Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amekimbizwa hospitali baada ya kuugua akiwa mahabusu.
Taarifa zinaeleza, Manji ambaye alikuwa mahabusu katika kituo Kikuu cha Polisi cha Dar es Salaam, alianza kuumwa tokea jana.
“Kweli amekimbizwa hospitali na sasa anapatiwa matibabu,” alisema mmoja wa watu wake wa karibu.
Manji
alikuwa mahabusu ambako amewekwa tokea Alhamisi iliyopita baada ya
kuitwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, akitajwa katika listi ya watu
65 wanaotuhumiwa katika suala la madawa ya kulevya.
Kumekuwa na taarifa huenda kesho akafikishwa mahakamani, lakini bado maofisa wa Jeshi la Polisi wamekuwa hawataki kulizungumzia suala hilo.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment