Wimbo mpya wa rapper Nikki Mbishi, I’m Sorry JK umefungiwa.
Uamuzi
huo umekuja saa chache baada ya rapper huyo kuitwa na Baraza la Sanaa
la Taifa, BASATA Jumatano hii kujielezea kuhusiana na wimbo huo. Kupitia
Instagram, Nikki amewaonya watu dhidi ya kuusambaza wimbo huo kwakuwa
mkono wa sheria utawaangukia.
“Naomba
niombe radhi kwa vyombo vyote vya habari kuwa sitoweza kuwapa
ushirikiano wowote kuhusu wimbo wangu wa “I’M SORRY JK” uliositishwa na
hii ni kwa usalama wao na wangu pia,” ameandika kwenye Instagram.
“Napokea
simu nyingi sana zikihitaji maelezo juu ya suala hilo ila kiukweli kwa
watakaohitaji taarifa kamili wanaweza kufika ofisi za BASATA,naomba
nisiwe msemaji tena juu ya jambo hili,” ameongeza.
Pia ameonya, “Kwa
yeyote atakayeendelea kuusambaza au kuucheza popote pale mimi
sitohusika naye maana technology iko huru popote duniani na siwezi
kuzuia watu wasiupate kwa kuwa ushasambaa,hivyo chukua tahadhari ili
usijikute mikononi mwa sheria. Asanteni sana,naomba msubiri ujio wangu
mpya wa #SINGELI na aina nyingine za muziki kama #NAIJA #MCHIRIKU n.k.”
Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ameandika kwenye Facebook: Serikali
imepiga marufuku wimbo wa msanii Nikki Mbishi. Wallah nilidhani ni
utani kumbe Kweli? Serikali hii inachoogopa ni nini? Dah kua uyaone.”
Bofya hii link usikilize nyimbo iliyofungiwa inayoitwa "‘I’m Sorry JK’ Nikki Mbishi>>>>>Bofya hapa hapa
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment