Dkt. Harrison Mwakyembe Waziri wa Sheria na Katiba ameendelea kufunguka
changamoto zilizomkwamisha kudhibiti upitishwaji wa dawa za kulevya
katika Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam wakati alipokuwa Waziri wa
Uchukuzi hadi kuzidiwa kete na Agnes Masogange
Kupitia kipindi cha Breakfast cha East Africa Waziri Mwakyembe
amesimulia kilichotokea wakati alipotaka kumdhibiti binti mmoja
aliyedaiwa kupitisha masanduku matano ya ‘materials’ za kutengenezea
dawa za kulevya aliyekamatwa nchini Afrika Kusini akitokea Tanzania.
Amesema baada ya kufuatilia sakata lile mbali na kuchukua hatua kwa watu
waliomsaidia kupitisha mzigo uwanja wa ndege, aliamua kufanya jitihada
za kumkamata binti huyo ili achukuliwe hatua, lakini muda mfupi baada ya
binti huyo kurejea nchini, yeye alihamishwa wizara, hivyo kukosa nguvu
ya kumshughulikia, hatua iliyofanya binti huyo kumfanyia “nyodo”.
Kumbukumbu zinaonesha kuwa binti ambaye alikamatwa nchini Afrika Kusini
wakati huo kwa madai hayo, na kisha Waziri Mwakyembe kumfuatilia hadi
kutimua baadhi ya watumishi wa uwanja huo Mwezi Agost mwaka 2013 alikuwa
ni ‘video queen’ maarufu nchini, Agnes Geral d ‘Masogange’.
Aidha Mwakyembe amesema kijana wake mmoja anayefahamika kwa jina la
Jingu ambaye yuko gerezani, anapaswa kuongezewa ulinzi kwa kuwa yeye
ndiye aliyekuwa jemedari wa kudhibiti dawa za kulevya uwanjani hapo,
lakini baadaye aliundiwa kesi na sasa huko gerezani anakutana na watu
ambao wanaweza kumdhuru kutokana na kwamba yeye ndiye aliyesababisha
wafungwe.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment