Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limemkamata askari feki
wa Jeshi la Magereza, Elius Msigwa akiwa amevaa sare za jeshi hilo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro,
aliwaambia waandishi wa habari kuwa mtuhumiwa huyo ambaye alimtaja kama
Elius Msigwa aliyekuwa akiwababaisha wananchi wa maeneo ya Kivule
anakoishi, alifukuzwa kazi tangu Disemba mwaka jana.
Alisema wakati mtuhumiwa huyo anafukuzwa ndani ya jeshi hilo, alikuwa na
cheo cha Koplo, lakini alipokamatwa alikuwa amevaa cheo cha Sajenti na
alikiri kuwa alifanya hivyo kutokana na kukosa nauli ya daladala.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari kwa nia ya kuomba radhi, kijana
huyo ambaye alikuwa akifanya kazi katika gereza la Keko, alisema
“Bahati mbaya siku ya juzi sikuwa na nauli ya kwenda mjini ndio nikavaa
hizi ‘uniform’ (sare). Nilikuwa nawaomba vijana wenzangu hata kama
umeacha kazi, umefukuzwa au chochote, msivae ‘uniform’ na baada ya
kutoka hapa nazirudisha hizi uniform katika kituo changu kilichokuwa cha
kazi,” alisema Msingwa.
Kamishina Sirro pia alisema jeshi hilo lilikamata watu watatu wanaodaiwa
kuwa ni majambazi katika maeneo ya Kivule, Ukonga wakijihusisha na wizi
wa kutumia silaha aina ya mapanga, kuvuta bangi na kunywa gongo.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment