JINA la Edward Lowassa, mmoja wa wasaka urais kwa udi na uvumba,
limeenguliwa katika hatua za awali za kinyang’anyiro hicho. Anaandika Saed
Kubenea … (endelea). ❝
Taarifa kutoka kwa watu waliokaribu na mmoja wa viongozi wakuu wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) zinasema, jina la Lowassa limeondolewa kutokana na shinikizo
kutoka kwa baadhi ya viongozi. “Ni kweli kuwa jina la Lowassa limeondolewa
katika kinyang’anyiro hiki. Wakubwa wamekuja na msimamo na wameapa kuwa
hawataki kumsikia mtu anayeitwa Lowassa akikatiza kuingia NEC ,” ameeleza mtoa
taarifa wa gazeti hili. Vikao vya uteuzi vya CCM – Kamati ya Maadili, Kamati
Kuu (CC) na Halamashauri Kuu – tayari vimeanza mjini Dodoma mchana huu. Kikao cha
NEC kinatarajiwa kuanza saa mbili usiku. Wachambuzi wa mambo ya kisiasa
wanasema, ikiwa jina la Lowassa litaondolewa katika hatua hiyo ya awali, basi
ndoto za mwanasiasa huyo kushika madaraka ya urais tangu mwaka 1995, zitakuwa
zimezimwa. Habari zinasema, kuzimwa kwa ndoto za Lowassa, kunafuatia taarifa
kuwa mchakato wa uchujaji majina ya wasaka urais, kuendeshwa na idara ya
usalama ya chama ambayo imesheheni “wabaya” wake. Katika hatua nyingine,
taarifa zinamnukuu mmoja wa viongozi wa kamati kuu akisema, chombo hicho muhimu
katika uteuzi wa wagombea urais, imegawanyika. “Mganyiko unatokana na baadhi ya
watu kutaka Lowassa asikatwe, huku wengine wakisema, sharti aondolewe,” anasema
mmoja wa watoa taarifa wa gazeti hili.
(REFERENCE)
Posted
by: Saed Kubenea ,4 mins ago
0 comments:
Post a Comment