Home »
Michezo
» Yanga Leo Kupambana na Wolaitta Dicha ya Ethiopia kwa Mechi ya Marudiano.
YANGA leo inacheza mechi ya marudiano na Wolaitta Dicha ya Ethiopia katika kufuzu makundi ya Kombe la Shirikisho, tayari timu hiyo imepambana na kuvivuka vikwazo viwili.Kwa mujibu wa Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, timu yake imeshapambana na baridi kali iliyopo Awassa huko Ethiopia watakapocheza mechi yao pia wamemaliza tatizo la ubutu katika safu yao ya ushambuliaji.Yanga leo inacheza mechi ya marudiano na Dicha ugenini mjini Awassa huko Ethiopia ili kufuzu makundi ya Kombe la Shirikisho baada ya awali kushinda mabao 2-0 nyumbani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Akizungumza na Championi Jumatano, Nsajigwa alisema, hali ya hewa pekee ndiyo ilikuwa ikilalamikiwa na wachezaji wake na sasa wameahidi kupambana nayo.Nsajigwa alisema: “Hatutaki kuifanya hali ya hewa ya baridi iwe sababu ya sisi kupoteza mchezo huu, nataka wachezaji kila mmoja kutimiza wajibu wake ndani ya uwanja ili kufanikisha ushindi katika mechi hiyo.“Tulifika mapema kwenye mji huu kwa ajili ya wachezaji kuzoea hali ya hewa ya hapa ikiwa ni siku mbili tulizofanya mazoezi ya pamoja.“Hadi kufikia siku ya mchezo huo tutakuwa tumefikisha saa 48, hivyo benchi letu la ufundi lina matumaini mazuri ya wachezaji wetu kuzoea hali ya hewa ya baridi tuliyoikuta hapa.“Tayari tumefanyia marekebisho kwenye kikosi chetu baada ya mechi iliyopita tuliyocheza nyumbani ambayo ni safu ya ushambuliaji pekee ambayo ilikosa umakini katika kufunga mabao.”Stori: Wilbert Molandi, Dar es Salaam
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
Related Posts:
#MICHEZO>>>>HIVI NDIVYO KANTE ALIVYOTUA CHELSEA NA KUIPA MKONO WA KWAHERI LEICESTER CITY.Fahamu zaidi hapa.
Baada ya maneno mengii, sasa hakuna mjadala kuwa N’Golo Kante ni mali ya Chelsea.
Kiungo
huyo aliyeisaidia Leicester City kubeba ubingwa, amejiunga na Chelsea
kwa day la pauni million 30 na mwenye amethi… Read More
#MICHEZO>>>TASWIRA NNE, WAZIRI MWIGULU NCHEMBA ALIVYOFIKA NYUMBANI KWA MANARA KUMJULIA HALI.Fahamu zaidi hapa.
Manara
anatarajia kuondoka nchini kesho kwenda nchini India kwa ajili ya
matibabu ya macho yake yote mawili. Moja likiwa halioni kabisa na
jingine linaona kwa kiasi kidogo kabisa.
MANENO YA HAJI MANARA, MSEM… Read More
#MICHEZO>>>>CRISTIANO RONALDO AKIWA NA BABA YAKE MZAZI KABLA YA KUFARIKI.Fahamu zaidi hapa.
Nilipokuwa mdogo,nilimuambia baba angu kuwa: “Tutakuwa matajiri na Na
tutakuwa na nyumba nzuri na kubwa” , Baba alinijibu : “Mwanangu hyo ni
ngumu” … Lkn Leo ninacho kile nilichomuambia baba, lkn sina baba yangu
kwa Sasa… Read More
#MICHEZO>>>MECHI YA KIRAFIKI TU VS WIGAN, SURA YA MOURINHO NDIYO HIVI, PREMIER LEAGUE ITAKUWAJE?...Fahamu zaidi hapa.
HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA SURA YA
KOCHA JOSE MOURINHO KWA KIPINDI TOFAUTI WAKATI AKIWAONGOZA VIJANA WAKE
KATIKA MECHI YA WIGAN LEO. ILIKUWA MECHI YA KIRAFIKI LAKINI MUONEKANO WA
MOURINHO ULIKUWA HIVI. KWENYE LIGI ITAKUWAJE?… Read More
#MICHEZO>>>>CHANONGO KASAINI MTIBWA SUGAR IKIWA NI SIKU KADHAA BAADA YA KUSAINI STAND UNITED ILIYOKATALIWA NA TFF.Fahamu zaidi hapa.
Haruna
Chanongo amejiunga na Mtibwa Sugar kwa mkataba wa miaka miwili. Awali
alisaini Stand United upande wa kampuni, hata hivyo tayari TFF
imetangaza kutoutambua upande huo na mchezaji huyo, rasmi leo amejiunga
na Mtib… Read More
0 comments:
Post a Comment