Sunday 30 April 2017

RAY C -Hapa Kazi Tu, Mapenzi Baadaye.

Msanii mkongwe wa muziki, Ray C, amedai kwa sasa anapambana kuhakikisha anafanya vizuri katika muziki wake.
Muimbaji huyo ambaye aliwahi kufanya vizuri kipindi cha nyuma na wimbo ‘Mapenzi Matamu’, alikuwa kimya kwenye muziki kwa muda mrefu akijaribu kuachana na matumizi ya dawa za kulevya ambazo zlimuathiri kwa kiasi kikubwa.
Akiongea  wiki hii akiwa mwenye siha njema, Ray C amedai anachokifikiria kwa sasa katika maisha yake ni muziki na siyo mapenzi.
“Mimi sina mpenzi,” alisema Ray C “Kwa sasa nafikiria kuhusu muziki wangu sitaki kujichanganya na mambo mengine. Mashabiki wangu wamenipambania kwa muda mrefu siyo kwaajili ya mpenzi wangu, wao wanataka kazi, muziki mzuri,”
Muimbaji huyo ambaye anafanya kazi chini ya Wasafi.Com ya Diamond Platnumz anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Unanimaliza’.
Katika hatua nyingine muimbaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwaajili ya albamu yake mpya.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment