Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya,
Rogers Sianga amesema watu wawili wameripotiwa kupoteza maisha mkoani
Mwanza kwa sababu ya kukosa dawa za kulevya mtaani kama walivyozoea.
Kamishna Sianga amesema taarifa hiyo ameipata kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza, hali inayomaanisha mafanikio ya mapambano ya dawa hizo, ambapo
kwa sasa usambaaji wake umepungua mtaani kwa kiasi kikubwa.
"Nimeongea na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, ameniambia kwamba kuna watu wwili
wamefariki sababu walikuwa drug addict na sasa dawa hizo hazipo mtaani"
Amesema Sianga
Sianga amesema mara baada ya kupokea kijiti cha mapambano kutoka kwa
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mamlaka hiyo imeendelea na
moto huo huo, na kwamba kwa hivi sasa timu yake hailali, ikiendelea na
mapambano kila siku na kwamba hata leo, kuna mtuhumiwa mkubwa wa dawa za
kulevya amekamatwa.
"Leo asubuhi tumemkamata mtuhumiwa mmoja mkubwa wa dawa kulevya, tupo
naye tunaendelea kumuhoji, mengi yataibuka" amesema Kamishna Sianga
Kuhusu kuendelea kutumia mbinu iliyokuwa ikitumiwa na Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam paul Makonda ya kutaja majina hadharani,, Kamishna Sianga
amesema hatatumia njia hiyo kwa kuwa kutaja majina ya watu hadharani
kunaweza kuiingiza serikali katika matatizo maana kuna watu wengine
wanaweza kutoa majina ya watu kwa sababu ya chuki binafsi.
Amesema njia anayoitumia ni kuwakamata na kuwahoji kimyakimnya na wakishajiridhisha hatua nyingine za kisheria zinafuata.
Katika hatua nyingine, Sianga amesema Tanzania iko makini katika
kuwashughulikia wahusika wakubwa wa dawa za kulevya duaniani tangu miaka
mingi iliyopita, akitolea mfano mtuhumiwa mmoja wa kike ambaye ni gwiji
katika biashara hiyo au 'King Pin', ambaye hivi sasa amefungwa katika
magereza ya Tanzania tangu mwaka 2010
"Tulimkamata mmoja kati ya watu waliokuwa wametajwa kama king pin wa
dawa hizo nchini Marekani, alikuwa ameshindikana, na huko Marekani
alikuwa na kesi zaidi ya 40, lakini alikamatwa hapa na amefungwa tangu
mwaka 2010, yuko gerezani nafikiri kama siyo Keko, ni Segerea". Amesema
Sianga.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza HapaFollow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment