Hatimaye Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeipokonya pointi tatu
Simba SC, ilizokuwa imepewa kutoka kwa Klabu ya Kagera Sugar.
Awali, Simba ilikuwa imepewa ushindi wa mezani wa pointi tatu na
magoli matatu dhidi ya Kagera Sugar, baada ya mchezo wake na timu hiyo
ya mkoani Kagera kumalizika ikiwa imepigwa magoli 2-1.
Ushindi huo wa mezani ulitokana na malalamiko kuwa Kagera Sugar
ilimchezesha mchezaji aliyekuwa na kadi tatu za njano, hivyo hakuwa na
sifa za kushiriki mchezo huo kwa mujibu wa kanuni na sheria za Soka.
Akitangaza uamuzi wa kurejesha matokeo ya awali ya uwanjani leo
katika ukumbi wa Habari wa TFF, Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Selestin
Mwesigwa alisema kuwa sababu zilizopelekea Kamati kuchukua uamuzi huo,
ni pamoja na kucheleweshwa kwa malalamiko ya Simba SC dhidi ya Kagera
Sugar, Simba kushindwa kulipia ada ya rufaa dhidi ya maamuzi ya mechi
hiyo na kukosekana kwa uhalali wa Kamati ya Saa 72 kwa kuwahusisha
wajumbe waalikwa ambao hawakuwa na sifa za kuwa kwenye kamati hiyo.
Kutokana na uamuzi huo, Simba imeendelea kuwa kileleni mwa Ligi Kuu
Tanzania Bara (VPL), ikiwa na pointi 59 badala ya 62 za awali.
Hali hiyo inawapa nafuu ya kupumua watani wao wa jadi, Young
Africans ambao wana pointi 56 huku wakiwa na michezo miwili nyuma ya
Simba FC.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment