Thursday, 15 March 2018

Breaking News: TFF Yamfungia Maisha Kujihusisha na Msuala ya Soka Michael Wambura.

Habari za ndani zinasema Kamati ya Maadili ya TFF imemfungia makamu wa Rais wa Shirikisho hilo, Michael Wambura kutojihusisha na soka maisha yake yote.


TFF imetangaza rasmi maamuzi ya Kamati hiyo saa 6 mchana muda ambao Wambura pia amepanga kuzungumza na waandishi wa habari baada katika hoteli ya Courtyard Upanga jijini Dar es salaam.


Sekretariati ya Shirikisho la soka Tanzania TFF ilimfikisha Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura kwenye kamati ya maadili akikabiliwa na tuhuma tatu ikiwemo kupokea fedha za malipo TFF za malipo ambayo hayakuwa halali.

Jana mchana afisa habari wa TFF Clifford Mario Ndimbo aliwaambia waandishi wa habari kwamba Wambura amefanya makosa hayo huku akijua anashusha hadhi ya shirikisho hilo ikiwa ni kinyume na katiba ya TFF.

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya TFF, baada ya kamati ya maadili kupokea malalamiko yanayomhusu Wambura na kukutana jana (Machi 14, 0218) kwa ajili ya kujadili, imemfungia maisha Wambura kujihusisha na masuala ya soka.

Kwa mujibu wa afisa habari wa TFF Clifford Ndimbo, Wambura alikuwa na uhuru wa kufika mwenyewe mbele ya kamati na kutoa utetezi wake kwa njia mdomo, kutuma kwa maandishi au kupeleka mashahidi au kutuma mwakilishi ambaye ataambatana na barua ya uwakilishi. Wambura alituma mwakilishi ambaye ni Wakili Emanuel Muga kwa ajili ya kumtetea


Emmanuel Muga amesema hakupewa nafasi ya kumtetea mteja wake kwa sababu kamati ilikuwa na dhamira yake ya kutaka kulimaliza suala hilo siku hiyohiyo (jana Machi 14, 2018).

“Ni kweli sikupewa nafasi ya kumtetea kwa sababu kamati ilikuja ikiwa na dhamira yake kutaka kulimaliza suala hilo siku hiyohiyo. Kwa hiyo nilivyowasilisha masuala ya kisheria ambayo ni ya kikanuni, kamati ilikataa ikasema sisi tunaamua tunavyoona”-Emanuel Muga, Wakili wa Wambura.

“Kwa hiyo wakalifunga suala kwamba yanaenda kufanywa maamuzi, lakini hayo maamuzi yatafanyika wakati Wambura hajasikilizwa na Wakili wake hajasikilizwa.” 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Zinaweza zikafungiwa nyimbo zetu zikachezwa za kina Nicki Minaj – Diamond.

Zinaweza zikafungiwa nyimbo zetu zikachezwa za kina Nicki Minaj – Diamond
Msanii Diamond Platnumz bado anaonekana kutokubaliana na uamuzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) wa kuzifungia nyimbo zake mbili ambazo ni Waka na Hallelujah.

Muimbaji huyo akizungumza na Classic FM nchini Kenya amesema serikali ni lazima iangalie maudhui ya wimbo husika na msanii husika nini hasa alilenga.

“Huwezi kuimba nyimbo za mapenzi usitaje maneno ya kimahaba, ni uongo kwa sababu utakuwa haufikishi ujumbe,” amesema.
“Nyimbo kama Waka na Hallelujah ni nyimbo ambazo nilifikiria kufanya kitu ili soko lingine watusikilize, serikali lazima ielewe. Na kinachouma zaidi zinaweza zikafungiwa nyimbo zetu zikachezwa za kina Nick Minaj, so ni lazima tuangalie,” amesisitiza Diamond.

February 28 mwaka huu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilipokea list ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kutoka kwa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) na kuamuru kutopigwa katika vyombo vya habari. Katika list hiyo Nay wa Mitego alifungiwa nyimbo tatu na Diamond nyimbo mbili.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Wednesday, 14 March 2018

BREAKING: Goodnews Kwa Watanzania Watakaopenda Kufanya kazi Mradi wa Bomba la Mafuta.

Watanzania watakaopenda kufanya kazi katika Bomba la Mafuta, Bonyeza PLAY hapa chini kutazama. VIDEO: 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Irene Uwoya Ampa Onyo Kali Dogo Janja " Thubutu Uwone Tena Ndo Utanijua ".

Mke wa msanii wa muziki Dogo Janja, Irene Uwoya ametoa majibu juu ya habari zilizopo za mumuwe kutaka kuongeza mke wa pili hadi wanne.

Uwoya ametoa majibu hayo baada ya kukuta habari zimezagaa katika mitandao mbalimbali juu ya mpingo ya mumuwe aliyoweka ya kutaka kufikisha idadi ya wake wanne katika ndoa.

“Ndoutajua mim Kabila gani…thubutu uwone tena wasikudanganye @dogojanjatz,” ameandika mrembo huyo katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram mapema leo baada ya kuona stori za mumuewe za kumuongezea mke zikitawala.

Katika kipindi cha The Playlist ya Times Fm kilichoruka juzi ( 12-03-2018) mkali huyo wa ‘Wayu Wayu’ alidai kuwa anampango wa kuongeza mke wa pili hadi wanne kila baada ya miaka 10. 
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Tuesday, 6 March 2018

Kumbe Daxx Ndo Baba Kijacho wa Dayna Nyange..... Dayna Afunguka A-Z "Ujauzito Haujifichi".

Msanii Dayna Nyange amezungumza na kuelezea skendo zilizopo za yeye kuhusishwa kutoka na Daxx ambaye ni Fashion Model na ameonekana kwenye video mpya ya Dayna Nyange ya ‘Sale Sale’ ikiwa ni pamoja na kuhusishwa kuwa mjamzito.

Dayna Nyange amesema kwamba yeye anamahusiano na Daxx lakini siyo ya kimapenzi kwani yeye anaye mpenzi wake na ishu ya yeye kuwa na mimba kasema hajawahi kusema kama ni mjamzito lakini Mimba haijifichi na kama ipo watu wataona na waandae Pampas na maziwa ya mtoto.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Gazeti Lililomuandika Mange Vibaya Lapewa Onyo Kali na Serikali.

Serikali imelionya Gazeti la Tanzanite kwa kuchapisha picha za utupu kitu ambacho ni kinyume na maadili ya kazi hiyo.

Hatua hiyo imekuja baada msemaji wa serikali Dkt. Hassan Abbas kuahidi kulichukulia hatua gazeti hilo baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kutokana na ukakasi wa habari zake pamoja na picha wanazochapisha.


Onyo hilo limetolewa hii leo mjini Dodoma na Msemaji wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema kuwa wametoa onyo kwa Gazeti hilo kwakua ni jipya pia ni mara yake ya kwanza kutenda kosa kama hilo hivyo ni bora kujirekebisha.

Amesema kuwa Gazeti hilo halikuwa na kosa katika maudhui ya kuandika ila kosa kubwa ni kutumia picha za utupu, hivyo kwenda kinyume na maadili.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Breaking News: Moto Mkubwa Waunguza Soko Mbagala.

Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii Machi 6, 2018.

Sehemu iliyoathirika zaidi ni ile ya wauza mitumba huku baadhi ya bidhaa zao zikiteketea kwa moto lakini hakuna aliyeripotiwa kupoteza maisha wala kujeruhiwa.

Chanzo cha moto huo kinadhaniwa kuwa ni hitilafu ya umeme ambapo tayari gari la jeshi la zima moto limefika  kuzima moto huo.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Picha: Hivi Ndivyo Polepole Alivyonusurika Kufa Baada ya Msafara Wake Kupata Ajali.

Msafara wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Hamphrey Polepole umepata ajali katika eneo la kijiji cha Nyamidaho, Kata ya Makere wilayani Kasulu mkoani Kigoma.


Ajali hiyo imehusisha gari aina ya Toyota V8 yenye namba T150 EWE iliyokuwa ikiendehswa dereva aliyefahamika kwa jina moja la Kibuta wakati wakielekea katika ziara ya kiongozi huyo wilayani Kakonko, mkoani humo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma ACP Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza chanzo cha ajali hiyo kuwa ni kupasuka kwa gurudumu la nyuma upande wa kulia.

Kwa mujibu wa Kamanda Otieno, waliojeruhiwa ni pamoja na Katibu wa CCM mkoa Naomi Kapambala, Mwenyekiti wa UVCCM Sylivia Sigura pamoja na Katibu Mwenezi, Feruz ambao wamekimbizwa katika hosiptali ya wilaya ya Kibondo kwa matibabu.

Poplepole amewasili leo mkoani Kigoma na kupokelewa wilayani Uvinza akitokea mkoani Tabora ambapo atakuwa Kigoma kwa takribani siku tatu


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Simba Yadhamiria Kuwamaliza Al Masry.

ILI kuhakikisha wanakiimarisha kikosi chao kila upande kuelekea mchezo wao dhidi ya Al Masry kutoka Misri, wachezaji wa Simba jana walishiriki darasa la saikolojia chini ya daktari na mwanasaikolojia maarufu nchini, Chris Mauki.


Mara ya kwanza Simba kumuita mwanasaikolojia huyo ilikuwa ni katika maandalizi ya mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC na vinara hao wa ligi waliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Emmanuel Okwi.

Simba inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya SportPesa inatarajia kuwakaribisha Al Masry katika mechi ya kwanza ya raundi ya Kombe la Shirikisho Afrika itakayofanyika kesho kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Mauki ametoa darasa na kuwaeleza wachezaji wanavyotakiwa kujijenga ujasili pale wanapokuwa ndani ya uwanja wakipambana kusaka ushindi.

"Mwanasaikolojia huyo aliwaambia aliwaeleza namna mchezaji anavyopaswa kujitambua na kujiamini pindi anapokuwa uwanjani wakati wa mechi ili kuisaidia timu kupata matokeo chanya," alisema kiongozi mmoja.

Baada ya mechi ya kesho, timu hizo zitaendelea na mechi zao za ligi na baadaye kurejeana katika mchezo utakaofanyika Machi 17 mwaka huu katika mji wa Port Said huko Misri.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Wameandamana Afrika Kusini Kushinikiza Ukweli wa Kifo cha Mtanzania Alieuawa.

Wanachama wa Shirika la Africa Diaspora Forum wamefanya maandamano nchini Afrika Kusini kushinikiza serikali ya nchi hiyo na ya Tanzania kubaini ukweli kuhusu kuuawa kwa mwanafunzi raia wa Tanzania mwezi February.

Baraka Leonard Naferi, mwanafunzi wa shahada ya uzamifu, alifariki baada ya kugongwa na gari la nje ya bweni la chuo kikuu.

Maafisa wa shirika hilo wameandamana kwa pamoja na baadhi ya wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Johannesburg nje ya bweni linaloitwa Sophiatown ambapo mwanafunzi huyo aligongwa na kufariki.



Maandamano hayo yalikuwa salama na watu walikusanyika kwenye uzio mahali gari lilipo mgonga marehemu Baraka Naferi wakiwa wamebeba mabango yanayosema tunataka haki kwa Baraka, haki itendeke kwa Baraka.

Mtuhumiwa alikamatwa na polisi wa Afrika Kusini lakini baadaye akaachiliwa huru kwa dhamana. Polisi walisema hakukuwa na ushahidi wa kutosha wa kumfungulia mashtaka ya mauaji.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Friday, 2 March 2018

Rufaa ya Kupinga Hukumu ya Kifungo ya Sugu, Masonga Yapelekwa Mahakama Kuu.

Rufaa ya kupinga hukumu ya kifungo cha mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wanaotumikia jela miezi mitano imewasilisha Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya jana Machi 1, 2018 na mmoja wa mawakili wa Sugu, Faraji Mangula na kupewa kumbukumbu namba 29/2018.

“Tayari rufaa yetu imepokelewa katika Mahakama Kuu (Mbeya), sasa tunasubiri ni kupangiwa tarehe ya kuanza kusikiliza. Tunawashukuru watu wa Mahakama hii wameshughulikia vizuri jambo hili,” alisema Mangula.

Mawakili hao wamekusudia kuomba dhamana kwa Sugu na Masonga ili wawe kuwa nje katika kipindi ambacho watakuwa wanasikiliza rufaa yao.

Sugu na Masonga walihukumiwa baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli ambapo walitoa kauli hiyo Desemba 30, 2018 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Thursday, 1 March 2018

TCRA Yawazipiga Marufuku Nyimbo za Diamond, Nay, Gigy na Roma.

Mamlaka ya Mawasiliano(TCRA) imepokea orodha ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kupiga marufuku nyimbo hizo kuendelea kurushwa katika vyombo vya habari huku ikisema hatua za kisheria kuchukuliwa kwa watakaokiuka.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Bell 9 Aleta Kali Aifananisha Basata na Baba Asiyejua Jina la Mwanaye.

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Belle 9 amelishangaa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa kushindwa hata kuwajua wasanii japo hata kwa majina.


Belle 9 amesema hayo baada ya BASATA kuchanganya majina kwa kumtaja kwenye orodha ya wasanii waliofungiwa nyimbo zao jana Februari 28, 2018 badala ya kuweka jina la Roma Mkatoliki.

“Kwahiyo mimi ni Roma Mkatoliki haya basi tongwe record baby jei mada yo yo yo Roma!  Hii ni sawa na kua na baba ambaye akisikia umekosa ana kuhukumu lakini akiulizwa jina la mwanao anaitwa nani anajiuma uma halafu analitaja jina la mtoto wa jirani ambalo huwa analiskia akiwa anakuja kukuhukumu,“ameandika Belle 9 kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Soma zaidi – TCRA yazifungia nyimbo 15, Diamond na Nay maumivu zaidi

BASATA walikosea kumtaja Belle 9 kwenye kipengele cha wimbo wa Kibamia ambapo waliandika Abemego Damiani a.k.a Roma Mkatoliki.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Tanzania Yazikataa Meli za Korea Kaskazini.

Waziri wa Mambo ya Nje, Dk. Augustine Mahiga amewafahamisha  mabalozi wa nchi tano ambazo ni wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwamba meli mbili zilizoonekana zikielekea Korea ya Kaskazini zikipeperusha bendera ya Tanzania;


Inadaiwa kuwa Meli hizo zilizokuwa zikipeperusha bendera ya Tanzania zilionekana kwa njia ya satelaiti, moja ikielekea Korea ya Kaskani moja kwa moja na nyingine ilinaswa ikihamisha mizigo ambayo haikutambulika kwenye meli nyingine ambayo baada ya zoezi hilo la uhamishaji ilielekea Korea ya Kaskazini baada ya kupakia mizigo hiyo.

Balozi Mahiga amewaomba Mabalozi hao kutoka Marekani, Uingereza, Ufaransa Urusi na China kuisadia Tanzania kuweza kuzibaini meli zinazopeperusha bendera ya Tanzania na kwenda kinyume na utaratibu wa kimataifa wa usafirishaji baharini.

Januari mwaka huu Tanzania ilizifutia usajili meli zote 450 zilizokuwa zinapeperusha bendera ya Tanzania kwenye maji ya kimataifa baada ya kupatikana kwa meli iliyokuwa imebeba shehena ya silaha na dawa za kulevya huku ikipeperusha bendera ya Tanzania.

Wiki moja iliyopita Rais wa Marekani Donald Trump alitishia kuyawekea vikwazo vya Kiuchumi Kidplomasia Kisiasa na kibiashara mataifa yote yatakayokiuka vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa na Marekani dhidi ya Korea ya Kaskazini.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Timu ya Simba Yapata Pigo Mchezaji Wao Afariki Dunia.

Mchezaji wa Zamani wa timu ya Simba SC na timu ya Taifa ya Tanzania, Arthur Mambeta amefariki dunia baada ya kuugua kwa kipindi kirefu jijini Dar es Salaam.


Kutoka na taarifa hizo, Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema wamepokea ujumbe huo kwa mshtuko mkubwa kifo cha mchezaji huyo ambapo msiba wake unafanyikia Kigamboni.

"Tumepokea kwa mshtuko mkubwa kifo cha mchezaji wa zamani wa kimataifa wa klabu yetu ya Simba Arthur Mambeta ambae amefariki jana hapa jijini. Mambeta anakumbukwa sana na wanasimba pale alipotoka kwenye kustaafu soka na kuja kuisaidia klabu yake kuifunga klabu ya Yanga kwenye mchezo wa fainali Ligi kuu goli 1-0. Hiyo ilikuwa mwaka 1973 huko nyuma mchezaji huyo alikuwa ni mshambuliaji mahiri kabla ya kuja kucheza beki", amesema Manara.



                                        Marehemu Arthur Mambeta  enzi za uhai wake.

Uongozi wa EATV kwa pamoja unawapa pole wadau wa soka nchini, familia ya marehemu na klabu ya Simba kwa kuondokewa na mtu muhimu.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Breaking News: Milipuko Yatokea Katika Mahakama ya Kisutu.

Mahakama ya Kisutu imekumbwa na hitilafu ya umeme leo baada ya mvua kunyesha na kusababisha mlipuko na sintofahamu mahakamani hapo.

Hitilafu hiyo ya umeme inadaiwa kutokea kwenye moja ya vyumba katika mahakama hiyo

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Wednesday, 28 February 2018

YANGA YAANDIKA HISTORIA MTWARA, YAICHARAZA NDANDA MABAO 2-1.

Young Africans imeandika historia ya kwanza katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona baada ya kuifunga Ndanda FC kwa mabao 2-1, mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Walikuwa Yanga walioanza kucheka na nyavu za Ndanda mapema kabisa kwenye dakika ya 6 ya mchezo, baada ya Pius Buswita kutumia vema madhaifu ya mabeki wa Ndanda kwa kfunga bao la kwanza.

Na katika dakika ya 29, Hassan Kessy, alifunga bao la pili kwa mguu wa kushoto katika eneo la hatari la wapinzani wao, na kuufanya mchezo uende mapumziko kwa mabao 2-0.

Kipindi cha pili, Ndanda walikuja na uhai wakipambana kupata mabao ya kusawazisha japo ammbo hayakuwa rahisi, lakini jitihada zao ziliwasaidia kupata bao la kufutia machozi katika dakika ya 83 kupitia kwa Nassor Kapama.

Mpaka dakika 90 zinamalizika, Ndanda FC 1-2 Young Africans.

Matokeo haya sasa yanaifanya Yanga kuwa na alama 40, nyuma ya Simba iliyo na 45.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Mwimbaji Misri Afungwa kwa Kuikashifu Mto Nile.

Mwimbaji wa Misri Sherine Abdel Wahab amehukumiwa miezi sita gerezani kwa kutania juu ya hali ya usafi wa mto Nile.

Sherine, ni mmoja wa waimbaji maarufu nchini humo pia ni jaji katika kipindi cha mashindano ya waimbaji, The Voice- alimwambia mashabiki wake kuwa kunywa maji kutoka mto huo kunaweza kumpatia vijidudu.

"Kunywa Evian badala yake." akatania
Mwimbaji mwingine, Laila Amer, pia alihukumiwa siku ya Jummane kifungo cha miaka miwili kutokana na video ya muziki.

Bi Amer - ambaye hana umaarufu kama Sherine - alipatwa na hatia ya 'kuchochea ufitini na uovu". Muongozaji wa kipindi na muigizaji walihukumiwa kwa vipindi vifupi.

Sherine, amehukumiwa na mahakama moja Cairo kwa kusambaza habari zisizo za kweli. Chombo cha habari Misri, Ahram kimesema aliagizwa kulipa paundi 5,000 za Misri.

Mzaha
Mashtaka dhidi ya Sherine yalifunguliwa mwezi Novemba, baada ya kuonekana video mtandaoni ikimuonesha akiombwa kuimba wimbo uitwao Mashrebtesh Men Nilha (umewahi kunywa maji ya mto Nile?).akajibu ''Nikinywa maji ya mto Nile nitapata kichocho''. Kichocho ni ugonjwa unaojitokeza maeneo ya vijijini nchini Misri.

Mbali na kesi dhidi yake, Chama cha wanamuziki nchini humo kimetangaza kuwa kimempiga maruguku kuuimba wimbo huo kuhusu Misri.

Abdel Wahab baadae aliomba radhi kutokana na tukio hilo akiwa kwenye tamasha lililofanyika huko Jumuia ya falme za kiarabu zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Another singer, Shyma alihukumiwa kwa kucheza video ya maadili mabovu


Maamuzi ya mahakama yaliyotolewa siku ya Jumanne inafanya idadi ya wanamuziki kuhukumiwa kifungo kufikia watatu miezi ya hivi karibuni

Mwezi Desemba, Shaimaa Ahmed ajulikanaye kifupi Shyma alihukumiwa kifungo cha miaka miwili baada ya kuonekana kwenye Video ya muziki akiwa amevalia nguo za ndani huku akila ndizi kwa mbwembwe.

alikutwa na hatia ya kuweka video yenye maadili mabaya akahukumiwa sambamba na muongozaji wa video hiyo.Baadae hukumu ilipunguzwa na kuwa ya mwaka mmoja baada ya kukata rufaa.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

EXCLUSIVE:Video ambayo inayoonyesha Hoteli aliyojenga Mr. II SUGU Mbeya.




Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

CCM na Polisi Wapangua Tuhuma za Freeman Mbowe.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameibua tuhuma mpya dhidi ya baadhi ya idara za Serikali ikiwamo polisi akidai kuna mkakati wa kuwafungulia kesi ya uhaini, mauaji na ugaidi viongozi wa chama chake.

Pia, ameinyooshea kidole CCM akidai kwamba inatafuta umaarufu kwa nguvu kwa kununua madiwani.

Hata hivyo, polisi na CCM wamekana tuhuma hizo na kumtaka Mbowe aache siasa za malumbano.

Mbowe alitoa kauli hiyo jana katika mkutano na waandishi wa habari, muda mfupi kabla ya kuwaongoza viongozi wa chama hicho kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam kuhojiwa kwa madai ya kufanya maandamano kinyume cha sheria na kuachiwa kwa dhamana.

Wakati Mbowe akieleza hayo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alisema tuhuma dhidi ya polisi si za kweli na ndio maana viongozi hao walifika kituoni hapo kwa ajili ya kuhojiwa.

“Tutaendelea kuwahoji hawa viongozi kwa kufanya maandamano bila ya kuwa na kibali jambo ambalo ni kosa,” alisema Mambosasa.

Mbali ya Mambosasa, katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey Polepole pia alimjibu akisema, “Mbowe na viongozi wenzake wa upinzani wafanye siasa safi na watoe uongozi bora. Waache siasa za matukio na uchochezi kwa sababu hazibadilishi maisha ya watu. CCM tumeamua, hasa Awamu ya Tano kushughulika na shida za watu na kuwaletea maendeleo.”

Alichokisema Mbowe

Mbowe alidai kwamba mkakati wa kuwafungulia kesi hizo unatokana na matukio mbalimbali yaliyotokea ya mauaji na utekaji huku akidai vyombo vya dola vinashindwa kutimiza wajibu wake hivyo kujenga chuki miongoni mwa jamii.

Alisema kuna matukio yaliyojitokeza katika uchaguzi mdogo wa ubunge wa Kinondoni uliofanyika Februari 17 yalisababisha kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini (22) na wanachama watano wa Chadema kupigwa risasi za moto.

Akwilina aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi Februari 16 akiwa ndani ya daladala eneo la Mkwajuni, Kinondoni wakati polisi wakiwazuia wafuasi na viongozi wa Chadema waliokuwa wakiambatana kwenda ofisi ya msimamizi wa uchaguzi wa Kinondoni kushinikiza kupewa viapo vya mawakala wao.

Siku nne baadaye, Mambosasa aliwataka viongozi saba wa Chadema kufika polisi kwa mahojiano.

Mbowe alisema, “Wanatafuta namna ya kutubambika kesi za kigaidi, mauaji au za kihaini... ni mkakati wa kweli na tunamweleza Rais, hatutarudi nyuma katika kutetea demokrasia ya kweli. Mpaka sasa wanachama wetu watano kati yao wawili ni wanawake waliopigwa risasi za moto hawataki kuwapatia dhamana, wanajua wakitoka wataongea yaliyowasibu ndio maana hawataki kuwaachia wala kuwapeleka mahakamani.”

Mbowe aliendelea kutuhumu, “Risasi hizo zilielekezwa kwetu, sitaki kusema mimi ila hii si Tanzania tunayoitambua... Tumeanza kuzoea kuuana, kuumizana na wanasababisha machafuko na haya ni maonevu na haya mambo hayakuwapo zamani, tujiulize kwa nini yanatokea sasa?

“Hizi chaguzi zitaendelea kuzaa majeraha na maumivu kwani wanaosababisha wanalindwa na viongozi wa juu. Haiwezekani mawakala wetu hadi siku ya mwisho walikuwa hawajapata hati ili waibe kura na ndicho walichokifanya.”

Kuhusu madai ya kuwapo kwa mkakati wa kuifuta Chadema, Mbowe alisema unaweza kufanikiwa lakini athari zake zitakuwa ni kubwa kwa Taifa, “Wataiua Chadema lakini si mioyo ya watu, utaiua CUF na vyama vingine si hisia za watu na unapoziua taasisi kama hizi zinazowasemea watu wanatengeneza magenge huko na wataunda vikundi vya kigaidi ambavyo ni hatari zaidi.

“Chama hiki si cha kigaidi ni chama cha mikusanyiko ya watu wengi na CCM kama wanataka kurudisha imani kwa wananchi wasifanye hivyo kwa kununua madiwani, wafanye mambo yanayoeleweka na watakubalika.”

Alikuwa akizungumzia barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi aliyoiandikia Chadema akitaka ijieleze kutokana na madai ya uvunjifu wa Sheria ya Vyama vya Siasa na ile ya maadili kwa kufanya maandamano Februari 16.

Barua hiyo ya Februari 21, iliyokuwa ikitakiwa kujibiwa kabla ya Februari 25, Jaji Mutungi katika sehemu ya barua hiyo alisema licha ya tuhuma hizo kuwa zinafanyiwa kazi na taasisi zingine za Serikali, hata ofisi yake kwa namna moja au nyingine anaweza kulishughulikia.

“Hivyo, kwa barua hii, nakitaka chama chenu kuwasilisha maelezo ya kwa nini kisichukuliwe hatua za kisheria, kwa kukiuka Sheria ya Vyama vya Siasa na Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa, kwa kuchochea wananchi kuandamana bila kufuata utaratibu wa sheria na kufanya vurugu,” ilieleza sehemu ya barua hiyo ambayo tayari Chadema ilishasema kuwa imeijibu.

Hukumu ya Sugu

Mbowe alizungumzia hukumu ya mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema) Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga iliyotolewa juzi ya kuhukumiwa miezi mitano jela akidai ni mkakati ovu uliopagwa.

“Tunaheshimu sana Mahakama na Mahakama inapaswa kuheshimiwa lakini mawakili mmojammoja wanapofanya makosa wanaichafua Mahakama. Jaji Mkuu (Profesa Ibrahim Juma) alisema wanasiasa tusiingilie Mahakama, hatutaisema vibaya au kuihukumu hapana, tunawahukumu watendaji wa mahakama,” alisema Mbowe.

“Hukumu hii tuliijua siku nne kabla na mtakumbuka hakimu (Michael Mteite) tulimkataa toka mwanzo na sisi kama Chadema hatutaki kusema hatuna imani na Mahakama, lakini Jaji Mkuu kama alivyosema tusiingilie Mahakama na Jaji Mkuu anapaswa kujua hili na kama anataka kuanza, basi aanze na kesi hii ya Mbeya.”

Mbowe alisema amekuwa akiombwa na wanachama na wananchi kutoa kauli ya kulipiza kisasi kwa yanayowakuta lakini alisisitiza kwamba hatafanya hivyo akisema kutofautiana kiitikadi si kigezo cha kusababisha uvunjifu wa amani.

“Tupambane na watawala waovu na si wananchi kwa wananchi na wanaostahili kulaumiwa ni Serikali. Wanachama wa Chadema waendelee kuwa makini, tuchukue kila tahadhari kwani vyombo vinavyopaswa kutupa ulinzi havifanyi hivyo,” alisema Mbowe.

Majibu ya Mambosasa

Hata hivyo, Kamanda Mambosasa alisema tuhuma za Chadema dhidi ya jeshi hilo hazina mashiko huku akisisitiza kuwa polisi wanafanya kazi yao kwa weledi na ndiyo maana viongozi hao walikuwa wakihojiwa kituoni hapo.

“Muwaulize hao Chadema kwa nini tuhuma wazielekeze jeshi la polisi? Wao wenyewe wanajua ndiyo maana leo (jana) hii tunaendelea kuwahoji kwa kufanya maandamano bila ya kuwa na kibali jambo ambalo ni kosa,” alisema Mambosasa.

Polepole amjibu Mbowe

Polepole alipotafutwa kutoa maoni yake juu ya kauli hizo za Mbowe alisema, “Hatuna muda wa kulumbana siasa za madaraka. Mbowe asitafute mchawi nje ya chama chake na yeye mwenyewe. Anayetuharibia wigo wa demokrasia sasa hivi ni mtu ambaye anazungumza masuala ya kuhamasisha na kuleta taharuki. Anazungumzia kubeba majeneza ya Watanzania, mbona hajazungumza kubeba majeneza ya watoto wake. Mbona hasemi watoto wake wako wapi? Anapiga mawe polisi na kuandamanisha watu lakini watoto wake wako salama.”

Alisema siasa za namna hiyo hazileti maendeleo katika Taifa na kwamba CCM sasa inafuatilia kazi ambayo iliwaahidi Watanzania katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Polepole pia alizungumzia madai ya Mbowe kuhusu hukumu ya Sugu na kusema, “Mtu kigeugeu ni mbaya sana. Mahakama ikiamua yeye mbunge wake halali, mahakama nzuri. Mahakama ikimhukumu mbunge wake Sugu na wengine wanaotoa lugha ya uchochezi na uongo na wanashindwa kuthibitisha, mahakama mbaya. Huo si ustaarabu wa uongozi ni ukigeugeu wa kisiasa.”

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa