Moto aliouwasha Mwenyekiti wa Kamati teule ya Bunge iliyochunguza sakata
la Richmond, Dk Harrison Mwakyembe, umemuibua mwanasiasa mkongwe
nchini, Philemon Ndesamburo.
Ndesamburo ambaye ni miongoni mwa waasisi wa mageuzi nchini, alisema Dk
Mwakyembe alificha baadhi ya taarifa za sakata hilo ili kuilinda
Serikali na mhusika mkuu.
Kauli ya Ndesamburo aliitoa jana, wakati akizungumza na waandishi wa
habari, kuhusu kauli ya Dk Mwakyembe aliyoitoa Bungeni hivi karibuni,
akitaka wanaohoji suala la Richmond walirudishe bungeni.
Bila kumtaja mhusika huyo mkuu, Ndesamburo alisema Dk Mwakyembe ni mtu
asiyeeleweka, asiye na msimamo na mwenye ndimi mbili katika suala moja
lenye mazingira yanayofanana. “Dk Mwakyembe alisoma ripoti yake bungeni
ikiwa na maelezo ya upande mmoja pasipo kumhoji mtu aliyemtaja kama
mhusika mkuu wakati anajua vizuri sheria. Natural justice (haki ya
asili) inataka umpe nafasi mtu ya kusikilizwa kabla ya kufikia uamuzi,
pamoja na kubobea katika sheria, Dk Mwakyembe hakumhoji Edward Lowassa.
Sakata la Richmond liliibuka upya Bungeni wiki iliyopita, baada ya
Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari kumtuhumu Dk
Mwakyembe kwa kutomtendea haki Lowassa, aliyekuwa Waziri Mkuu na
alijiuzulu kutokana na sakata hilo.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment