Kikosi cha klabu ya Simba SC kinatarajia kutua Jijini Dar es salaam
kikitokea Mkoani Morogoro, ambapo kiliweka kambi ya takribani siku 3
kujiweka sawa dhidi ya Matajiri wa Dar es salaam, klabu ya
wanalambalamba Azam Fc katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la
shirikisho, ikiwa ni mchezo utakaochezwa siku ya jumamosi katika Uwanja
wa Taifa Dar es salaam.
Kwa upande wao, Azam FC ambayo inaendelea na maandalizi makali kuelekea mchezo huo ili kuhakikisha inatinga fainali kwa kuichapa Simba, itashuka dimbani katika mechi yake ya 26 ya mashindano dhidi ya wekundu wa msimbazi.
Kikosi cha Azam FC kipo kwenye hali nzuri kuelekea mchezo huo, na itanufaika na urejeo wa wachezaji wake kadhaa ambao waliokuwa majeruhi, jambo ambalo limeongeza morali kikosini na kila mchezaji akiwa na hamu ya kufanya vyema kwenye mtanange huo ili kuibeba timu hiyo na kusonga mbele.
Wachezaji wanaorejea ni nahodha John Bocco ‘Adebayor’, mabeki Aggrey Morris, Yakubu Mohammed na kiungo Stephan Kingue, ambao kwa sasa wanaendelea na mazoezi na wenzao. .
Itakumbukwa kuwa hiyo ndio nafasi pekee iliyobakia kwa mabingwa hao wa Ngao ya Jamii na Kombe la Mapinduzi msimu huu ya kukata tiketi kushiriki michuano ya Afrika mwakani, ambapo ikiingia fainali itakuwa imetanguliza mguu mmoja kwenye kuwania nafasi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.
Hadi inaingia fainali, Azam FC ilizitoa Cosmopolitan (3-1), Mtibwa Sugar (1-0) na kwenye robo fainali iliichapa Ndanda mabao (3-1).
BY HAMZA FUMO
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment