SUALA la mfanyabiashara maarufu ndani na nje ya nchi, Mohamed Dewji
(Mo), kukabidhiwa Simba limefikia patamu baada ya viongozi wa matawi
kuutaka uongozi kupeleka mapendekezo ya mchakato huo baraza la wadhamini
la klabu hiyo haraka ili mpango huo ukamilike.
Mo alishaweka wazi kuwa anataka kuweka hisa ya asilimia 51 na
kilichobaki ni mchakato wa kubadili katiba ili zoezi hilo likamilike kwa
muda mwafaka.
Kutokana na umuhimu wa mabadiliko hayo, hivi karibuni uongozi wa Wekundu
hao wa Msimbazi ulikutana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kuangalia
namna ya kumaliza jambo hilo haraka iwezekanavyo.
Rais wa Simba, Evans Aveva, juzi alikutana na viongozi wa matawi wa Dar
es Salaam, ambapo suala kubwa walilolizungumza ni namna ya kuwafunga
Yanga Februari 25, mwaka huu lakini suala la Mo nalo likajitokeza,
ambapo viongozi hao wakitaka kujua kinachoendelea.
Licha ya wajumbe waliokaa katika kikao hicho hawakutaka kuweka wazi
mambo waliyoyajadili, lakini kuhusu suala hilo la Mo, viongozi hao wa
matawi walimbana Aveva na mwisho wakakubaliana kuwa uongozi upeleke
mapendekezo ya mchakato katika baraza la wazee ili wakae na wanasheria
wao kujadili suala hilo waone kama litakuwa na faida kwa klabu.
“Hakuna anayekataa mabadiliko, lakini lazima Wanasimba wote kwa kauli
moja tukubaliane, hatutaki mtu anung’unike ndiyo maana tumeshauriana na
uongozi wakutane na baraza la wazee ili jambo hili tulimalize vema,”
alisema mmoja wa waliohudhuria kikao hicho.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment