Tuesday, 14 July 2015

#YALIYOJIRI>> Mlinzi ameuwawa na Watu wasiojulikana wa mahakama ya Kingulwira Morogoro na kutelekeza mwili wake.







Waandishi  wamefika katika eneo hilo na kukuta mwili huo ukiwa umeharibika vibaya huku baadhi ya viungo vikiwa vimenyofolewa ambapo kwa mujibu wa mashuhuda na ndugu wa marehemu wamesema mtu huyo alipotea nyumbani takribani siku kumi na mbili zilizo pita hadi alipo okotwa na wachunga ng`ombe akiwa ameuawa na mwili wake ukiwa umeharibika.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa tambuka reli Adamu Mwamganga amesema amepata tarifa hizo kwa wachunga ng`ombe kisha kutoa tarifa jeshi la polisi ambapo ameeleza marehemu alikuwa na ugomvi na ndugu zake kuhusu mashamba huenda ndicho chanzo cha kifo chake .
Jeshi la polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuuchukua mwili wa marehemu na umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti wakati uchunguzi bado unaendelea.
      
            Chanzo
                          ITV





0 comments:

Post a Comment