Mwenyekiti wa wa Shirikisho la vyama
vya Watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Amon Anastaz Mpanju ambaye pia
alikuwa Mbunge wa Bunge Maalum la Katiba Mpya amejitokeza hii leo sambamba na
wana CCM wengine katika safari ya kuwania Ubunge katika Jimbo la Kawe Wilaya
ya Kinondoni.
|
Akizungumza katika ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni, Mpanju amesema huu ni wakati muafa kwake kuwatumiakia wana Kawe.
Mpanju ambaye kitaaluma ni Mwanasheria, amesema wanakawe wananafasi sasa ya kuandika historia ya aina yake si tu kumchagua mtu mlemavu bali kumchagua, kijana na mchapakazi mwenye uwezo wa kutetea na kuwasilisha hoja za kuleta maslahi kwa kawe na taifa.
“Huu
ni wakati wa wananchi wa Kawe kuandika historia ya aina yake, sit u kwa
kumchagua mtu mwenye ulemavu kuwaongoza bali kijana mwenye uwezo wa kutetea
hoja na maslahi yua wananchi na taifa kwa ujumla,”
alisema
Mpanju.
Mpanju amekuwa ni mwananchi wa 16 kujitokeza kugombea jimbo la Kawe na ni mwana CCM wa 39 kujitokeza kuomba ridhaa ya chama kuteuliwa kugombea Ubunge kwa tiketi ya chama hicho.
Mpanju amekuwa ni mwananchi wa 16 kujitokeza kugombea jimbo la Kawe na ni mwana CCM wa 39 kujitokeza kuomba ridhaa ya chama kuteuliwa kugombea Ubunge kwa tiketi ya chama hicho.
“Mimi
nitoe wito kwa watu wote wenye ulemavu nchini ambao wanasifa na vigezo
vinavyotakikana kugombea nafasi mbalimbali za uongozi nchini wajitokeze na
kufanya hivyo na watatendewa sawa sawa na wengine bila ubaguzi au unyanyapaa,”
alisema Katibu
wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe.
Mwenyekiti wa wa Shirikisho la vyama vya Watu wenye ulemavu
Tanzania (SHIVYAWATA) Amon Mpanju akizungumza na wanahabari. Kushoto ni Katibu
wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe.
Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe akimsaidia kutia
saini ya dole gumba Mpanji.
Mwenyekiti wa wa Shirikisho la vyama vya Watu wenye ulemavu
Tanzania (SHIVYAWATA) Amon Mpanju akipokea fomu kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya
ya Kinondoni, Athuman Sheshe, kwaajili ya kuomba ridhaa ya wana CCM Kinondoni
kumteua kugombea Ubunge Jimbo la Uchaguzi la Kawe katika uchaguzi mkuu Oktoba
mwaka huu.
Nae Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athumani Sheshe (pichani),
amempongeza Mpanju kwa uamuzi wake huo na kusema kuwa anatekeleza moja ya
kanuzi na sheria za Chama kuwa watu wote ni sawa na walemavu wanahaki ya
kuchagua na kuchaguliwa kuwa vipongozi.
Chanzo
(https://www.blogger.com)
0 comments:
Post a Comment