Kampuni ya Bia ya Tanzania Breweries (TBL), imepunguza watumishi wake takribani 100 ndani ya saa 24.
Kwa mujibu wa taatifa toka kwa watumishi wa TBL, watumishi waliopunguzwa ni wale wa kitengo cha masoko.
Mtoa
taarifa mmoja kutoka kwenye duru za uongozi wa TBL ambaye hakutaka jina
lake litajwe, alisema kuwa uamuzi huo ulitekelezwa Jumatatu ya wiki
hii.
Alisema
sababu kuu ya kupunguza wafanyakazi hao ni kulinda uchumi wa kampuni
baada ya mauzo ya bidhaa kuporomoka kwa kasi katika kipindi cha mwaka
jana hadi mwaka huu.
Ofisa
masoko mmoja wa kampuni hiyo ambaye hajakumbwa na panga la kupunguzwa
kazi, alidokeza kwamba uamuzi huo unatokana na hali ya mauzo na uchumi
wa kampuni kutokuwa rafiki.
Aliongeza
kuwa uamuzi wa Serikali wa kuzuia biashara ya pombe kali
zinazofungashwa kwenye mifuko ya plastiki(viroba) umeathiri kwa kiasi
kikubwa soko la bidhaa yao aina ya Konyagi.
“
Wameachishwa kinyama sana, waliitwa siku ya Jumatatu na kuachishwa papo
hapo(on spot), wakaambiwa wayaache magari yao na kusaini fomu ya
kuondoka, miye kwa bahati nzuri nimepona. Na hili jambo la viroba ndio
limepigilia msumali wa mwisho,” alisema ofisa huyo.
Msemaji
wa Kampuni ya TBL, Georgia Mutagahwa alipotafutwa kwa ajili ya
uthibitisho wa taarifa hiyo, hakupokea simu kila ilipopigiwa.
Credit: Mtanzania
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza HapaFollow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment