Beki wa Zambia ‘Chipolopolo’, Stoppila Sunzu amesaini mkataba wa
miezi mitano wa kuichezea klabu ya Arsenal Tula inayoshiriki Ligi Kuu
Russia.
Taarifa zinasema kuwa Sunzu, ambaye ni mchezo wa Lille ya Ufaransa, amesaini mkataba huo na Tula akiwa Uturuki ilipoweka kambi.
Kwa mujibi wa wakala wa mchezaji huyo Nir Karin amesema mkataba huo
utamfanya Mzambia huyo kucheza Russia hadi Juni 2017 na baada ya hapo
atarejea Lille ambako mkataba wake utamalizika 2019.
Taarifa zinadai kuwa Sunzu alikuwa anatakiwa Ubelgiji, United Arab
Emirates, Marekani na Uturiki, lakini klabu hiyo ya Russia ilionyesha
kumtaka zaidi.
“Tumechagua Russia na kuziacha Ureno, Uturuki na Marekani kwa
sababu hapa kuna ligi yenye ushindani zaidi. Na Juni akimaliza kucheza
kwa mkopo atarudi moja kwa moja Lille,” anasema Karin.
Sunzu tayari ameshazichezea klabu za Konkola Blades, Zanaco,
Chateauroux na TP Mazembe kabla ya kuhamia Sochaux ya Ufaransa na
Shanghai Shenhua ya China msimu wa 2015.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment