Friday, 24 February 2017

Dr Harrison Mwakyembe Aonywa na Chama cha Wanasheria Afrika Mashariki.Fahamu zaidi hapa.

Chama cha Wanasheria Afrika Mashariki (EALS) kimemwandikia barua Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe kikimtaka aache kuingilia uchaguzi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Barua hiyo imekuja baada ya Dkt. Mwakyembe kudaiwa hivi karibuni kutishia kuifuta TLS kwa madai kwamba imeanza kuingiliwa kisiasa.

Barua hiyo iliyoandikwa na kusainiwa na Rais wa EALS, Richard Mugisha, inasema TLS si chama cha kisiasa na kimeanzishwa kwa kufuata sheria zote.

“Mheshimiwa Waziri, tumesikitishwa na taarifa ambazo zimeenea kwenye vyombo vyote vya habari na gazeti la East African la Februari 18 ambalo limekunukuu ukisema kwamba Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kina muingiliano wa kisiasa,” inasema sehemu ya barua hiyo.

Katika barua hiyo, Mugisha anasema wanasheria wanatakiwa wapewe uhuru, wasiingiliwe na serikali kama ilivyo kwa nchi nyingine kwani kuingilia ni sawa na kuvunja sheria za nchi.

Rais wa sasa wa TLS, John Seka amesema kuwa chama chake kimefurahishwa na barua hiyo kwa Waziri na kwamba nao pia wanafanya taratibu kumuona ili kujadili mustakabali wa chama hicho.

Alisema kuwa TLS inaendelea na mchakato wa uchaguzi kama ulivyopangwa na kuwataka wagombea wote kujiandaa kwa uchaguzi huo ambao alisema ni halali.

Uchaguzi wa chama hicho unatarajiwa kufanyika machi 18 mwaka huu, huku wagombea kutoka vyama vya upinzani wakiwa wamejitokeza kuwania nafasi ya uongozi wa juu.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa


Related Posts:

  • SIRI ya Marekani Kufanya Njama za Kutaka Kumuua Rais wa Korea Kaskazini Zavuja. Maajenti wa Marekani na Korea Kusini wanapanga njama ya kumuua kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, vyombo vya habari nchini humo vimesema. Taarifa kutoka wizara ya usalama nchini Korea Kusini imesema mawakala wa kun… Read More
  • Sugu Amvaa 'Bashite' Bungeni. MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amemshambulia Bashite huku akisema kuwa mtu huyo alipaswa awe mahakamani na sio ofisini kwa madai kuwa amefoji vyeti vya elimu ya sekondari jambo ambalo ni kosa kisheria. Ha… Read More
  • Machangudoa Wajilipua Kwa Rais Magufuli. DAR ES SALAAM: Kama mbwai na iwe mbwai! Ndivyo wanavyosema baadhi ya wasichana wanaojihusisha na biashara haramu ya kujiuza (machangudoa) sehemu mbalimbali jijini Dar wakimaanisha liwalo na liwe baada ya kuamua kujilipua… Read More
  • Hali ya Mbunge wa CHADEMA Siyo Nzuri, Alazwa Muhimbili. Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche alifikishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jana akitokea Dodoma kwa ajili ya matibabu baada ya kyzidiwa ghafla. Mbunge huyo anasumbuliwa na uvimbe ambapo mdogo wake, Edwa… Read More
  • Mauaji mengine yatokea Rufiji. Rufiji.Mtu mmoja Aitwae Amri Chanjale (55), mkazi wa kitongji cha Makaravati katika Kijiji cha Umwe Kusini wilayani Rufiji ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa nyumbani kwake. Tukio hilo limetokea jana saa 1.30 usiku baada y… Read More

0 comments:

Post a Comment