Ligi
Kuu ya Mpira wa Wanawake, hatua ya timu sita Bora (6), ilianza rasmi
jana kwa Mlandizi Queens ya Pwani kuilaza JKT Queens ya Dar es Salaam
mabao 3-2 katika mchezo wa awali mchana kabla ya ule wa jioni Sisterz ya
Kigoma kuifunga Fair Play ya Tanga mabao 5-1.
Ligi
hiyo inayochezwa Kituo kimoja cha Uwanja wa Karume, Ilala Dar es Salaam
inakutanisha timu sita zinazowania ubingwa wa ligi hiyo ya wanawake
ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania. Pia ni ya kwanza
kwa nchi za Afrika Mashariki.
Timu
sita zilizofanikiwa kufika hatua ya Sita Bora ni JKT Queens ya Dar es
Salaam, Mlandizi Queens ya Pwani na Fair Play ya Tanga kutoka Kundi “A”
wakati kutoka Kundi “B” zimo Marsh Acedemy ya Mwanza, Sisterz ya Kigoma
na Panama ya Iringa.
Mara
baada ya mechi za jana Februari 26, 2017; ligi hiyo sasa itaendelea
kesho Februari 28, mwaka huu ambako kwa michezo ifuatayo:
Februari
28, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Marsh Academy na Panama saa
8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Mlandizi
na Fair Play.
Machi
2, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Sisterz na Marsh Academy saa
8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Panama na
JKT Queens.
Machi
4, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Fair Play na JKT Queens saa
8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Marsh
Academy na Mlandizi Queens.
Machi
6, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Panama na Sisters saa 8.00
mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya JKT Queens na
Marsh Academy.
Machi
8, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Sisters na Mlandizi Queens saa
8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Panama na
Fair Play.
Machi
10, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Marsh Academy na Fair Play saa
8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Mlandizi
na Panama.
Machi 11, mwaka huu kutakuwa na mchezo mmoja tu saa 10.00 jioni ambako JKT Queens watamaliza na Sisterz.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment