HOTUBA YA JK.. Mhe Spika, nashukuru kwa nafasi hii. Hatimaye siku
ya kulivunja Bunge imewadia. Nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi ya
kulihutubia bunge ili kutimiza wajibu wangu huo wa kikatiba. Lakini shukrani
yangu kubwa ni kwako kwa kuliongoza bunge hili kwa uhodari mkubwa. Hakika wewe
ni nahodha makini na jemedari hodari. Wewe ndiye mwanamke wa kwanza kushika
wadhifa huu wa juu kabisa katika muhimili huu wa kutunga sheria. Na
umethibitisha ya kuwa 'Wanawake wakipewa, wanaweza'. Niwashukuru wabunge kwa
kushiriki vema shughuli za bunge na mmelitendea haki na kuliletea heshima na
hadhi. Kikwete: Nilipofungua Bunge la tisa, nilisema; 'Tutatelekeza wajibu wetu
kwa Ari mpya. Nguvu mpya na Kasi mpya'. Niitaja vipaumbele vya kufanyia kazi na
ilipofika awamu ya pili, nikafungua Bunge la 10 kwa "Ari zaidi, Nguvu
zaidi na kasi zaidi". Kikwete: Tumekutana na changamoto nyingi sana kama
taifa, ikiwemo dalili za chuki za kidini, lakini kupitia mazungumzo tumeweza
kukabiliana na changamoto hiyo kwa kushirikiana na viongozi wa dini na
wengineo. Kikwete: Wanaozungumza hawagombani na humaliza tofauti zao bila
kugombana Kikwete: Nawashukuru wananchi wote kwa ushindi tulioupata kudumisha
Umoja wa Nchi yetu; tahadhari ni muhimu bado. Kikwete: Kama kura ya Maoni ingefanyika
tukapata Katiba Mpya, tungekuwa hatuongelei kero kadhaa Kikwete: Nawashukuru
wabunge kwa kuupitisha Muswada wa Gesi na Mafuta Kikwete: Mazingira ya Kisiasa
visiwani Zanzibar yamekuwa bora kuliko awali kabla ya Muafaka kati ya CCM na
CUF Kikwete: Nchi yetu iko salama, mipaka iko salama. JWTZ imefanya kazi na
Jeshi letu limeimarishwa nyanja zote Kikwete: Jeshi letu lina utayari wa kivita
kwa kiwango cha hali ya juu. Weledi umepanda kwa kiwango kikubwa Kikwete:
Namaliza kipindi changu kama Amiri Jeshi Mkuu kwa kujiamini, kwamba tupo
salama! Kikwete: Mwaka 2005/2006 kulikuwa na matukio makubwa ya Ujambazi,
niliahidi kupambana nao. Tumewadhibiti, hali ni tofauti sasa Kikwete: Lazima
tuendelee kutafuta muarobaini wa ajali za barabarani Kikwete: Changamoto kubwa
iliyopo hadi sasa ni msongamano wa wafungwa magerezani Kikwete: Serikali
imetimiza wajibu wake, Bunge limefanya kazi kubwa! Kikwete: Iwapo Katiba
Pendekezwa itapita, nchi yetu itapata heshima kubwa sana Kikwete: Tumeimarisha
demokrasia, wanasiasa wanaandamana, wanatoka nje ya Bunge. Kikwete: Habari
kubwa nchini kwa sasa ni Uchaguzi Mkuu. Tarehe 25 Oktoba ni siku ya Uchaguzi;
maandalizi yanaendelea Kikwete: Tumefanikiwa sana kutoa Uhuru wa Vyombo vya
Habari! Tuna magazeti ya Ijumaa, Uwazi, Sani... Kikwete: There's no Media
Censorship in Tanzania #PressFreedom Kikwete: Nasikitika kuwa hatukuweza kupata
Sheria ya Haki ya Kupata Habari na Media Services Bill; wenzetu wajao
watamalizia! Kikwete: TAKUKURU imepewa meno ya kudhibiti na kupambana na
Rushwa. Ina ofisi kila Mkoa na kila Wilaya Kikwete: Tumepata mafanikio makubwa,
mapato ya Serikali yameongezeka. Bajeti ya Serikali imekuwa mara 5 ya mwaka
2005 ilivyokuwa
Kikwete: Tumepunguza utegemezi wa misaada katika Bajeti toka 42%
hadi 8% kwa kusimamia ukusanyaji mapato Kikwete: Sehemu kubwa ya Fedha za
Serikali inaenda ktk Ununuzi wa Huduma; bila usimamizi mzuri wizi hutawala!
Kikwete: Nafurahi kuwa Taarifa za CAG zinapewa uzito mkubwa na hatua
huchukuliwa. POAC/PAC imefanya kazi nzuri pia Kikwete: Pale inapobainika kuna
wizi, hatua za haraka kuwajibisha wahusika zinachukuliwa hata bila kusubiri
kuwasilishwa Bungeni Kikwete: Hati zimeongezeka Serikalini tokana na utendaji
mzuri wa Ofisi ya CAG. Tuliajiri vijana wenye CPA km 780 hivi na kuwasambaza
nchini Kikwete: Ili shughuli zilizopangwa katika Bajeti ziweze kufanyika,
inabidi Hazina itoe fedha kwa wakati Kikwete: Tumeongeza Majaji wa Mahakama ya
Rufani toka 8 hadi 16. Majaji wanawake wameongezeka toka 8 hadi 37! Kikwete:
Tunao majaji wakazi 1,266 na kati yao majaji wanawake ni 534 Kikwete:
Mrundikano wa kesi utakuwa historia katika muda mfupi ujao tokana na ongezeko
la majaji na mahakimu Kikwete: Ujenzi wa Mahakama kila Mkoa unaendelea katika
Mikoa 9. Tunatenganisha kazi ya Upelelezi na Kushtaki Kikwete: Nimeamua
kuanzisha Mkoa mpya wa Songwe kwa kuugawa Mkoa wa Mbeya. Wilaya za Ubungo,
Kigamboni zimeanzishwa Kikwete: Kila mwaka tumeongeza kima cha chini cha
mshahara toka TZS 65,000/= (2006) hadi TZS 300,000/= (2015) Kikwete: Idadi ya
wabunge wanawake imeongezeka toka 62 hadi 127 sasa! Kikwete: Vyuo vikuu
kulikuwa na wanafunzi wa kike 10,000+ mwaka 2005 na sasa wamefikia 78,000+
Kikwete: Pato la Taifa limekua kwa 7%, Tanzania ni miongoni mwa mataifa 20
Duniani yenye uchumi unaokua kwa kasi Kikwete: IMF wanasema Pato la Tanzania ni
kubwa kuliko walivyodhania. Tumebakiza kidogo sana kuingia kwenye Nchi za Pato
la Kati Kikwete: Mauzo yetu nje (export) yameongezeka mara 7; mfumko wa bei si
mkubwa Kikwete: Tulianzisha BRN, tulianza na sekta 6; tukaongeza nyingine 3. Ni
mpango wenye manufaa makubwa Kikwete: Tulianzisha PPP ili kuweza kurahisha
ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi Kikwete: Tanzania
0 comments:
Post a Comment