LOWASSA RASMI CHADEMA BAADA ya
vuta nikuvute katika vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa), kuhusu kukubaliwa au kutokubaliwa kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Edward
Ngoyai Lowassa kujiunga na umoja huo ili kuongeza nguvu ya kisiasa, hatimaye
mwanasiasa huyo maarufu nchini amekubaliwa na tayari amejiunga rasmi Ukawa
akiwa mwanachama halisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
imefahamika. Taarifa rasmi kutoka Ukawa na kwa msemaji wa Lowassa ambaye
hakutaka jina lake litajwe, imeeleza kuwa uamuzi huo ulifikiwa baada ya
majadiliano ya kina katika Mkutano Mkuu wa Ukawa uliofanyika mapema wiki hii
huku ajenda kubwa ikiwa ni kumpokea Lowassa ili kuimarisha kambi ya upinzani
ikiwa ni pamoja na kumsimamisha kama mgombea urais wa umoja huo. Taarifa rasmi
zilizolifikia page hili zimeeleza kuwa Lowassa anatarajiwa kutangazwa rasmi
Jumapili hii hivyo maadalizi ya mkutano mkubwa wa aina yake yanaendelea. Chanzo
chetu kutoka katika mkutano huo kilisema kwa moyo mmoja, wenyeviti wa vyama
vyote vinavyounda umoja huo, yaani Freeman Mbowe (Chadema), Profesa Ibrahim
Lipumba (CUF), James Mbatia (NCCRMageuzi) na Emmanuel Makaidi (NLD), wameridhia
kuungana na Lowassa katika safari yao ya kuking’oa CCM madarakani huku
wakiamini kuwa wakimsimamisha kuwa mgombea wa Ukawa watafanikisha azma ya vyama
vya upinzani kuingia ikulu. “Katika kikao chetu tulijadili mikakati kadhaa ya
kuchukua dola lakini kubwa zaidi lilikuwa ni jinsi ya kuungana na Lowassa ili
kutimiza azma hiyo, ikizingatiwa kwamba hivi sasa anaungwa mkono na Watanzania
wengi na hasa jinsi ambavyo hawakuridhishwa na mchakato wa kumuengua kuwania
urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), hivyo tuna uhakika kwa mkakati
huu lazima tuking’oe CCM madarakani,” alisema mjumbe mmoja wa Mkutano Mkuu (jina
limehifadhiwa).
TUNDU LISSU AFUNGUKA Akizungumzia suala hilo,
Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, aliwaambia
wahandishi wa habari hili kuwa majadiliano kuhusu Lowassa yalikuwa ya lazima
kwa kuwa katika muungano wa vyama kila kiongozi ana mtazamo wake hivyo, kila
jambo la muhimu lazima lifanyike kwa majadiliano ili kufikia mwafaka kwani
lengo ni kuhakikisha kwamba kunakuwapo na mkakati wa pamoja kuhakikisha kuwa
CCM kinag’olewa madarakani ili makada wa chama hicho waelewe kuwa sasa Watanzania
wanahitaji mabadiliko na si maneno matupu ya majukwaani.
LIPUMBA NAYE ANASEMA Kwa upande wake,
Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, Profesa Ibrahim Lipumba alisema kwamba Ukawa hivi
sasa wamejipanga kimkakati kuhakikisha wanachukua dola na kuongeza kwamba
waliokuwa wakieneza propaganda kuwa anawakwamisha wataendelea kuumbuka kwa kuwa
vyama vyote vinavyounda Ukawa ni kitu kimoja. Aliongeza kwamba, kamwe umoja huo
hauwezi kusambaratika kwani ajenda kuu ni kuindoa CCM madarakani na kuongeza
kwamba, mambo mengine kama mgawanyo wa ruzuku yatafuata baadaye kwani
yanazungumzika katika ngazi ya uongozi. MSIMAMO WA LOWASSA Msemaji wa Lowassa
ambaye kawa sasa ndiye gumzo la taifa ukiachana na Dk. John Magufuli
aliyepitishwa na CCM kuwania kiti cha urais amewahakikishia wahandishi wa habari
kuwa Lowassa ameamua kuingia Ukawa ili kuendeleza siasa za kistaarabu kutimiza
azma yake ya Safari ya Matumaini kama ambavyo amekuwa akiwaahidi Watanzania.
Alisema ameamua kuungana na Ukawa kwa kuwa anaamini kuwa lengo la vyama vyote
vya siasa ni kuhakikisha vinatimiza malengo yao ya kuwahudumia wananchi, hivyo
inapotokea katika chama kimojawapo, bado kuna nafasi ya kutumia vyama vingine
kutimiza malengo ya kisiasa. Msemaji huyo aliongeza kwamba baada ya kuenguliwa
alikuwa na kazi ngumu ya kubaini nini cha kufanya ili kutimiza azma yake ya
kisiasa, ndiyo maana alikaa kimya ili kuepusha mivutano kati yake na CCM lakini
hakuwa amekata tama kuhusu jinsi anavyoweza kuwakomboa Watanzania kutoka katika
dimbwi la umaskini, jambo ambalo alikuwa akiwaeleza katika safari yake ya
kusaka wadhamini nchi nzima. MKAKATI WA KAMPENI Msemaji huyo alisema kuwa akiwa
katika Ukawa, Lowassa ameandaa mkakati kabambe wa uhamasishaji wananchi ili
watambue kwamba azma ya kuwakomboa ipo palepale na kuongeza kuwa ana uhakika
watamuunga mkono kwani anatambua kwamba wapo pamoja naye katika safari ya
matumaini. Alisema kwamba kazi iliyo mbele yake ni kuhakikisha kuwa anaisuka
upya ‘Team Lowassa’ na atakuwa makini na baadhi ya watu waliomsaliti ili
wasiharibu mkakati wake na kuongeza kwamba watazunguka nchi nzima kufanya
kampeni za kistaarabu, zisizokashfu wanasiasa wengine ili wananchi wapime ni
kiongozi gani anafaa kati ya yeye na wengine. TATHMINI YA USHINDI Chanzo chetu
ndani ya Ukawa kilieleza kwamba, tathmini iliyofanywa hadi sasa inawapa uhakika
wa kuchukua dola kwani katika maeneo mengi, Lowassa anaungwa mkono zaidi kuliko
mgombea mwingine yeyote yule. Kilisema kuwa katikamaeneo mengi CCM haikubaliki
kutokana na kuendesha siasa za kibabe na mizengwe, jambo ambalo limekuwa likiwakera
wananchi kwani kinachotokea ni kwamba wanachaguliwa viongozi badala ya wao
kuchagua viongozi wanaowataka. Kilisema Lowassa.
0 comments:
Post a Comment