Saturday, 29 April 2017

Download wimbo mpya wa Joh Makini - Young Killer unaoitwa "Diss".

https://my.notjustok.com/track/download/id/211419




Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

VIDEO:GOLI LA SIMBA ILIVYOIFUNGA AZAM (SIMBA 1-0 AZAM) UWANJA WA TAIFA.




Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

PICHA: Rais Magufuli Awasili Mkoani Kilimanjaro kwa Ziara ya siku Tatu ....Pia Atakuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho ya May Mosi.

Rais John Pombe Magufuli leo Aprili 29, 2017 amewasili mkoani Kilimanjaro ambapo atafanya ziara ya kikazi kwa muda wa siku tatu.

Sambamba na ziara hiyo, Rais Magufuli anatarajiwa kuhudhuria sherehe za Sikukuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi) ambapo atakuwa mgeni rasmi.
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

Kampuni ya Bia (TBL) yawafuta kazi wafanyakazi 100 ndani ya saa 24.

Kampuni  ya Bia ya Tanzania Breweries (TBL), imepunguza watumishi wake takribani 100 ndani ya saa 24.

Kwa mujibu wa taatifa toka kwa  watumishi wa TBL,  watumishi waliopunguzwa ni wale wa kitengo cha masoko.

Mtoa taarifa mmoja kutoka kwenye duru za uongozi wa TBL ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema kuwa uamuzi huo ulitekelezwa Jumatatu ya wiki hii.

Alisema sababu kuu ya kupunguza wafanyakazi hao ni kulinda uchumi wa kampuni baada ya mauzo ya bidhaa kuporomoka kwa kasi katika kipindi cha mwaka jana hadi mwaka huu.

Ofisa masoko mmoja wa kampuni hiyo ambaye hajakumbwa na panga la kupunguzwa kazi, alidokeza kwamba uamuzi huo unatokana na hali ya mauzo na uchumi wa kampuni kutokuwa rafiki.

Aliongeza kuwa uamuzi wa Serikali wa kuzuia biashara ya pombe kali zinazofungashwa kwenye mifuko ya plastiki(viroba) umeathiri kwa kiasi kikubwa soko la bidhaa yao aina ya Konyagi.

“ Wameachishwa kinyama sana, waliitwa siku ya Jumatatu na kuachishwa papo hapo(on spot), wakaambiwa wayaache magari yao na kusaini fomu ya kuondoka, miye kwa bahati nzuri  nimepona. Na hili jambo la viroba ndio limepigilia msumali wa mwisho,” alisema ofisa huyo.

Msemaji wa Kampuni ya TBL, Georgia Mutagahwa alipotafutwa kwa ajili ya uthibitisho wa taarifa hiyo, hakupokea simu kila ilipopigiwa.
Credit: Mtanzania
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

“Zitto hafai kuiongoza TFF, ni mbinafsi” – Jerry Muro.

Siku za hivi karibuni kumeibuka stori ambayo imekuwa ikimake headlines kwenye mitandao mbalimbali hasa katika medani ya soka la Tanzania ikimuhusu Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kutaka kugombea Urais wa TFF.

Habari hiyo imekuwa ikiwagusa watu wengi ambapo miongoni mwao ni aliyekuwa Afisa Habari wa Yanga Jerry Muro ambaye alipoulizwa kuhusu maoni yake juu ya hilo alisema Mbunge huyo hafai.

Akijibu swali la mtangazaji wa Clouds 360 ya Clouds TV, April 29, 2017 Jerry Muro ametoa mtazamo wake huo baada ya kuulizwa kama Zitto Kabwe atafaa kugombea Urais wa TFF akisema Zitto Kabwe hafai kuiongoza TFF kwa sababu ni mbinafsi ambaye alishindwa kukaa na wenzie akaenda kuanzisha chama chake binafsi.

“Hapana! Hawezi kuiongoza. Zitto ni mwanasiasa ambaye anatazama maslahi yake, hatazami maslahi ya watu wengine. Hafai kuiongoza TFF kwa sababu ni mbinafsi, ni mmimi. Kama mtu ameshindwa kukaa na wenzie akaamua kwenda kuanzia chama chake akiongoze mwenyewe ni mbinafsi.” – Jerry Muro.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

Simba Yaingia Fainali, Yaiadhibu Azam 1 - 0 Kombe la Shirikisho.

SIMBA SC imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), linalojulikana kama Azam Sports federation Cup baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Sifa zimuendee mfungaji wa bao hilo pekee dakika ya 48, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim ambaye hata hivyo hakumaliza mchezo baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu baadaye.

Kwa ushindi huo, Simba itasubiri kukutana na mshindi kati ya wenyeji Mbao FC na Yanga SC zinazomenyaa kesho Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Mathew Akrama wa Mwanza, Azam FC ilipata pigo dakika ya 15 baada ya kiungo wake mchezeshaji, Salum Abunakar ‘Sure Boy’ kutolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumchezea rafu mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Hajib.

Ilionekana kama wachezaji hao wamegongana kwa kawaida mno, lakini kwa namna Hajib alivyojirusha huku akipiga yowe la kuugulia maumivu Akrama aliingia kwenye mtego wa kumtoa kwa kadi nyekundu Sure Boy.

Tukio hilo lilileta kizaazaa kidogo uwanjani baada ya wachezaji wa Azam kumfuata refa na kuanza kumlalamikia kwa maamuzi yake. Walinzi wa Uwanja wa Taifa walimfuata Sure Boy na kujaribu kumtoa kwa nguvu, jambo ambalo liliwafanya wavutane na Meneja wa Azam, Philipo Alando.

Mchezo uliendelea baada ya tukio hilo, huku timu zikiendelea kushambuliana kwa zamu na kabla ya Akrama kupuliza kipyenga cha kumaliza ngwe ya kwanza kukiwa hakuna bao.

Kipindi cha pili, Simba walikianza vizuri na kufanikiwa kupata bao baada ya dakika tatu tu, kiungo Mohammed ‘Mo’ Ibrahim akimtungua vizuri kipa Aishi Salum Manula kwa shuti la mguu wa kulia kufuatia ya krosi ya mshambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo.

Simba wakaanza kucheza kwa tahadhari kwa kujihami zaidi baada ya bao hilo, huku Azam FC wakionekana kusaka bao la kusawazisha kwa nguvu zao zote.

Mo Ibrahim akaonyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 77 baada ya kumchezea rafu beki wa Azam FC, Shomary Kapombe.

Beki Mkongo, Janvier Besala Bokungu akaizuia Azam FC kusawazisha baada ya kuokoa mpira uliopigwa kwa kichwa na Nahodha wa timu hiyo, John Raphael Bocco uliokuwa unaelekea nyavuni dakika ya 84.

Kikosi cha Simba kilikuwa; Daniel Agyei, Janvier Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murshid, James Kotei/Said Ndemla dk88, Jonas Mkude, Shizza Kichuya, Muzamil Yassin, Laudit Mavugo/Mwinyi Kazimoto dk86, Ibrahim Hajib na Mohammed Ibrahim.

Azam FC; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Gardiel Michael, Aggrey Morris, Daniel Amoah, Himid Mao, Stephan Kingue/Joseph Mahundi dk58, Shaaban Iddi/Frank Domayo dk46, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na Ramadhani Singano ‘Messi’/Mudathir Yahya dk82.
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

Friday, 28 April 2017

YANGA WAKESHA CCM KIRUMBA WAKIWALINDA MBAO WASIFANYE YAO USIKU.

Na Fahad Ally, Mwanza
Kama wewe unaichukulia poa mechi ya Mbao FC dhidi ya Yanga hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho, basi unajidanganya.


Mechi hiyo inapigwa keshokutwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa na mashabiki wa Yanga maarufu kama “Makomandoo” wameamua kuulinda uwanja huo.
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

JOSHUA, KLITSCHKO WAPIMA UZITO, KILA MMOJA ATAMBA KUMMALIZA MWENZAKE LEO.

Anthony Joshua na Wladimir Klitschko, kila mmoja anaamini ni mbabe na atashinda katika pambano la leo.

Rasmi wababe hao wamepima uzito jana la Joshua na 

Klitschko kutoka Ukraine, kila mmoja anataka kumaliza ubishi leo katika pambalo hilo la uzito wa juu jijini London.


TAKWIMU ZA JOSHUA
Age: 27
Fights: 18
Wins: 18
Draws:  0
Losses: 0
KO percentage: 100 
Height/Reach: 6ft 6ins/82ins


TAKWIMU ZA KLITSCHKO
Age: 41 
Fights: 68
Wins: 64
Draws:  0
Losses: 4
KO percentage: 82
Height/Reach: 6ft 6ins/81ins
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo mpya wa Ray C unaoitwa "Unanimaliza".

https://my.notjustok.com/track/download/id/210994


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo mpya wa Z anto & Momba unaoitwa "Nilie Nawe".

https://my.notjustok.com/track/download/id/210993


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

Makubwa!!! Ndoa ya Nuh Mziwanda Kufungwa Upya.

Ni siku moja tu imepita tangu staa wa Bongo Fleva Nuh Mziwanda kupitia account ya Instagram kupost picha ya mtoto wake aliyebarikiwa katika ndoa yake, inadaiwa ndoa hiyo kuingia katika mvutano.

Inasemekana kuwa ndugu wa Nuh Mziwanda hawakuridhia ndoa ya ndugu yao iliyofungwa miezi kadhaa iliyopita kwa kuwa Nuh alibadili dini kufuata dini ya mke wake ambapo kupitia U-heard  ya XXL ya Clouds FM April 28 2017 mtangazaji Soudy Brown ameinasa sauti ya mke wa Nuh Mziwanda akimzungumza mama mkwe wake:

“Nilimwambia mama unachelewa, mwambie aniache. Na anajua kuwa mimi sijaolewa na mwanawe, ila anajua nimezaa tu na mwanawe. Kwenye sherehe ya harusi hakuwepo, alikuwa kwenye msiba. Yule mama ni mzee wa Kanisa, alikuwa anataka niende kanisani nibadili dini ndio niolewe.” – Mama ANYA
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

Aina 12 Ya Wanawake Ambao Watayafanya Maisha Yako Kuwa Magumu Sana.

 tumekuja na orodha ya wanawake ambao kama mwanamume unafaa kuwa chonjo nao kwani watayafanya maisha yako ya mahusiano kuwa ya balaa.

Labda sahizi uko katika mahusiano ya muda mrefu na mpenzi wako ama sahizi uko mbioni unatafuta, kuwa macho na aina hii ya wanawake ambao wanaweza kukuharibia ama kukuletea shida
katika mahusiano yako nao mbeleni.
 1. Mwanamke anayekuganda nguoni
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye amekupenda kisai cha kuwa hawezi kufanya jambo lolote bila kukuhusisha wewe.

Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye amekuwa amezama na penzi lako kiasi cha kuwa hakupi nafasi ya kupumua. Kila kitu atakachofanya lazima uwe karibu nayeye. Well, hii ni poa kwa mahusiano lakini itafikia mahali fulani ambapo utachoshwa na tabia zake haraka.

Na pia yeye kama mwanamke atakuwa na mawazo finyu kwani kila wakati anapokumbwa na jambo fulani hawezi kulitatua bila kukuhusisha.
 2. Mwanamke aliyepagawa kimapenzi
Nani hapendi mwanamke anayempenda kupindukia? Kila mtu angekuwa na mwanamke aina hii wanaume wangekuwa na furaha milele.

Lakini kulingana na utafiti ni kuwa aina hii ya mwanamke ni miongoni mwa wanawake wabaya kabisa ambao wanaweza kufanya maisha yako kuwa ya taabu.

Mwanamke kama huyu ungempenda siku za kwanza kwanza lakini tatizo ni kuwa kadri siku zinavyopita mnapokuwa pamoja utagundua tatizo flani, mwanamke aina hii hangependa ufanye chochote bila yeye kuwa karibu yako.

Hii inamaana kila mahali unapoenda lazima akuandame. Aidha ukiwa na marafiki zako, vilabuni, wanjani…nk, yaani kiufupi kila uendapo anataka awe hapo hapo ili akuangalie na akupende zaidi. Utamweza kweli huyu?
 3. Mtumiaji
Kuna aina ya wanawake ambao wanakuona wewe kama mwanamume mzuri ili wakutumie kama chambo kuwafanikisha kimaisha.

Unaweza kuwa mwanamume ambaye unauunganishi na watu wengi, ama unaweza kuwa mwanamume ambaye unapendwa na wengi.

Mwanamke aina hii ataona kuwa akiwa karibu na wewe itakuwa nafasi rahisi kwake kupata connection na marafiki zako kwa

urahisi. Hii inamaana kuwa pindi mwanamke aina hii akifanikiwa kupata kile ambacho amekuwa akitafuta, bila kupoteza wakati atakutema na kukuacha kwenye giza.
 4. Mwanamke asieomba msamaha
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye hawezi kuomba msahama kwa jambo lolote ambalo amefanya hata kama ni la makosa kiasi gani.

Anaweza kuomba msahamaha kwa shingo upande ama aamue kunyamaza kimya tu kwa jambo alilofanya la kukwaza ama kuudhi.

Owk kwanza ni kuwa aina hii ya mwanamke anaogofya sana kwani mtu ambaye hakubali makosa yake si mtu mzuri wa kuishi naye hata mara moja.
 5. Mlalamishi
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye nyakati zote yeye hulalamikia kuhusu hili na lile. Yaani kwake hakuna jambo zuri ambalo limeshawahi kumfanyikia.

Aidha atakuwa akilalamika kuhusu marafiki zake, maisha yake ya kila siku nk. Yaani yeye siku zote hana amani. Aina hii ya mwanamke haifai kabisa kwani ulalamishi wake wa kila siku utakuchosha kwa haraka.
 6. Asiyejielewa
Huyu ni mwanamke ambaye haelewi anachotaka maishani. Wakati wote yeye atakuwa anahangaika na uchaguzi wake na hajiamini na chochote ambacho anachagua.

Aina hii ya mwanamke achana nayo kwa sababu wewe pia inamaanisha hayuko asilimia mia moja kama aendelee kuwa nawe au la.

Aina hii ya mwanamke mara nyingi huwa na wanaume wengi na nirahisi kwake kukuendea kinyume kimapenzi. So kama wewe unamahusiano na mwanamke aina hii aidha uachane naye fasta ama akuwache wewe wa kwanza.
 7. Anayetawala na kutotosheka
Hii ni aina ya mwanamke ambaye anatarajia makuu kila wakati na hatosheki kile alicho nacho. Anapenda kutawala na kila kitu anataka kifanywe vile ambavyo anavyotaka yeye.

Owk najua wanawake wanapenda wanaume ambao ni gentlemen, lakini baada ya muda mfupi utakuja kugundua kwamba aina hii ya mwanamke watakufanya bwegu muda unaposongea, yaani watakukalia kichwani na wao kujifanya mabosi.
 8.Mwenye maoni ya ukashifu wakati wote
Kuwa na maoni na kukashifu si jambo baya kwani kukosoa mambo katika mahusiano ni jambo zuri katika maisha. Lakini usizidishe.

Aina hii ya wanawake wanaokashifu kupitia kiasi ni wale ambao wakisema jambo fulani basi litabakia hilo hilo na hata ufanyeje hawawezi kujeuza. Aina hii ya wanawake watafanya maisha yako kuwa balaa kwani wakisema jambo flani, bila hata kufikiria wenzao.
 9. Nusa Nusa
Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye haipiti siku bila kukuchunguza. Kila wakati anapopata mwanya anajaribu kukuchunguza mindoko yako.

Unaweza kuwa mwaminifu kwake lakini yeye bila kutosheka lazima akuchunguze chunguze, mara aangalie simu yako, atake kujua umetoka wapi umeenda wapi, jana ulivaa nguo gani, anawauliza maswali marafiki zako kukuhusu nk. Owk aina hii ya mwanamke muogope sana kwani pia yeye haaminiki.

Kila anachofanya yeye anashuku pia wewe utafanya. Hivyo mara nyingi ukiona mwanamke anashindwa kukuamini kwa uhusiano, inamaanisha kuwa pia yeye ana hilo tatizo, so ukiona mwanamke wako ana hizo tabia achana nayeye mara moja.
 10. Asi na maono
Aina hii ya mwanamke inafanana karibu na ile ya asiyejielewa lakini hii ni kuwa mwanamke aina hii hana maoni kujihusu yeye mwenyewe.

Ukimmuliza kitu chochote anakwambia kuwa hajui ama hana mtazamo wowote kuhusu jambo lolote. Mwanamke huyu anaweza kuonekana mwanamke mzuri mara ya kwanza kwa sababu hawezi kukupinga na chochote unachosema lakini pindi muda unaposongea utaona kuwa ataanza kuwa mzigo kwako.

Aina hii ya mwanake iogope sana kwa sababu anaweza kuwa anafanya hivyo maksudi huku akiwe ameweka mtego ama anamalengo yake kibinafsi kutoka kwako. Mwanamke asiyetoa maoni kuhusu chochote unachosema ni umuogope
sana.
 11. Mcheza ndondi
Hii ni aina ya mwanamke amabye anakasirika kwa haraka na akichukizwa na chochote kile ambacho kinakuja kwa akili yake ni vita. Aina hii ya mwanamke sitaigusia sababu kila mtu anajua matokeo yake.
12. Mtoto wa mama
Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye hatofanya chochote bila kuingiza wazazi wake katika maongezi yake.
Aina hii ya mwanamke ni mbaya kwa sababu mwanamke aina hii hata ufanye nini lazima aingize wazazi wake ndani yake. Hii inamaanisha kuwa hawezi kudhamini maoni yako kabla kuwauliza wazazi wake.

Hii ni baadhi ya tabia za wanawake ambazo mwanamume yeyote anafaa kuwa chonjo kwani mwishoni wanaweza kuleta taabu ambazo zitakuwa vigumu kutatu  
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

UNATATIZO la Nguvu za Kiume..Soma Hapa Ujue Jinsi Gani Mbegu za Tikiti Maji Zinavyoweza Kukusaidia.

Tikiti ni moja ya matunda ambayo hupendwa na watu wengi na yamekuwa na faida zake kiafya, lakini leo naomba tuzifahamu hizi faida za mbegu zake za tunda hilo.

1. Husaidia kulinda afya ya moyo.
Hii ni kutokana na kuwa na madini ya kutosha ya magnesium ndani ya mbegu hizo.

2. Husaidia kwa wenye chunusi
Unapotumia mafuta ya mbegu za tikiti huweza kuwasaidia wale wenye tatizo la chunusi. Ambapo mafuta hayo utapaswa kuyapaka kwa kutumia pamba kwenye sehemu zilizoathirika.

3. Husaidia kuimarisha kinga za mwili
Kutokana na kuwa na madini ya magnesium ya kutosha hiyo husaidia kuimarisha kinga zako za mwili na kufanya kutokumbwa na maradhi mara kwa mara.

4. Huboresha mfumo wa uzazi kwa wanaume
Wanaume wanaotumia mbegu hizi huwa katika hali nzuri kwenye tendo la ndoa na uzalishaji kwa ujumla.

5. Husaidia kuzuia tatizo la nywele kukatika
Mbegu hizi zina utajiri wa fatty acid ambayo husaidia kuboresha afya ya nywele


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

#MICHEZO>>>Kesho club ya Mbeya City itaingia mkataba na kampuni ya vifaa vya michezo ya Sports Master wa kutengenezewa vifaa.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

PICHA:Muonekano mpya wa msanii Diamond platnumz baada ya kunyoa rasta alizokuwa nazo.

Diamond Platnumz ni miongoni mwa mastaa wa Bongo Flava wanaopenda fashion. Muimbaji huyo ameamua kubadilisha muonekano wa nywele zake kwa kuirudia style ya zamani ambayo mashabiki walikuwa wameizoea.
Hitmaker huyo wa ‘Marry You’, wikiendi hii atatumbuiza katika show yake nchini Zimbabwe. Tazama picha zaidi hapa chini.
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

VIDEO:Yusuph Mlela Amtumbua Live Nay Wa Mitego, Aanika Siri Nzito.

Hali inazidi kuwa mbaya katika beef inayoendelea kati ya mastaa wawili hapa Bongo, muigizaji mkali Yusuph Mlela na rapper mkali Nay wa Mitego ambapo Global TV imefanikiwa kukuletea Exclusive interview inayozungumzia sakata zima lilivyoanza na linavyoendelea.



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

Taarifa kwa madaktari waliokidhi vigezo kwenda kufanya kazi Kenya.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,jinsia na Watoto,Idara kuu ya Aya, inawatangazia madaktari walioomba kufanya kazi nchini Kenya na sasa kuajiriwa hapa nchini Tanzania, kutakiwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi siku ya 14 ya tangazo hili kutoka.
Soma taarifa kamili:


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

HAYA YALIKUWA MAUAJI YA KUTISHA MKOANI MWANZA, BABA, MAMA NA MTOTO WAUAWAWA KINYAMA BILA HURUMA.

Katika eneo la tukio la mauaji hayo mlango wa nyumba ulikuwa umefungwa kwa nje, na mara baada ya kufunguliwa maiti ya baba wa familia hiyo Jonus Elias (44) ilikuwa sebuleni huku ikiwa imechinjwa, nako chumbani kulikuwa na mwili wa mama wa familia hiyo Bi. Lucia Jonus na mwili wa mtoto aliyekuwa na umri wa miezi saba.
Polisi wakiondoa mwili wa marehemu Jones Lulinga, kutoka nyumbani kwake kuupoeleka Hospitali baada ya kuuwa kwa kukatwakatwa na mapanga na watu wasiojukikana katika kijiji Ihila, Kata ya Buhingwa mkoa Mwanza jana.
Polisi akiwa ameubeba mwili wa mtoto aliyeuawa.
Polisi wakishirikiana kupakia miili ya marehemu hao kwaajili ya kwenda kufanyiwa uchunguzi zaidi.
Watu watatu wa familia moja wameuawa kikatili usiku wa kuamkia jana na watu wanaosadikika kuwa ni majambazi katika kijiji cha Ihila B, Kata ya Buhongwa Wilaya ya Nyamagana hapa Mkoani Mwanza.

Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinaeleza kwamba watu hao ambao ni Jonus Elius (44) ambae ni baba wa familia, Lucia Jonus (35) ambae ni mama wa familia pamoja na Eliud Jonus (1) ambae ni mtoto wa familia hiyo wameuawa kikatili kufuatia baba wa familia hiyo kuchinjwa shingoni na kitu kinachosadikiwa kuwa na ncha kali huku mama na mtoto wakisadikiwa kunyongwa na kitu kinachosadikiwa kuwa ni waya.

Uchunguzi wa awali unaeleza kwamba kulikuwa na mgeni ambae alifika katika familia hiyo ndani ya siku nne kwa ajili ya shughuli ya kufyatua tofali za ujezi wa nyumba ya familia hiyo, ambae anasadikiwa kutenda tukio hilo kwa kuwa baada ya mauaji hayo ametoweka katika familia hiyo.

Akiwa katika eneo la tukio Mkuu wa makosa ya upepelezi Mkoa wa Mwanza RCO Joseph Konyo ameeleza kwamba mauaji hayo yanasadikika kutekelezwa kati ya majira ya saa nane hadi saa kumi usiku wa kuamkia leo.

Aidha RCO Konyo amesema kwamba bado uchunguzi zaidi juu ya mauaji hayo unaendelea na taarifa zaidi zitatolewa na msemaji wa jeshi la polisi Mkoa wa wa Mwanza ambae ni RPC pindi upelelezi

utakapokamilika ambapo amewataka wananchi kutoa ushirikiano wao ili kuweza kufanikisha upelelezi huo mapema.

Kufuatia mauaji hayo ya kusikitisha ambayo yanasadikika kutekelezwa huku sababu zikiwa bado ni kitendawili, wananchi na majirani wa eneo hilo la tukio wameeleza kusikitishwa kwao na matukio ya aina hiyo ambayo wametoa rai kwa jeshi la polisi kuhakikisha likamilisha upelelezi wake mapema na kuhakikisha kwamba wahusika wote wanafikishwa katika vyombo vya dola.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa