Na Mwandishi Wetu, MBEYA
KIUNGO
wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Geoffrey Bonny Namwandu (37)
amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa
muda mrefu.
Dada
wa mchezaji huyo wa zamani wa Prisons ya Mbeya na Yanga SC ya Dar es
Salaam, Neema ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba
wamempoteza kipenzi chao baada ya kuhangaika naye kumuuguza kwa muda
mrefu.
Neema amesema kwamba msiba upo nyumbani kwao mjini Mbeya ambako taratibu za mazishi zimekwishaanza.
Geoffrey Bonny hali yake ilivyokuwa siku za mwisho za uhai wake
Bonny alikuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars enzi za kocha Mbrazil, Marcio Maximo na wengi wanamkumbuka kwa soka yake maridadi katika sehemu ya kiungo, licha ya kwamba aliibuliwa wakati umri wake umekwishaenda.
Alicheza Yanga chini ya kocha Mserbia, Profesa Dusan Kondic na akaendelea hata alipoondolewa mwalimu huyo na kuletwa Mseribia mwingine, Kostadin Papic. Timu ya mwisho ya Geoffrey Bonny kuchezea, Simrik SYC ya Nepal. Geoffrey Bonny (wa pili kulia waliosimama) akiwa kwenye kikosi cha Simrik SYC ya Nepal. Wa pili kushoto waliosimama ni mchezaji mwingine wa Tanzania, Pius Kisambale. Geoffrey Bonny akiichezea Taifa Stars kwenye michuano ya CHAN mwaka 2009
Ni kati ya wachezaji walioiwezesha Taifa Stars kukata tiketi ya kucheza fainali pekee za michauno ya Ubingwa wa Afrika (CHAN) zinazohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.
Hata hivyo, Maximo akamtema katika kikosi cha Stars baada ya fainali za CHAN nchini Ivory Coast mwaka 2009 kutokana na kuwa majeruhi.
Maumivu hayo yalimfanya aachwe na Yanga mwaka 2011 akaenda kumalizia soka yake Simrik SYC ya Nepal.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment