Home »
Burudani
» Hussein Machozi Afunguka Mazito...Adai Watu Wake wa Karibu Wanataka Kumpora Mke Baada ya Kushuka Kisanii.Fahamu zaidi hapa.
Kwa
msanii au mtu maarufu, kinga pekee inayomsaidia kuendelea kuwa na
heshima yake, ni kuwa na wimbo unaofanya vizuri ama kuwa na fedha.
Anapokosa
hivyo, mambo hubadilika na hapo ndipo ule usemi wa Fid Q kuwa usupastaa
ni mzigo wa miiba huwa na maana. Hussein Machozi anaijua hali hiyo na
kupitia mitihani aliyopitia miaka miwili iliyopita, amejifunza mengi.
“Nimejifunza kuna watu wa kweli na kuna watu feki,” Machozi ameiambia Bongo5.
“Kuna
watu wa kweli ambao wamekaa na mimi kwa shida mpaka sasa hivi wapo na
mimi, marafiki wa kweli. Na kuna watu baadhi ambao walikuwa wapo karibu
sana na mimi kipindi nipo juu, lakini kipindi ambacho nilikuwa kimya kwa
muda mrefu, wameniacha mbali wamenitupa,” anasema.
“Wamenisahau,wameninyanyasa,
imefikia kipindi wengine wanatongoza mpaka mke wangu. Ni kitu ambacho
kinauma sana na sio kwamba mtu anamtongoza mtu hamjui, anamtongoza
anajua kabisa huyu ndio future ya Hussein Machozi, yaani ndio mtu
anayemtegemea. Siwasemi wengine ni mabosi walikuwa wanajifanya mabosi na
vitu kama hivyo. Lakini yote tupilia mbali, ni kwamba mimi nasonga
mbele na maisha naendelea na maisha yangu, nimesahau mabaya yote,
nimefungua ukurasa mpya.”
Machozi
ambaye kwa sasa anaishi nchini Italia amesema amenyanyuka tena na sasa
yupo tayari kurudi kwenye muziki. Anatarajia kuachia kazi yake mpya
iitwayo Nipe Sikuachi.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Related Posts:
Penny Afunguka Kuwa na Gundu la Ndoa kwa Mwaka 2017.
MTANGAZAJI wa Runinga ya Magic Swahili kupitia kipindi cha Harusi Yetu,
Penniel Mungilwa ‘Penny’amefunguka kuwa, kuna uwezekano alikuwa na gundu
la kutoolewa mwaka 2017 lakini anaamini mwaka huu, 2018 ataolewa kwa
uwezo … Read More
Lucy Kombaa Kumzalia Mtoto Mzungu Wake.
MSANII wa filamu Bongo, Lucy Komba ambaye kipindi cha nyuma aliweka
ngumu kumzalia mzungu wake, sasa anadaiwa kuwa kwenye mkakati mzito wa
kusaka mtoto baada ya mwanaume huyo na familia yake kuchachamaa azae.
Akizungumza… Read More
Sherehe ya Kuchumbiwa Wolper Balaa..... Muoaji Afanya Kufuru ya Aina Yake.
SHEREHE ya kuchumbiwa kwa Staa wa sinema za Kibongo na Malkia wa Mavazi,
Jacqueline Wolper imezua gumzo la aina yake baada ya muoaji kufanya
kufuru ya aina yake, Amani linaripoti habari hii kwa mara ya kwanza
(exclusive)… Read More
Rose Muhando Atangaza Kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM.
Msanii wa nyimbo za Injili aliyetamba kwa vibao vyake murua na vyenye kuburudisha Rose Muhando, ametangaza kujunga rasmi na Chama cha Mapinduzi.
Msanii huyo ambaye aliomba kujiunga na chama hicho amekabidhiwa kadi ya Ch… Read More
Baada ya Babu Seya na Mwanaye Kwenda Ikulu Mjadala Mkali Waibuka.
Inawezekana ilikuwa ni nia njema kwenda kumshuku Rais kwa kumpa msamaha
uliomuepusha na kifungo cha maisha, lakini kitendo hicho cha Nguza
Mbangu Viking na wanawe kimepokelewa kwa hisia tofauti.
Nguza, ambaye ni mtunzi w… Read More
0 comments:
Post a Comment