Friday 28 April 2017

Man City na United ngoma nzito EPL.

Usiku wa jana uliona mchezo mmoja mkubwa wa ligi kuu ya Uingereza – Mchezo huo,ambao ulikuwa ukitazamwa na mashabiki wengi duniani uliwaona Manchester City wakiwakaribisha majirani zao Man-United katika uwanja Etihad.

Tofauti na matarajio ya mashabki wengi, mpaka dakika 90 kukamilika, timu hizo zilitoka sare ya kutofungana.

Katika mchezo huo, kiungo wa Manchester United, Marouane Fellaini-Bakkioui, alipewa kadi nyekundu kwenye dakika ya 84 ya mchezo, kwa kosa la kumpiga kichwa Sergio Aguero. Wakati huo huo, katika dakika ya 83 Fellaini alipewa kadi ya njano kwa kosa la kumchezea rafu msambuliaji huyo [Aguero].

Kutokana na matokea hayo, Man City inaendelea kubaki katika nafasi ya nne ya msimamo wa ligi hiyo, ikiwa imejikusanyia jumla ya alama 65 katika michezo 33 waliyoicheza. Nao Man United wanaendelea kubaki katika nafasi yao ya tano wakiwa na jumla ya alama 64 katika michezo 33 waliyocheza katika ligi.

Chelsea bado wanaendelea kuongoza wakiwa wamejikusanyia jumla ya alama 78 katika michezo 33 wakifuatiwa na Tottenham Hotspur wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na alama 74.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment