Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa mapema leo 28 Februari 2017, ameongoza mkutano
wa siku moja wa watendaji wakuu na wenyeviti wa bodi za mashirika ya
umma, unaojadili nafasi za mashirika ya Umma katika utekelezaji wa
Mpango wa Pili ya Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2016/17-2020/21),
Unaofanyika Ikulu Jijini Dar e Salaam.
Mkutano
huo ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Ofisi ya
Msajili wa Hazina,Waziri Majaliwa amewapongeza wakuu hao ambapo
amewataka kuhakikisha wanaongeza juhudi na maarifa katika mashirika yao
ili kusonga mbele.
Akisoma
hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo, Waziri Mkuu Majaliwa amewataka wakuu
hao kuongeza ubunifu zaidi ili kuongeza maarifa katika mashirika yao
hii ni pamoja na kujiendesha kwa faida ili kuipunguzia Serikali mzigo wa
kujiendesha.
Majaliwa
amelipongeza Shirika la Nyumba NHC ambalo kwa miaka ya nyuma lilikuwa
likiendeshwa kwa hasara, hata hivyo baada ya kuongeza ubunifu na kuingia
kijana mzawa, wameweza kupiga hatua na sasa wamekuwa wa mfano wa kuigwa
huku pia akipongeza baadhi ya mifuko ya Maendeleo ya Jamii pamoja na
mabenki mengine kwa ikiongozwa na benki kuu, kutokana na kuwa na
menejimenti nzuri, ubunifu na kutumia wataalamu waliobobea katika fani
zao, wameweza kufanya mambo makubwa.
“Kumekuwa
na dhana potofu kwamba Mashirika ya Umma hayatakiwi kufanya biashara,
na kwamba yakifanya biashara lazima yapate hasara inaendelea kubaki kuwa
ni dhana potofu. Ipo mifano mbalimbali” ameeleza Majaliwa huku akitolea
mifano ya nchi zilizofanikiwa kwa mashirika ya Umma kufanya vizuri
mfano
Mashirika
kama Petrobras la Brazil, Statoil la Norway, CNOOC la China ambayo ni
makubwa na yameweza kuwekeza nje ya mipaka ya nchi zao.
Majaliwa
amesema mpaka sasa Serikali imeweza kuwa na Mashirika ya umma 264
ambapo kati ya Mashirika hayo, Mashirika 65 ni Mashirika ya Kibiashara,
Mashirika 187 ni mashirika ya huduma wakati mashirika 12 ni udhibiti.
Kati ya Mashirika 65 ya kibiashara, Mashirika 8 yanaendeshwa kwa ruzuku
ya Serikali, wakati Mashirika 57 hayategemei ruzuku ya Serikali.
Awali
akifungua mkutano huo, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Profesa
Joseph Semboja amesema malengo ya mkutano ni kukusanya maoni ya viongozi
kuhusu nafasi ya mashirika ya umma katika utekelezaji wa Mpango wa Pili
wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, kuzungumzia changamoto tarajiwa
katika utekelezaji wa majukumu haya na kutoa mapendekezo ya namna ya
kukabiliana na changamoto hizo.
“Mashirika
ya Umma yana nafasi na uwezo mkubwa wa kufanikisha utekelezaji wa
Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano, 2016/17–2020/21 wenye
kaulimbiu ‘Maendeleo ya Viwanda kwa Mabadiliko ya Kiuchumi na Maendeleo
ya Watu’,” amesema Profesa Semboja.
Profesa
Semboja aliongeza, “Katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya Rais
John Magufuli, mkutano huu umewezakutanisha viongozi kutoka serikalini
na mashirika ya umma kwa lengo la kubadilishana maarifa na uzoefu wa
jinsi mashirika haya yatakavyoiwezesha Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwa
maendeleo endelevu.”
Mkutano
huo unajadili namna ya kuboresha mifumo ya kiutendaji ndani ya
mashirika na uhusiano miongoni mwa mashirika na taasisi za serikali,
kufungamanisha mipango ya mashirika ya umma na Mpango wa Pili wa
Maendeleo, kutathmini kiwango na aina ya rasilimali zinazohitajika
kuwezesha utekelezaji wa mipango na; kufanya ufuatiliaji na tathmini ya
mipango.
Jumla ya washiriki 100, kutoka wizara, mashirika ya umma na mamlaka za udhibiti takribani 52 nchini.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment