Monday, 31 August 2015

#MICHEZO>>>De Bruyne atua Man City.Fahamu zaidi hapa.

 *Januzaj ajiunga na Borussia Dortmund
*Javier Hernendez aenda Bayer Leverkusen
*De Gea atua Real Madrid
*Man U wamnasa Martial kutoka Monaco
* Borini njiapanda, Jelavic ni West Ham
Hatimaye Manchester City wamekamilisha usajili wa kiungo waliyekuwa wakimsaka kwa udi na uvumba, Kevin De Bruyne kutoka Wolfsburg, kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 55.

De Bruyne, 24, amesaini mkataba wa miaka sita Etihad na anakuwa mchezaji wa nne mkubwa kusajiliwa kiangazi hiki, baada ya Raheem Sterling kutoka Liverpoo na Timu ya Taifa ya England, Fabian Delph wa Aston Villa na mchezaji wa kimataifa wa Argentina, Nicolas Otamendi aliyekuwa Valencia.

De Bruyne ni mchezaji wa kimataifa wa Ubelgiji, ambaye anakuwa wa pili aghali katika usajili kwa klabu za England, nyuma ya Angel Di Maria aliyesajiliwa kiangazi kilichopita na Manchester United kwa pauni milioni 59.7 kutoka Real Madrid, akashindwa kung’ara na sasa ameuzwa Paris Saint-Germain (PSG).

Kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini alionesha furaha yake kumpata mchezaji huyo, na alikuwa na haya ya kusema kumhusu: “Inabidi uwe na mchezaji wa kipekee ili kuboresha kikosi. Sisi hupenda mchezo wa kushambulia sana na unaovutia, kwa hiyo kusajili mchezaji kama huyu utakuwa msaada mkubwa sana kwetu. Ana kila tunachohitaji – utimamu wa mwili, akili, ufundi na mbinu zinazotakiwa uwanjani.”

De Bruyne aliyekuwa Chelsea kabla ya kutupwa kwa madai hana kiwango, amesema anataka kufika katika kilele cha mafanikio kwa maana ya kiwango cha juu cha uchezaji soka huku akiwapatia klabu yake mataji. Amepewa jezi
Picha zaidi hizi hapa.





Sunday, 30 August 2015

#YALIYOJIRI>>>Uzinduzi wa kampeni za ubunge jimbo la Dodoma Mjini leo ambao umeongozwa na Mgombea wa Chadema+Ukawa Benson kigaila.

 Wanadodoma waliojitokeza kusikiliza mkutano wa UKAWA Uzinduzi wa kampeni za ubunge jimbo la Dodoma Mjini leo.
  Wanadodoma waliojitokeza kusikiliza mkutano wa UKAWA Uzinduzi wa kampeni za ubunge jimbo la Dodoma Mjini leo.

#YALIYOJIRI>>>Mapokezi ya Mhe.Edward Lowassa yanoga huko Iringa.Fahamu zaidi hapa.

 Mhe.Edward Lowassa  akiwaaga Wananchi wa Iringa mjini baada ya mkutano viwanja vya Gagilonga Iringa 
 Mhe.Edward Lowassa akiwasalimia wanaIringa kuelekea viwanja vya Gagilonga Iringa 
  Mgombea wa UKAWA Mhe.Edward Lowassa akiwautubia wanaIringawa kwenye viwanja vya Gagilonga Iringa.
 Mhe.laumasha akiwautubia wanaIringa kwenye viwanja vya Gagilonga.
  Waziri Mkuu Mstaafu,FredrickSumaye akihutubia Mkutano wa Kampeni Mgombea Urais UKAWA EdwardLowassa leo Iringa



 wanaIringawa Iringa wakimsikiliza mgombea wa UKAWA Mhe.Edward Lowassa viwanja vya Gagilonga Iringa.
  wanaIringawa Iringa wakimsikiliza mgombea wa UKAWA Mhe.Edward Lowassa viwanja vya Gagilonga Iringa.

 Waziri wa zamani wa Elimu Mungai akiwasil mkutano wa UKAWA viwanja vya Gagilonga.

Saa 11:56 jioni baada ya Mhe.edward lowassa kumaliza mkutano wa kampeni Iringa.

 Wafanyakaz wa Msalaba Mwekundu tayari kwa yeyote atakayepata tatizo ktk mkutano wa kampen Iringa leo.
 WanaIringa wakitembea kurudi nyumbani baada ya Edward lowassa  kuongea nao leo.

wanaIringawa Iringa wakimsikiliza mgombea wa UKAWA Mhe.Edward Lowassa viwanja vya Gagilonga Iringa.

#YALIYOJIRI>>>>Mgombea wa UraisCCM Dk. John Magufuli akisisitiza jambo kwa wakazi wa Ludewa kwenye mkutano wa kampeni za CCM Leo.Fahamu zaidi hapa.

 Dk. John Magufuli akisisitiza jambo kwa wakazi wa Ludewa hii leo
 Wanachama wa CCM wakimsikiliza Mgombea wa UraisCCM Dk. John Magufuli
 Mgombea wa UraisCCM Dk. John Magufuli akihutubia wakazi wa Ludewa kwenye mkutano wa kampeni za CCM Leo


#MICHEZO>>KOMBE LA DUNIA LA VIJANA.Fahama yaliyojiri hapa.

*Mali, Senegal robo fainali
*Nigeria watolewa na Ujerumani
Michuano ya Kombe la Dunia kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 imefika patamu, ambapo Mali na Senegal wameingia robo fainali.
Mali waliwashangaza Ghana waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kusonga mbele kwa kuwachabanga 3-0 mabingwa hao wa 2009.
Kwenye kundi lao la B Ghana waliwafunga Argentina na kuwa juu hivyo kupewa nafasi kubwa ya kuingia robo fainali.
The Eaglets waliuanza mchezo kwa nguvu na wakafanikiwa kuwaibua washabiki wao vitini katika dakika ya 20 tu pale Diadie Samassekou alipokwamisha kombora nyavuni baada ya kugongeana haraka haraka na Adama Traore.
Baada ya mapumziko walipata bao la pili kupitia kwa Diedonne Gbakle, aliyekatiza kutoka upande wa kulia, akawalamba chenga wachezaji wawili wa Ghana na kuachia fataki na kuzama chini tu ya mtambaa wa panya.
Ghana walishaona Jua limewachwea na wakati wakijaribu bila mafanikio kurudia hali yao ya zamani, walipachikwa bao jingine dakika tisa kabla ya mpira kumalizika, kwa bao la Aboubabacar Doumbia aliyewatoka walinzi wa Ghana na kuweka kitu kwenye kona ya goli.
Senegal nao walifanikiwa kuingia hatua ya robo fainali baada ya kuwafunga Ukraine kwa mikwaju ya penati, kwani katika muda wa kawaida walikwenda sare ta 1-1, shujaa wa mechi akiwa kipa Ibrahima Sy.
Licha ya kuingia katika muda wa ziada, walibakia nguvu sawa, mabao yakiwa yamefungwa na Artem Biesiedin’ dakika ya 77 na kusawazishwa na Sidy Sarr dakika ya 83.
Katika changamoto ya penati, Senegal walishinda.
Toa maoni yako hapa.

#MICHEZO>>>Bolt na Farah wafurai Medali.Fahamu zaidi hapa.

 Wanariadha Mo Farah wa Uingereza na Usain Bolt wa Jamaica wameendelea kuitikisa dunia kwenye mchezo huo, baada ya kutwaa medali nyingine za dhahabu.
Wakati Farah, mzaliwa wa Somalia aliyekimbilia Uingereza kukwepa machafuko akizoa medali ya dhahabu kw akukimbia umbali wa mita 5,000 kwa Dakika 13:50.38, Bolt alipata dhahabu ya 11 baada ya kushinda kwenye mbio za kupokezana vijiti kwa watu wanne umbali wa mita 100.
Huu ni ushindi wa tatu mfululizo kwa Farah aliyepata pia kutwaa dhahabu kwenye mashindano ya dunia lakini pia kabla kwenye michuano ya Olimpiki. Haikuwa ushindi rahisi kwa Farah, wala hakuongoza muda wote wa mchezo, kwani mshindi wa Kenya kwenye michuano ya Jumuiya ya Madola, Caleb Ndiku aliongoza kwa kipindi fulani.

Hata hivyo, Farah aliongeza kasi na kumpita Ndiku kwenye kona ya mwisho na kujihakikishia medali ya saba ya dhahabu ya dunia. Alieleza furaha yake kwa kutwaa ubingwa lakini zaidi kuweka historia duniani.
Alidokeza kwamba hakuwa anajihisi timamu sana kiafya, kwani misuli ya paja ilionekana kutaka kumharibia mambo lakini jopo la madaktari wake wakamsaidia. Akasema kwamba awali alihisi woga lakini hatimaye mambo yakaenda vyema.
Kwa upande wa Bolt, alifanya vyema na wenzake watatu walipopokezana vijiti na kumaliza mita 100 kwa sekunde 37.36, na kwa Bolt ilikuwa ukamilisho wa dhahabu tatu katika mashindano haya, kwani alitwaa ya kwanza kwenye mbio za mita 100 na kisha mita 200.
Toa maoni yako hapa.

#YALIYOJIRI>>>MGOMBEA MWENZA WA CCM SAMIAH SULUHU ANADI ILANI YA CCM MWAKA 2015 KATIKA KATA YA KYENGEGE,WILAYA YA IRAMBA.

 Bi.Samiah Suluhu ambaye ni Mgombea Mwenza wa nafasi ya Urais kwa tiketi ya chama cha mapinduzi akizungumza na Wananchi wa kata ya kyengege mambo mbalimbali anayodhamiria kuwafanyia mara baada ya kushinda hapo October 25.Kubwa amewaahidi kutatua kero ya Maji kwa Tanzania nzima ,Kujenga mabweni kwaajili ya watoto mashuleni,Kuinua Uchumi wa akina mama kupitia Mikopo mbalimbali na kupitia Utekelezaji wa Ilani ya CCM inayosema kila kijiji kimetengewa Milion 50 kwaajili ya maendeleo.
 Mgombea Mwenza wa nafasi ya Urais kwa Chama cha Mapinduzi Bi.Samia Suluh akisalimiana na Mh;Mwigulu Nchemba ambaye ni mgombea Ubunge jimbo la Iramba hii leo,Bi.Samiah suluhu katika ziara yake ya kampeni ndani ya mkoa wa Singida,hii leo amefika Kata ya Kyengege Jimbo la Iramba kwaajili ya kunadi Ilani ya CCM ya uchaguzi ya Mwaka 2015 na kuomba kura za kishindo kwa nafasi zote za Udiwani,Ubunge na Urais ifikapo Tar.25.10.2015
 Kushoto ni Mgombea Ubunge jimbo la Mkalama kupitia CCM ambaye pia alihudhuria mkutano wa Kata ya Kyenge wilaya ya Iramba.
 Mgombea mwenza wa nafasi ya Urais Bi.Samiah Suluhu akimuombea Kura Mh;Mwigulu Nchemba kwa wananchi wa kata ya kyengege hii leo wakati wa mkutano wa kampeni za kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015.
 .Makamu wa Rais mtarajiwa wa Kwanza Mwanamke Nchi Tanzania akimnadi Mgombea Udiwani wa kata ya Kyengege wilaya ya Iramba.
Hapa akiwanadi washindi wa Ubunge Viti Maalum Mkowa wa Singida,Kushoto ni Ashyrose na Kulia ni Bi.Martha Mlata.  Picha na Sanga Festo Jr.

#MICHEZO>>>Amina Karuma achaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake nchini.

Uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake nchini (TWFA)  umemalizika ambapo Amina Karuma amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho, kufuatia uchaguzi uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
 Nafasi ya katibu msaidizi imekwenda kwa mwandishi wa habari za michezo Someo Ng’itu, na nafasi ya wajumbe wa kamati ya utendaji ya TFWA imekwenda kwa Debora Mkemwa na Theresia Mng’ongo.
Mgeni rasmi katika uchaguzo huo alikuwa ni katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine ambapo na uchaguzi ulisimamiwa na Kamati ya Uchaguzi ya TWFA chini ya uangalizi wa Jeremia Wambura kutoka kamati ya Uchaguzi ya TFF.
TFF inawapongeza viongozi wapya waliochaguliwa na kuwatakia kila la kheri katika majukumu hayo mapya, na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika maendeleo ya mpira wa miguu ya wanawake nchini.
Toa maoni yako hapa.   

#YALIYOJIRI>>>ACT yafungua kampeni Zakheem Jijini Dar-es-salaam hii leo.Fahamu zaidi hapa.



 Mshauri wa chama cha ACT-Wazalendo, Prof. Kitila Mkumbo akihutubia kwenye uzinduzi huo.

 Viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiimba wimbo wa taifa.
 Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto, akiwatambulisha wagombea ubunge wa majimbo yote ya Dar es Salaam
 Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto, akigawa ilani ya chama hicho kwa mgombea urais na mwenza wake.
Mgombea Mwenza, Hamad Mussa Yusuph akihutubia kwenye uzinduzi huo.
 Mwana muziki Bwana misosi, akitoa burudani katika uzinduzi wa kampeni wa Chama cha ACT-Wazalendo uliofanyika viwanja vya Zakhem Mbagala Dar es Salaam leo
 Umati wa Wananchi ukiwa katika uzinduzi wa kampeni wa chama cha ACT-Wazalendo uliofanyika viwanja vya Zakhem Magala Dar es Salaam leo.

#YALIYOJIRI>>>TICTS yaipongeza TPA kwa mageuzi yanayofanyika bandari.Fahamu zaidi hapa.

 Meli kubwa kabisa kuwahi kuingia katika bandari ya Dar es Salaam, Clemens Schulte. Meli hiyo yenye urefu wa mita 255 ilitia nanga nchini 26 Agosti 2015 na kufunga gati katika kitengo cha Kontena kinachoendeshwa na Kampuni binafsi ya TICTS katika bandari ya Dar es salaam siku iliyofuata.
 Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bi. Apolonia Mosha (katikati) akiwa na nahodha Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Capt. Abdul Mwingamno (kulia) na Kaimu Meneja Mawasiliano wa mamlaka hiyo, Bi. Janeth Ruzangi wakati wa tukio la kukaribisha kuwasili kwa meli kubwa kuwahi kufika katika bandari ya Dar es Salaam. Meli hiyo, MV. Clemens Schulte, yenye urefu wa mita 255 ilitia nanga nchini 26 Agosti 2015 na kufunga gati katika kitengo cha Kontena kinachoendeshwa na Kampuni binafsi ya TICTS katika bandari ya Dar es salaam siku iliyofuata.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kimataifa cha Makasha (TICTS), Bw. Paul Wallace (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Maendeleo wa kampuni hiyo, Bw. Donald Talawa (kushoto) wakimsikiliza nahodha Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Capt. Abdul Mwingamno (kulia) wakati wa tukio la kukaribisha kuwasili kwa meli kubwa kuwahi kufika katika bandari ya Dar es Salaam. Meli hiyo, MV. Clemens Schulte, yenye urefu wa mita 255 ilitia nanga nchini 26 Agosti 2015 na kufunga gati katika kitengo cha Kontena kinachoendeshwa na Kampuni binafsi ya TICTS katika bandari ya Dar es salaam siku iliyofuata

Uongozi wa kitengo cha kimataifa cha makasha (TICTS) umepongeza juhudi zinazoendelezwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) za kuimarisha bandari ya Dar es Salaam. Akiongea wakati wa kukaribisha kuwasili kwa meli kubwa kabisa kuwahi kufika katika bandari hiyo, Afisa Mkuu Mtendaji (CEO) wa TICTS, Bw. Bw. Paul Wallace aliuita ujio huo kuwa wa muhimu sana kwa maendeleo ya bandari hapa nchini. “Tunaona maendeleo makubwa ya kiutendaji katika bandari yanayopelekea mashirika makubwa kama Maersk Line kuleta meli zake katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki,” alisema mwishoni mwa wiki. Alisema ujio wa meli hiyo pia ni uthibitisho wa ushirikiano wa wadau mbalimbali katika kuhakikisha kuwa bandari ya Dar es Salaam inafunguka zaidi kimataifa. Meli hiyo yenye urefu wa mita 255 ilitia nanga nchini 26 Agosti 2015 na kufunga gati katika kitengo cha Kontena kinachoendeshwa na Kampuni binafsi ya TICTS katika bandari ya Dar es salaam siku iliyofuata. Meli hiyo iliyoongozwa na nahodha Vladislav Barisovscy inajulikana kama Clemens Schulte ina uwezo wa kubeba makontena 5466. Wakati wa safari hiyo ya kwanza, MV. Clemens Schulte yenye ukubwa wa Postmanax ilishusha makontena 250 na kupakia mengine 1300. Bandari ya Dar es Salaam iko katika mageuzi makubwa kuifanya ya kisasa zaidi ambapo moja ya maboresho yaliyofanyika hvi karibuni ni pamoja na kuanzisha mfumo wa malipo ya huduma za bandari kwa njia ya kielektroniki na kufunga mifumo mipya ya kisasa ya ulinzi ikiwa ni pamoja na CCTV. “Tunajivunia bandari yetu, tumeongeza ufanisi na tuko tayari kupanua zaidi huduma zetu,” alisema. Bw. Wallace alisema TICTS iko katika harakati za kununua mashine kubwa zaidi za kubebea mizigo zenye thamani ya Tshs bilioni 46 zitakazowezesha kampuni hiyo kuhudumia meli kubwa zaidi ya Clemens Schutle na hivyo kuifanya bandari ya Dar kuwa shindani katika ulimwengu unaobadilika kwa kasi. Kaimu Meneja Mawasiliano wa TPA, Bi. Janeth Ruzangi alisema ujio wa meli hiyo toka bandari ya Laem Chabang ya nchini Thailand ni uthibitisho wa kuzidi kuaminika kwa bandari hiyo kimataifa. “Uaminifu huu unatokana na kuimarika kwa huduma tunazotoa,” alisema. Mkurugenzi wa Maendeleo TICTS, Bw. Donald Talawa alisema ujio wa meli hiyo ni kielelezo cha ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi ambao unatakiwa kuigwa na wadau wengine nchini. Mara ya mwisho Kitengo hicho kupokea meli kubwa ilikuwa mwezi Februari 2014 ambapo meli iliyoitwa Msc Martina iliyokuwa na urefu wa mita 242. Pamoja na kuhudumia wateja wa ndani bandari ya Dar es Salaam pia inahudumia nchi za DRC Congo, Zambia, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi na Zimbabwe.

Tukumbushane watu wangu Sheria ya Mitandaoni.Sheria ipo hapa.

Sheria ya mitandao inaanza kutumika rasmi tarehe 1 September 2015, haya ni baadhi ya mambo ya kuzingatia ili kuepukana na mkono wa dola: 1. Tujiepushe kusambaza ujumbe wa uchochezi ama ushawishi wa kisiasa unaoweza kuleta athari kwa jamii kupitia mitandao; 2. Tujiepushe kusambaza au kutunga ujumbe unaoleta uchochezi wa kidini unaoweza kupelekea kuvuruga Amani na maelewano kwa jamii kupitia mitandao; 3. Tujiepushe kusambaza picha ama video za utupu ama zilizokosa maadili kwa jamii kupitia mitandao; 4. Tujiepushe kusambaza picha ama video za uchochezi wa kidini ama kisiasa kupitia makundi mbalimbali ama mitandao ya kijamii; 5. Tujiepushe kusambaza kwa wengine ujumbe wowote unaohusiana na mambo yaliyotajwa 1 – 4; 6. Tujiepusha na kufanya wizi kupitia mitandao mbalimbali ya simu; 7. Tujiepushe kumpatia mtu yeyote line zetu za simu ili zitumike kufanya wizi au utapeli wa mitandao ya simu; 8. Tujiepushe kushiriki kumchafua mtu, taasisi, kikundi cha watu kwa namna yoyote kupitia mitandao; 9. Tujiepushe na tabia ya kutokutoa taarifa polisi juu ya upotevu wa simu au kifaa chochote cha kielektroniki kinachoweza kutumika kwa mawasiliano ya kimtandao; 10. Tujiepushe kutumia mtandao kwa utapeli kupitia “brand” ama jina la mtu; 11. Tujiepushe na “ujamaa” wa kushirikiana vifaa vya kielektronic na mtu yeyote yule hata kama unamuamini sana; 12. Tujiepushe na kumtajia mtu password zetu au email account zetu kwa namna yoyote ile (kila mtu au mwanafunzi aliyeko field atumie username na password yake akitaka kutumia computer za company); 13. Tuhakikishe kwamba website yoyote inayotuhitaji kutumia username na password zetu ipo secured. Website zote zilizo secured address (url) huanzia na https://; 14. Tukumbuke kutoa elimu hii kwa watoto, ndugu, marafiki na majirani zetu.
Toa maoni yako hapa.