Msanii wa filamu nchini Steve Nyerere amefunguka na kuweka wazi kuwa
yeye na Wema Sepetu hawana tatizo lolote na kudai yule ni dada yake
hivyo wanaheshimiana na kuendelea kuishi kama zamani licha ya Wema
Sepetu kuhama Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Steve Nyerere amesema hayo kwenye kipindi cha eNewz na kusema ni kweli
kulikuwa na matatizo hapo nyuma lakini matatizo hayo siyo sababu wao
kuharibu undugu wao na urafiki wao, hivyo ule ulikuwa ni upepo na
umepita kwa sasa wanaendelea kuishi kama zamani.
"Wema hawezi kuwa adui yangu Wema ni rafiki yangu, Wema ni ndugu yangu
hivyo yeye kuhama chama na kuhamia CHADEMA si kubadilisha urafiki, na
kuhusu matatizo na Mama Wema yule ni mama yangu kwa hiyo yaliyopita si
ndwele tugange yajayo, mimi na wewe ni ndugu yangu kabisa na
tumeshakutana mara kwa mara baada ya yale kutokea na maisha yanaendelea.
Wema na mama yake ni ndugu zangu wale siwezi kuwatupa sijakosana na mtu
Wema ni dada yangu, rafiki yangu kipenzi na mama ni mama yangu mzazi
yale yalipita ule ni upepo tu" alisisitiza Steve Nyerere
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment