Tuesday, 6 March 2018

Simba Yadhamiria Kuwamaliza Al Masry.

ILI kuhakikisha wanakiimarisha kikosi chao kila upande kuelekea mchezo wao dhidi ya Al Masry kutoka Misri, wachezaji wa Simba jana walishiriki darasa la saikolojia chini ya daktari na mwanasaikolojia maarufu nchini, Chris Mauki.


Mara ya kwanza Simba kumuita mwanasaikolojia huyo ilikuwa ni katika maandalizi ya mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC na vinara hao wa ligi waliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Emmanuel Okwi.

Simba inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya SportPesa inatarajia kuwakaribisha Al Masry katika mechi ya kwanza ya raundi ya Kombe la Shirikisho Afrika itakayofanyika kesho kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Mauki ametoa darasa na kuwaeleza wachezaji wanavyotakiwa kujijenga ujasili pale wanapokuwa ndani ya uwanja wakipambana kusaka ushindi.

"Mwanasaikolojia huyo aliwaambia aliwaeleza namna mchezaji anavyopaswa kujitambua na kujiamini pindi anapokuwa uwanjani wakati wa mechi ili kuisaidia timu kupata matokeo chanya," alisema kiongozi mmoja.

Baada ya mechi ya kesho, timu hizo zitaendelea na mechi zao za ligi na baadaye kurejeana katika mchezo utakaofanyika Machi 17 mwaka huu katika mji wa Port Said huko Misri.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment