Hatimaye
aliyekuwa mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CCM Edward Lowassa amejiunga rasmi na
chama cha demokrasia na maendeleo Chadema huku akisisitiza kuwa hakuusiki kwa
namna yoyote ile na sakata la Richimond.
Mwaka
1995 akihutubia mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma, baba wa taifa alisema miaka
25 baada ye moja ya vigogo wa CCM anakiri kwa kusema mabadiliko ya kweli yako
ndani ya upinzani.
Bw
Edward ametoa kauli hiyo ambayo inavunja ukimya na minongono ya muda mrefu
baada ya kukatwa katika harakati za kuwania nafasi ya urais ndani ya CCM,
anasema alichokishuhudia Dodoma ni ubakaji wa demokrasia.
Toka
mwaka 2008 alipojiuzulu nafasi ya uawziri mkuu jinamizi la sakata la Richimond
limekuwa likimuandama, anasema sasa inatosha.
Mwenyekiti
wa Chadema akizungumza mara baada ya kuwakabidhi kadi za uanachama Edward na
mke wake Bi Regina Lowasa anasema chama chake kimefanya maamuzi sahihi
kumualika Bw Edward Lowasa.
Hafla
hiyo ya kumkabidhi Lowasa kadi ya Chadema imefanyika jijini Dar es Salaam na
kuhudhuliwa na familia yake ikiwa ni pamoja na viongozi mbalimbali wa Ukawa.
UNAKUMBUKA
MWAKA-2008
kama kweli wewe mchambuz
namfuatiliaji wa siasa ..... kumbuka hiki.............. Lowassa Ngoyai Edward
2008 . "Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru
sana kwa kunifanya msemaji wa kwanza katika hoja hii. Lakini la pili,
nimpongeze Dk. Harrison Mkwakyembe, Mwenyekiti wa kamati Teule kwa kuwasilisha
kwa mbwembwe nyingi sana taarifa yake, mbwembwe zilikuwa nzuri kweli. Kwa kazi
nzuri kwa maoni yao, wamewasilisha vizuri. Lakini nimesimama kuweka kwenye
kumbukumbu kutoridhika kwangu na jinsi kazi hiyo ilivyofanywa. Mheshimiwa Dk.
Mwakyembe ni Mwanasheria, tena Daktari alikuwa anafundisha Chuo Kikuu. Moja ya
vitu alivyokuwa anafundisha ni "Natural Justice". Mheshimiwa Spika,
wewe ni Mwanasheria unafahamu suala la Natural Justice. Kwamba Kamati Teule
imesikiliza watu wengine wote pamoja na wanaoita minong'ono ya mitaani,
wamesafiri mpaka Marekani kutafuta mashahidi, lakini mimi ambaye ni mmoja kati
ya watuhumiwa mle hawakunihoji hata siku moja. Mheshimiwa Spika, nimesimama
kueleza masikitiko yangu. Ofisi ya Bunge mpaka ofisini kwangu hata kama
wangeniita ningekwenda kwa miguu kama hamna gari na nilikuwa tayari kufanya
hivyo. Hawa ni watu makini sana siwezi kuamini kwamba wanaweza wakafanya
oversite kama hiyo. Kwa sababu katika kila hoja walizojenga wamesema Waziri
Mkuu ilikuwa hivi. Kulikuwa na shida gani kuja kuniuliza Waziri Mkuu wanasema
uliotoa dokezo hili ni sawa sawa kweli? Kulikuwa na shida gani kwa mfano
kufuata utaratibu wa Westminster kuthibitisha hapo unaposema mwenye Richmond ni
fulani uka-lay on the table records na ushahidi kuwa ni fulani. Mheshimiwa
Spika, Taifa letu ni Taifa changa, lakini chombo hiki ndiyo mahali pa
demokrasia pakubwa katika nchi pote, hapa ndipo penyewe. Kama katika chombo
hiki haki haitaonekana kutendeka nchi yetu haitakwenda vizuri. Hapa ndipo
tunategemea tuwaonyeshe umakini wetu, umahiri wetu katika mambo ya demokrasia.
Kwa nhiyo nilichofanyiwa napenda kuweka kumbukumbu sawa kwamba naona si sahihi,
nimefadhaika sana, nimedhalilishwa sana, nimeonewa sana katika hili. Maana
zimechukuliwa tuhuma zikaelezwa hapa kwamba hivi ndivyo ilivyo. Mimi sijauliza.
Kulikuwa na shida gani kuniuliza, kwa nini muamini minong'ono ya mitaani kuliko
maelezo yangu. Sisi wote hapa ni wanasiasa tukianza kuamini minong'ono ya
mitaani niambieni mwanasiasa atakayesimama. Hatuwezi, Tume imepewa muda wa
kutosha lakini inashindwa kumuona mtu ambaye wanamtuhumu na wanamsema kwa
kirefu sana. Mheshimiwa Spika, lakini hata pale uliponinong'oneza ukaniambia
una ushahidi wowote? Nilikupa ushahidi huo wa maandishi. Katika taarifa yao
hakuna hata moja ya ushahidi ambao umetoka Waziri Mkuu. Kile kitabu cha
majedwali kimejaa majedwali mengi pamoja na magazeti mpaka ya Udaku lakini
maelezo ya Waziri Mkuu hakuna hata moja. Mheshimiwa Spika, naamini ingekuwa ni
heshima wangeiweka halafu wakasema tunakataa kitambulisho hiki kwa sababu hii
na hii, hiyo ndiyo imejengwa hoja. Lakini kujenga hoja na kuja hapa Bungeni
tunahutubia nchi nzima na kusema Waziri Mkuu amefanya hiki, amefanya hiki bila
ya kumsikiliza nachelea kuuliza hivi mtu wa chini itakuwaje? Mheshimiwa Spika,
lakini nimetafakari kwa makini sana jambo hili nikajiuliza hivi kulikoni mpaka
watu wazima wenye uwezo wao, watu maarufu wenye heshima zao, mpaka wafike
mahali waache jambo la msingi kama hilo kulikoni? Mimi nadhani there is a wish
which I am going to grant, ni Uwaziri Mkuu. Nadhani tatizo ni Uwaziri Mkuu.
Kwamba ionekane Waziri Mkuu ndio amefanya haya, tumuondolee heshima au
tumwajibishe. Mheshimiwa Spika, nimetafakari kwa niaba ya chama changu, kwa
niaba ya Serikali yangu nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumwomba niachie
ngazi. Nafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya uwajibikaji
lakini kutokubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani ya Bunge wa
kumsingizia mtu. Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kumshukuru sana Rais kwa
heshima aliyonipa ya kutumikia nchi hii kwa Uwaziri Mkuu kwa miaka miwili.
Namshukuru sana Mheshimiwa Rais. Nakushukuru wewe, nawashukuru Mawaziri na
Manaibu Waziri, nawshukuru Waheshimiwa Wabunge na wanachama wa CCM
tuliyosimamia Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi. Mheshimiwa Spika, baada
ya kusema hayo nashukuru". [07:56, 7/28/2015] rexus regregum: Kwa nini
lowasa aliitwa fisadi, hii ni kwa sababu yeye kama waziri mkuu, msimamizi mkuu
wa serikali alitakiwa akemee inshu zote za richmond, lakini, yeye alipata
shinikizo kutoka kwa Mkulu. Ndiyo maana Kuepuka Mkulu asianguke ilibidi Lowasa
ajiuzuru. Vinginevyo Mkulu angetawala Miaka mitatu tu, Na serikari yake
ingehanguka. Sasa leo Loawasa ataongea Ukweli kuhusu Richmond,ataongea Vitu
vyote ambavyo Mwakyembe aliviacha Kuongea katika Riport yake ,Kwa kuilinda
Ikulu.Hata Ongea hayo tu, Pia ataongea kuhusu wamiliki Halisi wa IPTL, pia
atagusia Mambo ya Escrow ni nani aliyeengeer Mchakato wote wa Escrow, Ataelezea
ni nani Anamiliki Kampuni ya Simba Trust, iliyochukua Bilion 75 kwenye Kashifa
0 comments:
Post a Comment