Rais Dk. John Pombe Magufuli, leo amewaongoza Watanzania katika maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Wakati
akihotubia Rais Dokt. John Magufuli amewasii watanzania kuendelea
kudumisha na kuimarisha Muungano baina ya Tanzania na Zanzibar ulijengwa
na waasisi wa taifa hili huku akisisitiza kuwa atakayethubutu kujaribu
kuvunja Muungano huo atavunjika yeye.
Rais Magufuli ameyasema hayo pindi alipokuwa anahutubia wananchi katika kilele cha maadhimisho ya sherehe za Muungano zilizofanyika kwa mara ya kwanza katika uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma kwa kusema kila mtanzania anaowajibu wa kulinda Muungano uliopo na kusisitiza kwamba njia pekee ya kuulinda ni kuchapa kazi kwa bidii.

"Mimi na mwenzangu Dkt.
Shein tutafuta nyayo za wenzetu waliotutangulia kulinda Muungano huu kwa
nguvu zote.... Asitoke mtu yoyote akajaribu kutaka kuuvunja Muungano
wetu maana atavunjika yeye". Alisema Rais Magufuli
Pamoja na hayo, Rais Magufuli amesema kupitia Muungano kuna mafanikio
mengi yamepatikana kutoka na juhudi za viongozi wa taifa na waasisi wa
Muungano huo huku akipiga kijembe kwa kusema 'ukiona vyaelea ujue
vimeundwa'Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment