Kimara jijini Dar es Salaam.

==> Msikilize hapo chini



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa