Rais
wa Ufaransa, Francois Hollande, ametaka kuundwe serikali kamili ya Ukanda wa
Ulaya, itakayokuwa na bunge lake na bajeti yake nzima. Katika mahojiano na
gazeti moja la nchini Ufaransa, bwana Hollande amesema kuwa mkasa ulioikumba
Ugiriki ni ishara tosha kuwa na ushirikiano wa karibu zaidi kati ya nchi
wanachama wa Ulaya na hata utumiaji wa sarafu moja.
Huku
hayo yakitokea, nchini Ujerumani, Chansela Angela Merkel ameambia vyombo vya
habari kuwa yuko tayari kujadili uwezekano wa kusamehe sehemu ya deni la
Ugiriki, lakini kwa sharti kuwa maelezo yote yakamilishwe katika makubaliano ya
punde zaidi ya kuukomboa uchumi wake kupitia deni lipya.
Hatma
ya Mabenki
Hii
leo mabenki ya Ugiriki yanatarajiwa kufunguliwa baada ya kufungwa kwa wiki 3.
Mabenki
hayo hata hivyo yanafunguliwa huku kkodi inayotozwa kwa bidhaa muhimu
ikipandishwa ikiwemo pia kwa mahoteli na sekta nzima ya usafiri. hatua hii
inanuiwa kurejesha imani a raia wa ndani ya Ugiriki na hata jamii ya kimataifa
nje ya Ugiriki kufuatia msaada uliokuja kwa masharti ya kufanywa mageuzi
kusainiwa wiki iliyopita na hivyo kukomboa nchi hiyo isifilisike.
Bado
idadi ya juu zaidi ambayo raia wataruhusiwa kutoa kwenye akaunti zai itaendelea
kudhibitiwa na benki kuu ya nchi. awali idadi hiyo iliwekwa kuwa Euro 60 kwa
siku, japo sasa kuna matumaini idadi hiyo ikaongezwa hadi Euro 240 kwa siku.
hata hivyo wengi wa raia wanasema kuwa kwa muda mrefu uchumi wa nchi hiyo
umeharibika na wameshazoea kuishi kwa hata chini ya idadi hiyo kwa siku
Chanzo
BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment