Wakati
zoezi la uchukuaji fomu za kugombea nafasi za ubunge na udiwani kwa ajili
ya uchaguzi mkuu mwaka huu likiwa limepamba moto katika vyama mbalimbali vya
siasa hapa nchini,waliokuwa madiwani wapatao 10 kutoka katika vyama vya CCM na
UDP wilayani Bariadi mkoani simiyu wamevihama vyao vyao na kujiunga na chama
cha demokrasia na maendeleo CHADEMA.
Wametangaza
uamuzi wa kuvihama vyama vyao katika mkutano wa hadhara wa chama hicho
ulofanyika katika kijiji cha dutwa.
Katibu
mwenezi wa chama hicho wilaya ya bariadi,martini moga amesema kujiunga kwa
madiwani hao kutakiongezea nguvu chama hicho hasa ukizingatia kwamba sasa hivi
wanaelekea katika uchaguzi mkuu.
Katika
hatua nyingine mwenyekiti wa mkoa wa chama hicho Wilson Mshuda amesema chama
hicho kimechukizwa na mbinu chafu zilizofanywa na aliyekuwa mbunge wa jimbo
hilo Andrea Chenge la kuzuia jimbo hilo lisikatwe wakati kuna wilaya hapa
nchini zina wakazi wachache majimbo yao yamekatwa na kwamba kufanya hivyo ni
kuwanyima wananchi kupata huduma za msingi huku mwenyekiti wa baraza la vijana
mkoa huo mark malulu akiwataka vijana wa mkoa huo kutojenga uoga katika
kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Chanzo
ITV HABARI
ITV HABARI
0 comments:
Post a Comment