MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetoa zuio la muda kwa Jeshi la
Polisi kuacha kumkamata Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Freeman Mbowe hadi maombi yake ya kupinga kukamatwa
aliyowasilisha mahakamani hapjana yatakaposikilizwa Ijumaa Februari 24,
mwaka huu, saa saba mchana.
Aidha mahakama hiyo pia imemtaka Mbowe kurekebisha hati ya mashtaka na
kumwingiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, katika kesi yake ya Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro na Mkuu wa Upelelezi wa kanda hiyo,
Camilius Wambura aambapo ametakiwa kuyawasilisha Jumatatu, Februari 26,
mwaka huu.
Wakati kesi hiyo ikiendelea katika chemba namba 64, mahakamani hapo,
Kamanda Wambura pekee kati ya walalamikiwa waliotajwa katika kesi hiyo
ndiye aliyeonekana mahakamani hapo na kupotea ambapo haikufahamika mara
moja alikwenda wapi.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment