Mlimbwende wa Tanzania ‘Super Model’, Asha Mabula anayekwenda
kuiwakilisha Tanzania katika shindano la dunia la urembo jijini Macau,
China jana alitambulishwa bungeni na kuzua mjadala mzito kuhusu
kuchangiwa fedha kwenda katika mashindano hayo.
Baada ya kipindi cha maswali na majibu, jana asubuhi, Mwenyekiti wa
Bunge, Andrew Chenge alimtambulisha mrembo huyo miongoni mwa wageni
waliokuwa bungeni jana.
Baadaye, Mbunge wa Urambo, Margaret Sitta alisimama kuomba muongozi wa
spika, kuhusu haja ya wabunge kumchangia fedha, walau Sh30,000 kutoka
kwa kila mmoja ili mrembo huyo aweze kusafiri kwenda China kuwakilisha
taifa.
Alisema hilo ni tukio kubwa hata timu ya taifa ilipokwenda Bungeni ilichangiwa na hivyo akatoa hoja kuomba wabunge wamchangie.
Kutokana na hoja hiyo, Mwenyekiti Chenge alitoa fursa kwa wabunge
kujadili suala hilo kwa ufupi na wakatikea baadhi ya wabunge wakipinga
huku wengine wakiunga mkono.
Akichangia hoja hiyo, Cosato Chumi wa Mufindi Mjini, alisema hoja ya
Sitta ilikuwa ya msingi na kuwa umekuwa utamaduni wa kawaida kwa wabunge
kuwachangi wanamichezo wanaofanya vizuri na kutembelea bunge.
Alisema hata timu ya taifa ya vijana ilipotembelea Bunge na mwanariadha
Felix Simbu walichangiwa, hivyo Mama Sitta aungwe mkono na kumchangia
mlimbwende huyo.
Mbunge wa Viti Maalumu, Martha Mlata alisema wabunge wanapata kadi
nyingi za kuchangia mambo mbalimbali zikiwamo harusi na wanachanga na
hivyo hawakuwa na sababu ya kukataa kumchangia mrembo huyo.
Alisema anajisikia vibaya kuona wabunge wanawake ndiyo wanaoongoza
katika wanopinga kumchangia mwanamke mwenzao, alipendekeza anayetaka
kuchanga achange na asiyateka aache.
Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy aliungana na Mlata akusema kuwa
anayetaka kuchanga afanye hivyo asiyetaka aache na kuwa yeye ni mmoja
ambaye hatachanga.
Mbunge wa singida mashariki, Tundu Lissu alisema ni jambo jema sana
kumchangia Mrembo, lakini wananchi wa jimbo lake wana njaa na Rais John
Magufuli amekataa katakata kutoa chakula cha msaada, hivyo ni bora
kuwachangia wenye njaa na huyo mlimbwende asubiri.
Ally Salehe, mbunge wa Malindi alieleza kumshangaa mbunge aliyesema
wanawake wawe na huruma, huku akihojia mbona hawakuwa na huruma na
kupotea kwa Ben Sanane, jambo ambalo Mwenyekiti Chenge alimkataza
akitaka ajielekeze kwenye hoja iliyoko mezani.
Baada ya mjadala huo, Chenge aliamua kuwahoji wabunge huku zikisikika
sauti mbalimbali na kushindania suala hilo, lakini alipowahoji alisema
anaamini walioafiki kumchangia mlimbwenda huyo wameshinda.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment