Hali ya ulinzi imeimarishwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete
(JKCI) alikolazwa mfanyabiashara Yusuf Manji baada ya kuugua ghafla
akiwa polisi alikokuwa akihojiwa.
Manji aliyekuwa akihojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini hapa
alipelekwa hospitalini hapo juzi jioni akiwa ndani ya gari la wagonjwa
aina ya Toyota Land Cruiser lenye nembo ya Shirika la Umoja wa Mataifa
la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) huku gari lake aina ya Range Rover
likifuata kwa nyuma.
Askari wenye sare na wengine wakiwa na mavazi ya kiraia nje ya wodi
aliyolazwa mwenyekiti huyo wa klabu maarufu nchini ya Yanga walionekana
wakiimarisha ulinzi.
Ilipofika saa 4:13 asubuhi mfanyabiashara huyo alitoka kwenye chumba hicho na kuongozwa kuelekea upande mwingine wa jengo hilo.
Akiwa amevalia nguo za wagonjwa zenye rangi ya kijani, Manji alitembea taratibu kuelekea upande aliokuwa akielekezwa.
Alipoulizwa kuhusu uwapo wa Manji hospitalini hapo, Mkurugenzi Mtendaji
wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi alisema hawezi kuzungumzia taarifa za
mgonjwa.
Februari 8, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alitoa orodha ya
watu 65, akiwamo Manji ambao aliwataka wafike Polisi kwa ajili ya
mahojiano kuhusu masuala ya dawa za kulevya.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment