MAHAKAMA
Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi namba 301 iliyofunguliwa na
Kampuni ya kufua Umeme ya IPTL, PAP pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya PAP Bw
Harbinder Singh Sethi dhidi ya Mbunge wa Kigoma Kusini Mhe David Kafulila kwa
madai kuwa Kafulila alichafua jina kampuni hizo na muhusika huyo kwamba
walichota zaidi ya 300bn kwenye akaunt ya Tegeta escrow kinyume cha sheria na
taratibu.
Katika
shauri hilo, Kampuni ya IPTL,PAP na Herbinder Singh Sethi walitaka Mahakama
imuamulu Mhe Kafulila alipe fidia ya 310bn kwa kuchafua jina la kampuni na
mkurugenzi huyo.
Katika
kesi hiyo Mhe Kafulila alikuwa akitetewa na taasisi za kisheria za Legal&
Human Righ Centre pamoja na kituo cha Human Righ Deffenders.
Akitoa
uamuzi huo mbele ya mawakili wa Human Right Defenders na Legal & Human
Right Center wakiongozwa na wakili Mtobesya huku mawakili wa IPTL, PAP na Sethi
wakiwa hawakufika mahakamani, Jaji Rosemary Teemba alisema Mahakama Kuu
imejiridhisha kwamba kampuni ya IPTL, PAP na Mkurugenzi wao Harbinder Sethi
hawakuwa na hoja za msingi kuthibitisha madai yao kama msingi wa kufungua kesi
mahakama kuu na hivyo kwa kuzingatia hali hiyo Mahakama Kuu kanda ya Dar es
salaam inatupilia mbali shauri hilo kuanzia.
0 comments:
Post a Comment