YANGA leo inacheza mechi ya marudiano na Wolaitta Dicha ya Ethiopia katika kufuzu makundi ya Kombe la Shirikisho, tayari timu hiyo imepambana na kuvivuka vikwazo viwili.
Kwa mujibu wa Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, timu yake imeshapambana na baridi kali iliyopo Awassa huko Ethiopia watakapocheza mechi yao pia wamemaliza tatizo la ubutu katika safu yao ya ushambuliaji.
Yanga leo inacheza mechi ya marudiano na Dicha ugenini mjini Awassa huko Ethiopia ili kufuzu makundi ya Kombe la Shirikisho baada ya awali kushinda mabao 2-0 nyumbani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza na Championi Jumatano, Nsajigwa alisema, hali ya hewa pekee ndiyo ilikuwa ikilalamikiwa na wachezaji wake na sasa wameahidi kupambana nayo.
Nsajigwa alisema: “Hatutaki kuifanya hali ya hewa ya baridi iwe sababu ya sisi kupoteza mchezo huu, nataka wachezaji kila mmoja kutimiza wajibu wake ndani ya uwanja ili kufanikisha ushindi katika mechi hiyo.
“Tulifika mapema kwenye mji huu kwa ajili ya wachezaji kuzoea hali ya hewa ya hapa ikiwa ni siku mbili tulizofanya mazoezi ya pamoja.
“Hadi kufikia siku ya mchezo huo tutakuwa tumefikisha saa 48, hivyo benchi letu la ufundi lina matumaini mazuri ya wachezaji wetu kuzoea hali ya hewa ya baridi tuliyoikuta hapa.
“Tayari tumefanyia marekebisho kwenye kikosi chetu baada ya mechi iliyopita tuliyocheza nyumbani ambayo ni safu ya ushambuliaji pekee ambayo ilikosa umakini katika kufunga mabao.”
Stori: Wilbert Molandi, Dar es Salaam
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Kwa wafuatiliaji wa mitandao ya kijamii nchini Tanzania, hususani kwa wale ambao wanamfuatilia Diamond Platnumz utagundua kuwa jana Aprili 12, 2018 aliahidi kuachia video ya wimbo wa ‘Kwa ngwaru’ ambayo amemshirikishwa na Harmonize lakini mpaka sasa hivi hakuna chochote kile walichofanya.
Diamond kupitia kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii jana aliahidi kuachia video ya Kwa ngwaru kwa kuahidi kuwa endapo angepata maoni (Comments) 10,000 kwenye posti yake aliyochapisha kwenye mtandao wa instagram, basi wangeachia video ya wimbo huo ambao umetokea kupendwa sana na mashabiki wa wakali hao lakini posti hiyo hadi sasa imefikisha comments elfu 13 na video hiyo bado haija achiwa.
Hii haina ubishi kuwa video ya utupu ya Nandy na Bill Nass imepoteza attention kwa mashabiki wengi wa muziki nchini Tanzania kutokana na ukubwa wa wasanii hao ambao kila Mtanzania alikuwa anaamini kuwa ndio zao jipya la wasanii wa kizazi kipya.
Hata hivyo, mpaka sasa hivi si Diamond wala Harmonize aliyetoa kauli yoyote ile kuhusiana na kuachia video hiyo ingawaje mashabiki wengi walitazamia kuona video hiyo kwa siku ya jana.
Kwa mujibu wa maelezo ya Nandy na Bill Nass kuhusu video yao ya utupu iliyovuja siku ya jana hadi sasa bado haijajulikana ni nani aliyevujisha kwani wamekuwa wakitupiana lawama kila mmoja.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
KIUNGO wa Simba, Haruna Niyonzima amenusurika katika ajali aliyoipata eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam.
Niyonzima amepata ajali hiyo juzi baada ya gari lake kupiga bonde na kupoteza mwelekeo wakati akirejea nyumbani kwake.
Taarifa zinaeleza Niyonzima raia wa Rwanda alikuwa mwenyewe kwenye gari na akiwa njiani wakati anarejea nyumbani, akakutana na majanga hayo.
Jana Championi lilifanya juhudi za kumpata Niyonzima aliyetua nchini kuichezea Yanga akitokea APR ya Rwanda na baada ya kumpata alithibitisha kupata ajali na kusema anamshukuru Mungu kwa kuwa haikuwa ajali kubwa.
“Gari lilipoteza mwelekeo wakati nikiwa njiani narejea nyumbani na kuingia kwenye msingi. Bahati nzuri sikuwa katika mwendo mkubwa na kuna mtu alikatiza ghafla, nilipojaribu kumkwepa nikapoteza mwelekeo wakati najitahidi kurudi barabarani, nikapiga bonde gari likanishinda nikaingia msingini.
“Haukuwa msingi mrefu, baadaye walikuja watu tukalitoa nikaondoka. Nashukuru sikuumia wala yule mtu sikumgonga hivyo hakuna aliyeumia. Gari ilipata mikwaruzo,” alisema.
Taarifa za Niyonzima kupata ajali zilisambaa jana mchana na kila mmoja alikuwa akieleza tofauti zikiwemo taarifa za kwamba aliumia na wengine wakisema alikuwa na rafiki zake.
Lakini Niyonzima alisisitiza alikuwa mwenyewe kwenye gari na taarifa hizo ziliifikia familia yake yeye akiwa nyumbani na baadhi ya watu walisema wamesikia ameumia sana, jambo ambalo halikuwa sahihi.
Niyonzima amejiunga na Simba akitokea Yanga lakini hakuwa na msimu mzuri baada ya kuumia na kulazimika kwenda kutibiwa India. Hivi karibuni ameanza kurejea taratibu akicheza mechi kwa dakika kadhaa, jambo ambalo limeamsha matumaini upya kwake.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Kwa wafuatiliaji wa mitandao ya kijamii nchini Tanzania, hususani kwa wale ambao wanamfuatilia Diamond Platnumz utagundua kuwa jana Aprili 12, 2018 aliahidi kuachia video ya wimbo wa ‘Kwa ngwaru’ ambayo amemshirikishwa na Harmonize lakini mpaka sasa hivi hakuna chochote kile walichofanya.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Wabunge wa upinzani wakiwamo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ni kama wamesusia Mkutano wa 11 wa Bunge ulioanza vikao vyake mjini Dodoma jana huku viti vyao vikionekana vitupu.
Aidha, kutokana na kutokuwapo bungeni kwa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), swali laki ilibidi liulizwe na Mbunge wa Liwale, Zuberi Kuchauka (CUF).
Wabunge hao wameshindwa kuhudhuria vikao hivyo ambapo jana wabunge waliokuwapo walikuwa wanne tu kutoka Chama cha Wananchi (CUF) na wabunge wawili wa Chadema.
Hata hivyo, leo wabunge wa Chadema hawakuwapo kabisa ambapo baadaye walionekana wabunge wawili tu, akiwamo Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na Mbunge wa Viti Maalumu, Rose Kamili ambao walionekana kwa muda mfupi kwa nyakati tofauti na kupotea.
Kubenea aliingia bungeni asubuhi na kutoka kabla ya kikao kuanza huku Kamili akionekana nje ya ukumbi wa bunge bila kuingia ndani.
Wabunge wa CUF walikuwapo lakini idadi yao ikiwa haifiki 20 wakati wa kipindi cha maswali na majibu na kubaki tisa pekee baada ya kipindi hicho.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Mwanamuziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul maarufu Diamond Plutnumz na mwanasoka wa kimataifa, Mbwana Samattapamoja na Watanzania watatu na raia wa Marekani, wameteuliwa kutunukiwa tuzo katika tamasha lililoandaliwa na Watanzania waishio ughaibuni (Diaspora) litakalofanyika Dallas nchini Marekani.
Katika tuzo hizo atapewa Dk Steve Meyer ambaye ni daktari bingwa katika Hospitali ya Mercy iliyopo jiji la Sioux, Marekani aliyewatibu manusura wa ajali ya wanafunzi wa Lucky Vincent.
Akizungumza na gazeti hili kutoka Dallas jana, mratibu wa tamasha hilo, Ben Kazora alisema wanampa tuzo daktari huyo kwa kutambua mchango wake katika kuokoa maisha ya watoto hao.
“Sote tunatambua namna ajali ilivyokuwa mbaya na ilivyopoteza wapendwa wetu wengi. Dk Meyer na timu yake walifanya kila njia kuokoa maisha ya watoto wale watatu walionusurika,” alisema.
“Tunampa Diamond zaidi kwa kutumia kipaji chake cha muziki kuitangaza nchi kitaifa na kimataifa, vivyo hivyo Samatta kwa kutumia kipaji chake cha kusakata kabumbu kuitangaza Tanzania,” alisema.
Kwa mujibu wa Kazora, mwingine ni mwanariadha John Akhwari ambaye mwaka 1968, alimaliza mbio katika michezo ya Olympic iliyofanyika Mexico City licha ya kuumia mguu.
Naye meya wa Dallas Texas nchini Marekani, Mike Rawlings aliwakaribisha Watanzania hao kushiriki tamasha la Tanzania Day, litakalofanyika jijini humo kwa lengo la kutangaza fursa za biashara na utalii.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limetoa taarifa kwa klabu za Yanga na Wolaitta Dicha SC ya Ethiopia ambayo imesema wachezaji wanne wa Yanga na wawili wa Wolaitta hawatacheza katika mechi kati ya timu hizo ambayo itachezwa mwishoni mwa juma hili kutokana na kuonyeshwa kadi mbili za njano katika michezo iliyopita baina ya timu hizo.
Wachezaji wa Yanga watakaohusika ni Kelvin Yondani, Obrey Chirwa, Papy Tshishimbi na Said Juma, ambapo kwa upande wa Wolaitta ni Teklu Tafese na Eshetu Mena.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Viongozi wa Chadema wakiongozwa na mwenyekiti wao, Freeman Mbowe wametimiza masharti ya dhamana na kuachiwa huru katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Machi 3, 2018. Mahakama hiyo imejiridhisha na nyaraka za udhamini zilizowasilishwa mahakamani hapo.
Masharti ya dhamana yalikuwa ni kila mshtakiwa kuwa wadhamini wawili watakaosaini bondi ya TZS 20m, barua ya utambulisho toka serikali za mtaa.
Aidha, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar ili kusomewa mashtaka yanayomkabiri.
Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi ameomba kufanya marekebisho ya hati ya mashtaka ili kumjumuisha Mdee katika kesi inayowakabili viongozi wenzake sita wa Chadema wanaokabiriwa na mashataka manane yakiwemo ya uchochezi, uasi na kuhamasihsa maandamano, hivyo wote kwa pamoja watasomewa mashtaka upya.
Mdee alikamatwa juzi Jumapili akiwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar wakati akiwasili kutokea nchini Afrika Kusini. Hata hivyo Mahakama imempa dhamana baada ya kuridhika na sifa za wadhamini.
Mbowe na wenzake ambao ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vincent Mashinji na manaibu wake wa Bara na Zanzibar, John Mnyika na Salum Mwalimu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko wote wanakabiliwa na mashtaka manane yakiwemo mawili ya uchochezi wa uasi yanayomkabili Mbowe na wanatarajiwa kuachiwa kwa dhamana leo.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa